Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

View attachment 2217431
Asante kwa taarifa.
P
 
Hii siyo vizuri kwa afya ya mkuu wa nchi.

Mheshimiwa angewapa dondoo wasaidizi wake ambao ni mawaziri wenye dhamana wampatie taarifa na mapendekezo yao ifikapo kesho asubuhi juu ya kupata jibu la kutatua kadhia hii.

Kazi ingekuwa mawaziri husika pamoja makatibu wakuu kujikusanya usiku huu pamoja na makamishina, wakurugenzi na wataalamu kutafuta jibu muafaka.
Huyu bibi hana haiba za uongozi wala maarifa.
 
Waafrika tunapenda sana kula imagine kikao serious kama hicho kimejaa machupa na majuisi sijui makorosho kwani wangekula baada ya kumaliza ingekuwaje? Hatuko serious kabisa kila sehemu tunawaza kula kula hovyo tu.
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
Waziri wa fedha ni Mwigulu Nchemba alafu unatarajia miracles.
 
Back
Top Bottom