Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

BF361AC7-DF29-4C56-8CF9-34E66AEE2655.jpeg
 
Great..sio tu kushusha bei ya mafuta bali wabuni (actually Waige ) mbinu za kuweza kustabilize price za mafuta nchini on long run, sio wakisikia tu bei imepanda soko la dunia ndani ya masaa yameshapanda bei mpaka ushirombo 🤔 makampuni yote Makubwa ya mafuta duniani Total, BP, Shell yametangaza faida ya kutupa kutokana na price ya mafuta kupanda ghafla kutokana na speculations za ovyo.
 
Hivi makamu yuko wapi mbona anakosa kwenye vikao muhimu Kama hichi?

Isitoshe alishawahi kuwa waziri wa fedha, hivyo anaufahamu mzuri sana juu ya uchumi Sasa anakosaje kwenye swala Kama hili!
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

View attachment 2217431
Tutarajie kushuka kwa bei ya mafuta.
 
Hivi makamu yuko wapi mbona anakosa kwenye vikao muhimu Kama hichi..?
Isitoshe alishawahi kuwa waziri wa fedha,hivyo anaufahamu mzuri sana juu ya uchumi Sasa anakosaje kwenye swala Kama hili!
Yupo msibani itakuwa hajarudi
 
Hii siyo vizuri kwa afya ya mkuu wa nchi.

Mheshimiwa angewapa dondoo wasaidizi wake ambao ni mawaziri wenye dhamana wampatie taarifa na mapendekezo yao ifikapo kesho asubuhi juu ya kupata jibu la kutatua kadhia hii.

Kazi ingekuwa mawaziri husika pamoja makatibu wakuu kujikusanya usiku huu pamoja na makamishina, wakurugenzi na wataalamu kutafuta jibu muafaka.
 
Back
Top Bottom