Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Rais Samia aitisha kikao cha dharura usiku huu (Mei, 08 2022) Ikulu Dar Es Salaam kujadili mafuta

Waafrika tunapenda sana kula imagine kikao serious kama hicho kimejaa machupa na majuisi sijui makorosho kwani wangekula baada ya kumaliza ingekuwaje? Hatuko serious kabisa kila sehemu tunawaza kula kula hovyo tu.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Iz mambo za ajabu sana mchana royal tuwa, usiku kikao cha dharula kazi ipo
 
Tunaweza ku-criticize serikali kwa namna yoyote ile, ila sio kila kitu tuseme tu kwa vile we have the freedom to express our views.

Unasema swala la kutoa 920tsh sio swala la majadiliano, upo serious kweli? Every coin counts kama hujui, na kodi yoyote, ongezeko lolote linaathiri mapato ya serikali hivyo ni lazima kuangalia athari za kupunguza/kuongeza chochote

Umeongea kiustadi sana, na nikubaliane na wewe kwamba kuongoza nchi ni kazi sana na Kila maamuzi yana athari Kwa namba moja ama nyingine.

Lakini kama Hilo wanalijua, hakuna haja hata ya hicho kikao Cha dharura kama njia pekee ni kupunguza Kodi.

Kama every coin counts, wanakusanya pesa nyingi sana za tozo ambazo kimsingi hazikuwa kwenye bajeti. Na nikiri Hadi Sasa kama wananchi, hatupewi taarifa sahihi za matumizi ya hizo tozo.

Nnachotaka kusema ni kwamba, kuirusha kikao Cha dharura na kutoa maagizo tu bila kuwa na nia thabiti ya kutatua tatizo ni aina nyingine ya hadaa Kwa wananchi.

Kauli zao zimepelekea wafanyabiashara kupandisha Bei za bidhaa kama wanavyotaka. Hii yote inawaumiza wananchi.
 
Azi longi azi watu wote, wakijani, wanjano, wekundu, weupe, wadhambarau n.k wanapitia tanuru hilo hilo, waendeleze tu ujinga wao.

Zichukuliwe bara, wazenji wapunguziwe gharama za umeme, bei ya mafuta, mishahara ipande...kwamba bara uchumi wao ni mbovu kulinganisha na zenji

Jambo lenu lishakamilika, chekini na zenji
 

kikao cha dharura unaitisha Rais then unawaagiza wakatafute Suluhu sho ?​

Wewe kama Rais unatakiwa ukitisha kikao cha dharura uwe na suluhisho tena la haraka.​

Hali ya mafuta ya kula ni mbaya hata kuliko mafuta ya petrol nchini , lita moja ni Tsh 9,000 wakati petrol ni Tsh 3,341​

Kwani ni mara ya ngapi ana itisha hivi vikao?
Mwigulu kakomaa. Mafuta ya kula na bidhaa nyingine zina panda hovyo tuu. Hivi sasa sukari kilo 4000/ tuko kwenye royal tour. Mwigulu ana furajia anguko la Mama.
 
Mimi nashangaa sana, ukienda pale kariakoo hakuna mtu anajali risiti hata ukichukua mzigo wa milioni 10.

Huwezi kuwaambia wabongo walipe kodi kwa hiari alafu utegemee watalipa.

Matokeo yake ndio haya matozo kwenye simu na mafuta.

Ukiona kiongozi anabuni matozo ya hovyo kama haya ya kwenye simu ujue kashindwa kukusanya kodi kunakostahili
Huwezi kukusanya kodi toka kwa wafanyabiashara wanao kufadhiri mambo yako!! Ndio maana hawatoi orodha ya wafadhiri wa Royal Tour!
 

Watanzania tusipoweza kutofautisha Degree za university of Dar Es Salaam na za Open university Samia atatusumbua sana .​

 
Upumbavu mtupu,ndo shida ya kuongozwa na mtu alie unga unga elimu.

Kwanza yeye alituambia vitu vyote vitapanda bei sababu ya mafuta kupanda bei,alikuwa wapi hapo awali wakati akisema hayo maneno kutafuta suluhisho? Sasa hivi wananchi wameumia vya kutosha ndo anajifanya kuitisha kikao,huu ni upumbavu wa hali ya juu.

