Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Great..sio tu kushusha bei ya mafuta bali wabuni (actually Waige ) mbinu za kuweza kustabilize price za mafuta nchini on long run, sio wakisikia tu bei imepanda soko la dunia ndani ya masaa yameshapanda bei mpaka ushirombo 🤔 makampuni yote Makubwa ya mafuta duniani Total, BP, Shell yametangaza faida ya kutupa kutokana na price ya mafuta kupanda ghafla kutokana na speculations za ovyo.
Namashaka kama wa uwezo huo. Wangekua nao wasingekurupuka “this late in the game”
 
mbona kikao hakina gender balance, anyway, twahitaji mikakati endelevu kuivusha nchi katika mambo yasiyohitaji mihemkoo
 
Rais Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo Mei 8, 2022 Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati ,January Makamba, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

Mwananchi
 
Waafrika tunapenda sana kula imagine kikao serious kama hicho kimejaa machupa na majuisi sijui makorosho kwani wangekula baada ya kumaliza ingekuwaje? Hatuko serious kabisa kila sehemu tunawaza kula kula hovyo tu.

Na si ajabu wakala na kuvimbiwa na wakashindwa kuja na SULUHU la mfumuko wa Bei 😌
 
Hivi makamu yuko wapi mbona anakosa kwenye vikao muhimu Kama hichi..?
Isitoshe alishawahi kuwa waziri wa fedha,hivyo anaufahamu mzuri sana juu ya uchumi Sasa anakosaje kwenye swala Kama hili!
Alibaki JNCC anaangalia Royal Tour episode two...walikua wote kabla kwenye episode one whole day
 
1.Mbinu za kukuza uchumi.
2.Kupunguza makali ya maisha.
Kila uchao maeneo hayo mawili ,majibu na mikakati inasuasua.
 
Rais Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo Mei 8, 2022 Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati ,January Makamba, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

Mwananchi
Nikajua amewaita ili kuangalia namna,, kumbe ni maagizo kama kawaida
 
Kwa mwenye kutafakari, wamefeli mapema sana, wangeonekana wanajari wananchi kama wangekuwa wamedhibiti bei kabla hawajapigiwa kelele. Kwani wao hawana mbongo kutafakari juu ya nini maana ya mfumuko wa bei ya mafuta? Kama wasingekuwa peke yao Bungeni mule Serikali ingeisha vunjwa kama kwenye Escrow. Ndugu zangu uchaguzi ujao Tuongeze wapinzani na tukalinde kura kwelikweli ili Serikali ifanye kazi kwelikweli. Police na vyombo vingine nanyi muna ndugu zenu wanaumia je Ninyi mna kula asali?Kasimamieni haki kwenye uchaguzi ili tukajenge uwajibikaji kwenye nchi yetu na hatimae tukapate maendeleo yetu na vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom