Ni uamuzi muhimu sana na umma unastahili kufahamu kama nchi hii ina mipango yoyote ya uokozi au hakuna kabisa kama ilivyodhihirika katika ajali hiyo ya ndege, na ajali nyingi zilizotangulia.
Fikiria abiria wamekufa siyo kwa sababu ya maji wala siyo kwa sababu ya crush, bali kwa sababu ya kukosa hewa. Na wakati huo zaidi ya theluthi mbili ya ndege ikiwa nje juu ya maji. Watu wamekufa kwa sababu walio wazima, wameshindwa hata kutengeneza matundu madogo tu ya kuwaingizia hewa!! Huu ni uuaji wa binadamu wenzetu.
Wakisema tu kuna wapinzani wamekutana mahali fulani, mara moja polisi na usalama wa Taifa wamefika kuwatawanya, tena ni watu wasio na madhara ya kiusalama kwa yeyote. Lakini tukio linalohitaji kuokoa maisha ya wenzetu, masaa matatu hakuna chombo chochote cha Serikali kilichofika kufanya uokozi. Ni wavuvi wenye vifaa duni, ndio angalao walijitahidi sana kufanya uokozi na kufanikiwa kuokoa wachache.
Ndege iliyotua kwenye mto kule US, abiria wote 155 waliokolewa ndani ya dakika 24, sisi masaa 3, hakuna ushiriki wa Serikali katika uokoaji lakini kwa maneno, tuna vitengo vyote vya uokoaji.
Kwa nchi za wanaoheshimu dhamana na wajibu, ilitakiwa Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Wakuu wa idara za uokoaji na maafa, wawe wamekwishajiuzulu au wawe wamefukuzwa zamani. La sivyo, watu wangekuwa wapo barabarani wakiandamana kudai uwajibikaji wa wahusika. Sisi hapa kwetu tunaandamana mitandaoni maana huko nje, hawa waliowaacha ndugu zetu wafe kwa kukosa hewa, wapo standby wakati wote kuwavunja miguu hata vichwa watakaoandamana kuhoji uwajibikaji wao. Hili la kuwabonda wanaohoji uwajibikaji wao ndilo walilojipa kjwa ndiyo jukumu lao kuu.