Rais Samia aitisha Baraza la Mawaziri kwa dharula, kujadili ajali ya ndege ya Precision

Rais Samia aitisha Baraza la Mawaziri kwa dharula, kujadili ajali ya ndege ya Precision

Watu wanakufa kila uchao kwa ajali za magari lakin ndege tu kikao cha dharula
 
Ni uamuzi muhimu sana na umma unastahili kufahamu kama nchi hii ina mipango yoyote ya uokozi au hakuna kabisa kama ilivyodhihirika katika ajali hiyo ya ndege, na ajali nyingi zilizotangulia.

Fikiria abiria wamekufa siyo kwa sababu ya maji wala siyo kwa sababu ya crush, bali kwa sababu ya kukosa hewa. Na wakati huo zaidi ya theluthi mbili ya ndege ikiwa nje juu ya maji. Watu wamekufa kwa sababu walio wazima, wameshindwa hata kutengeneza matundu madogo tu ya kuwaingizia hewa!! Huu ni uuaji wa binadamu wenzetu.

Wakisema tu kuna wapinzani wamekutana mahali fulani, mara moja polisi na usalama wa Taifa wamefika kuwatawanya, tena ni watu wasio na madhara ya kiusalama kwa yeyote. Lakini tukio linalohitaji kuokoa maisha ya wenzetu, masaa matatu hakuna chombo chochote cha Serikali kilichofika kufanya uokozi. Ni wavuvi wenye vifaa duni, ndio angalao walijitahidi sana kufanya uokozi na kufanikiwa kuokoa wachache.

Ndege iliyotua kwenye mto kule US, abiria wote 155 waliokolewa ndani ya dakika 24, sisi masaa 3, hakuna ushiriki wa Serikali katika uokoaji lakini kwa maneno, tuna vitengo vyote vya uokoaji.

Kwa nchi za wanaoheshimu dhamana na wajibu, ilitakiwa Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Wakuu wa idara za uokoaji na maafa, wawe wamekwishajiuzulu au wawe wamefukuzwa zamani. La sivyo, watu wangekuwa wapo barabarani wakiandamana kudai uwajibikaji wa wahusika. Sisi hapa kwetu tunaandamana mitandaoni maana huko nje, hawa waliowaacha ndugu zetu wafe kwa kukosa hewa, wapo standby wakati wote kuwavunja miguu hata vichwa watakaoandamana kuhoji uwajibikaji wao. Hili la kuwabonda wanaohoji uwajibikaji wao ndilo walilojipa kjwa ndiyo jukumu lao kuu.
Hii ndio ajali ya kwanza kutokea Tz? Waziri mkuu yupi amewahi kujiuzulu kwasababu ya ajali? Acha fitna, umeme haueleweki, maji hakuna, uchumi hovyo kila kitu kimepanda bei, vifurushi vya simu kadhalika, wapi umesema mikamba, michemba na yule mwenye tumbo kubwa kama kameza kibanda cha simu wawajibike kwa kujiuzuru? Una maslahi gani na kujiuzuru kwa PM?
 
Rais Samia Suluhu ameitisha kikao cha dharula na baraza la mawaziri kujadili ajali ya ndege ya precison iliyobeba uhai wa watu 19. Wakati ajali inatokea Rais Samia alikuwa nchini Misri.

Mara ya mwisho baraza la mawaziri kuitishwa kwa udharula huu ni miaka ya 90.

=====

President Samia Suluhu Hassan has convened an emergency meeting on November 14 in the capital Dodoma.

The meeting will involve cabinet ministers to discuss the Precision Air plane crash that claimed the lives of 19 people.

Samia was in Egypt immediately after the tragedy, meaning she didn't participate in the national funeral service.

The emergency meeting comes hot on the heels of calls from the public for government to be answerable for the lack of proper rescue strategy.

The last time such an emergency cabinet meeting was called by a president was in the 1990s, and it led to major changes.

An investigation into the plane crash is underway.

Citizen
Mtu nabebeshwa gunia la misumari muda si mrefu.
 
Na mnasimama kabisa majukwaani mnawasifu wavuvi kuokoa watu, hamuoni albu hata kidogo? Kwa mtiririko wa matukio haionekani hata sehemu moja ambayo msaada ulitoka Serekalini au airport wakati wa uokozi! Hii ni mbaya sana!
Tuko vizuri kwenye kuandaa mikushanyiko yenye mbwembwe nyingi kuliko utendaji, bado nina mashaka na yale maonyesho ya vifaa 9.12.annually, labda tupime uwezo wetu na jirani mmoja
 
Waongelee na nini kimetokea maana bundles zimepanda bei ghafla
 
Nyie watu!
Hivi hamjui nafasi ya usafiri wa ndege ni kubwa mno kwa uchumi na ustawi wa Tz. Na Hasa ukizingatia "watalii na washirika waletao miradi kutoka nje ya nchi "wanavyochangia uchumi wetu na maendeleo yetu"
Au hamwelewi hilo? Tutakuja kususiwa na kuachwa pembeni!
 
Back
Top Bottom