Rais Samia aitisha Baraza la Mawaziri kwa dharula, kujadili ajali ya ndege ya Precision

Rais Samia aitisha Baraza la Mawaziri kwa dharula, kujadili ajali ya ndege ya Precision

Rubani hakuweza kuuona vizuri uwanja wa kutua ndege wa Bukoba kwa sababu ya giza lililosababishwa na hali ya hewa. Kwa nini taa za uwanja hazikuwashwa au umeme wa tanesco ulikuwa umekatika kama kawaida yake? Kama uwanja haukuwa na taa, ni wizara gani ilizembea?
 
Hii ishu sio ndogo kama watu wengi wanavyoichukulia. Nia aibu sana kwa Taifa.

Waziri Mkuu wangu sikusemi kwa ubaya ila unatakiwa uwe ngangari sana. Ni aibu sana kwa karne hii ndege inaanguka mita 100 kutoka airport unashindwa kuokoa watu. Tena inaangukia kwenye maji!

Na mnasimama kabisa majukwaani mnawasifu wavuvi kuokoa watu, kwa mtiririko wa matukio haionekani hata sehemu moja ambayo msaada ulitoka serekalini au airport wakati wa uokozi! Hii ni mbaya sana!
.
 
Rais Samia Suluhu ameitisha kikao cha dharula na baraza la mawaziri kujadili ajali ya ndege ya precison iliyobeba uhai wa watu 19. Wakati ajali inatokea Rais Samia alikuwa nchini Misri.

Mara ya mwisho baraza la mawaziri kuitishwa kwa udharula huu ni miaka ya 90.

=====

President Samia Suluhu Hassan has convened an emergency meeting on November 14 in the capital Dodoma.

The meeting will involve cabinet ministers to discuss the Precision Air plane crash that claimed the lives of 19 people.

Samia was in Egypt immediately after the tragedy, meaning she didn't participate in the national funeral service.

The emergency meeting comes hot on the heels of calls from the public for government to be answerable for the lack of proper rescue strategy.

The last time such an emergency cabinet meeting was called by a president was in the 1990s, and it led to major changes.

An investigation into the plane crash is underway.

Citizen

Ajali ilitokea lini? Hicho kikao cha dharura ndo kinaitishwa leo? Ingekuwa dharura kwanza asingeenda Misri badala yake angeitisha hicho kikao wakati huo.

MaCCM ndo yalivyo!
 
Kuna watu wanawajibika hapo
Tatizo letu wahusika ni wazembe sana wa kufuatilia mambo mpaka sisi wananchi wa kawaida tunaanza kutunga yetu

Inatakiwa sisi tupewe Habari kadiri zinavyotokea na sio kusubiri siku kadhaa ndio serikali inatoa majibu

Rais ana haki ya kukutanana nao maana wamekuwa waongo kwa taarifa kibao
Mwanzo walikurupuka wakasema ni hali ya hewa
Halafu tena Habari zinazunguka kuwa matairi yaligoma kutoka

Piga chini safu nzima Mheshimiwa Rais
Well Noted Mkuu....
 
Mazoezi ya utayari, Uwepo wa Zana na Vifaa vya Uokozi, Weledi wa Wanaovitumia pia bajeti ya fedha

Mazoezi ya utayari ya jeshi la Zimamoto na Uokozi, Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoa, Magari ya Wagonjwa / Majeruhi (ambulance), Ma Engineer, Vikosi vya Ulinzi na Usalama n.k kukabiliana na majanga yaonekane yakitumiwa pindi kukitokea ajali ya aina yoyote

Mafunzo wanayopitia cabin crew ili kujua cha kufanya kunapotokea ajali, mfano ndege kutua ktk maji n.k

SIMULATION YA NDEGE KUISHIWA MAFUTA NA KUAMUA KUTUA KARIBU NA FUKWE YA BAHARI, HUKU CABIN CREW, FIRST OFFICER, CAPTAIN WAKISIMAMIA ZOEZI

Mafunzo ya wafanyakazi wa SAA la Afrika ya Kusini, mafunzo haya mashirika yote duniani hulazimika kuyafanya kila wakati yaani mazoezi ya utayari.

Mamlaka mbalimbali FAA, ICAO, TCAA Tanzania, mashirika ya ndege yote yanabanwa kuhakikisha mafunzo haya ya utayari hufanyika mara kwa mara ili wafanyakazi wote ndani ya ndege wawe na utayari wakati wa dharura ikitokea.

CABIN CREW TRAINING: DITCHING - LONG (FULL) PREPARATION

SAA Cabin Crew CRM and procedures training: Cabin preparation when there is more than 10 minutes available to prepare the cabin.

Isambazwe katika mitandao yote. Ni muhimu kuiangalia hii klip kabla hujapanda ndege, na kurudia mara kwa mara kuiangalia.

Hata kwa wasiopanda ndege ni muhimu vilevile kuiangalia, hujui itakufaa lini pengine utakuwa muokoaji ajali inapotokea. Nawasilisha.
 
Rubani hakuweza kuuona vizuri uwanja wa kutua ndege wa Bukoba kwa sababu ya giza lililosababishwa na hali ya hewa. Kwa nini taa za uwanja hazikuwashwa au umeme wa tanesco ulikuwa umekatika kama kawaida yake? Kama uwanja haukuwa na taa, ni wizara gani ilizembea?
Uwanja hauna taa
 
Hakuna kitu kipya CCM inaweza kudeliver kwa nchi hii.. HAKUNAAA
 
Swala la ajali ya ndege yenye abiria 48 linapataje umuhimu kuliko swala la maji linalowatesa Watanzania ndani na nje ya Dar? Kwangu la maana ni kutoka na jibu la kutengeneza vyanzo vingine vya maji si kila siku Ruvu chini na Ruvu juu
Kwasababu hakuna takwimu za vifo/magonjwa vinavyosababishwa na ukosefu wa maji. Ni tatizo lililo nyuma ya pazia.
 
Ndege 3 katika ya 4 ilizonazo aina ya airbus a220-300 za shirika la ndege la Air Tanzania haziruki na kubaki zimepaki kutokana na tatizo la engine linalofahamika duniani kote hivyo ATCL nayo imesitisha kurusha ndege aina ya a220-300 hadi hapo ufumbuzi utapopatikana

Air Tanzania Suspends Services As Most Of Its Airbus A220s Are Grounded​

BYJAKOV FABINGER
PUBLISHED 1 DAY AGO

Three out of Air Tanzania's four Airbus A220s are not flying at the moment.


Air Tanzania has announced a temporary suspension of some of its services because of the ongoing technical problems with the Pratt & Whitney engines on some of its Airbus A220s. The East African airline does not have a target date by which it hopes to resolve this issue, so half of its A220 fleet remains grounded for the foreseeable future ........
Source : Air Tanzania Suspends Services As Most Of Its Airbus A220s


Mkuu kwani tuna;
1. Bombadia ngapi?
2. Dreamliner ngapi?
3. Airbus ngapi?

Nasikitika hizi ndege kuwa na engine mbovu kwani ukizipanda ni tamu sana pamoja na dreamliner.
Bombadia zina vikelele flani na kuyumba angani
 
Swala la ajali ya ndege yenye abiria 48 linapataje umuhimu kuliko swala la maji linalowatesa Watanzania ndani na nje ya Dar? Kwangu la maana ni kutoka na jibu la kutengeneza vyanzo vingine vya maji si kila siku Ruvu chini na Ruvu juu
Wanatuyumbisha tu akili.
 
Huu ni mwanzo mzuri wajadili pia na namna ya kukabiliana na majanga kwa haraka endapo yatatokea kama haya huko mbele.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
"Yaliyopita si ndwele tuganage yajayo "
kauli hii hawezi kuelewa mfiwa. waliopewa dhamana wawajibishwe
 
Mazingira ya wahuni kumuondoa waziri mkuu ili wamuweke mtu wao waendelee kula nchi yanaandaliwa. Bei ya bidhaa kupanda/Mgao maji/Umeme pia si dharura??

Waziri mkuu aliyeko madarakani kwa wizi wa kura sio muhuni? Bidhaa zimepanda yeye akiwa waziri mkuu, sasa kuna ajabu gani akitolewa?
 
Si wameshachukua hatua kupitia kipimajoto sijui malumbano ya hoja itv? Maana tumeona kina Kova sijui wana kampuni za uokoaji na kina Mbatia wataalamu wa majanga wakilumbana kwenye iko kipindi lakini hawakukimbilia eneo la tukio ili waokoe watu siku hiyo!
 
Huu ni mwanzo mzuri wajadili pia na namna ya kukabiliana na majanga kwa haraka endapo yatatokea kama haya huko mbele.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Hatukujifunza kwenye ajali ya Mv Bukoba ikatokea tena ziwa Victoria ajali ya kivuko MV Nyerere.
Hatukujifunza kwa Ajali ya Treni Morogoro. Hagukujifunza kwenye ajali ya moto Idweli Mbeya, ikatokea ajali ya namna ileile Morogoro

Majanga yote haya na mengine mengi bado hayajaacha somo kwenye akili za viongozi wa nchi hii na sisiyemu yao. Kazi ulafi tu
 
Tena katika nchi ambayo viongozi huteuana kwa misingi kujuana! Badala ya sifa za mtu za kielimu, uadilifu wake, na pia uzoefu wake katika utendaji wa kazi!!

Kwa kweli hata mimi sitegemei kusikia tamko lenye uwajibikaji ndani yake.
Kwani Kuna kiongozi hapa duniani huteu Watendaji usio wajua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhimu Mawaziri waangazie na kujadili mambo yafuatayo:
1. Hali ilivyo kwa sasa kuhusu majanga na uokoaji. Wawe wakweli kuhusu hali halisi,weledi,vifaa, wataalam, magari na mfumo mzima na changamoto zake
2. Sera,sheria na kanuni,miongozo na mifumo waone kama inakidhi matarajio na inaenda na mabadiliko ya teknolojia na aina na ukubwa majanga na complexity zake.
3.tumejifunza nini kuhusu majanga mbalimbali 1961-2023,udhaifu na changamoto
4.uwezo wa kitaasisi kukabiliana na majanga
5.uwekezaji binafsi na kiserikali kwenye kukabiliana na majanga
6. Uratibu
7.elimu kwa wananchi
8. Predictions....Kwa baadaye nini kifanyike kuhusu majanga ya majini,ardhini, tetemeko,ajali za mageri,treni,moto migodini, ndege nk. Tuje na suluhisho pro active.
Vinginevyo tusikimbilie kufikiria nani anaachia ngazi PM,KAMISHNA ZIMA MOTO,MAMBO YA NDANI, UJENZI etc So far taarifa ya uchunguzi haijatoka tujue chanzo cha ajali hasa ni ndege, kiwanja,control tower, Tujikite kwenye mitigation zaidi na yanayoonaka kwa macho ya kiuzembe vinginevyo likiisha hili linakuja lingine utamaliza watu,tunahitaji mikakati ya muda mfupi na mirefu na yenye mbinu za kisasa.
 
Back
Top Bottom