Kiongozi wa Taifa huwezi toka hadharani kusema kila kitu kitapanda bei,mafuta yatapanda bei huku ukijuanwafanya biashara wa Tanzania huwa wanasubiria palipo na weaknesses wanapitia hapo,badala ya kutafuta suluhisho wewe kila siku wimbo ni ule ule,vitu vitapanda bei! Jitafakari sana wewe Dada kama hicho kiatu kinakutosha,kama kinakupwaya sio lazima uongoze,sifa ya kuwa Rais tayari unayo,is better you quit out of the state house,Nalog out!
Alisema Rais hakosei
 
Kama wanavuka lengo kwanini wanazidi kuongeza matozo kwenye bidhaa?

Ona matozo ya kwenye simu,!.. Ona ya kwenye mafuta!

Makamba akaja na ngonjera eti tumefuta sh 100 ya tozo kwenye mafuta, mamako akapiga kelele hoo hiyo tulishaipangia bajeti, kwanini hiyo inayovuka lengo hapo TRA isifidie?

Hamna rais hapo.
Na mama'ko akafa kwa njaa kwa kuwa hukuweza kumpa kula yake? Na wewe ukasema mama'ko kafa kwa njaa kwa sababu vitu vimepanda bei, au siyo?
 
Hivi makamu yuko wapi mbona anakosa kwenye vikao muhimu Kama hichi..?
Isitoshe alishawahi kuwa waziri wa fedha,hivyo anaufahamu mzuri sana juu ya uchumi Sasa anakosaje kwenye swala Kama hili!
Kachoka, alikuwa kwenye Royal Tour
 
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
 

Attachments

  • IMG_0300.MP4
    2.2 MB
Rais Samia ameitisha kikao ikulu udiku huu kujadili kupanda kwa bei ya mafuta , huku kikao hiko kikihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati January Makamba, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata na wajumbe wengineo

Tutarajie tamko la namna gani baada ya kikao hiko ndugu mdau wa jamii forums?

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

View attachment 2217468
Basi wafikie maamuzi manake nchi hii sasa hivi kila mtu analalamika, wananchi wanalalamika, wabunge wanalalamika,waziri nishati ndio kabisa hata hajui afanye nini anaishia kulalamika na mh Rais tena sijui tusemeje manake yy anaona sawa mara aseme (vita ya Ukraine na Russia ,mara bei ya mafuta ya tz ni stahimilifu ukilinganisha na US) yaani yy mwenyewe hata haelewi afanye nini.

Wote wanalamika, sasa hapa ndipo Mwendazake anapo jichukuliaga points 3,hawa walio kuwepo ni mwendo wa kulalamika wanashindwa kufanya maamuzi sasa sijui wanamuogopa nani au kwenye issues ya mafuta kuna maslahi yao wana ya linda.
 
Kama boss wa TRA yupo,tutegemea kuondoa au kupunguza Kodi/ushuru wa forodha kwenye bidhaa za mafuta.Gharama ya mafuta (CIF value ya petrol) ni Kati ya Shs 1,680-Shs1,800,lakini kodi mbalimbali zinafikia Shs1,340.
Serikali ipunguze au iondoe baadhi ya kodi kwa kipindi hiki cha mpito.
 
Nchi hii sasa hivi kila mtu analalamika, wananchi wanalalamika, wabunge wanalalamika,waziri nishati ndio kabisa hata hajui afanye nini anaishia kulalamika na mh Rais tena sijui tusemeje manake yy anaona sawa mara aseme (vita ya Ukraine na Russia ,mara bei ya mafuta ya tz ni stahimilifu ukilinganisha na US) yaani yy mwenyewe hata haelewi afanye nini.

Wote wanalamika, sasa hapa ndipo Mwendazake anapo jichukuliaga points 3,hawa walio kuwepo ni mwendo wa kulalamika wanashindwa kufanya maamuzi sasa sijui wanamuogopa nani au kwenye issues ya mafuta kuna maslahi yao wana ya linda.
 
Sio kushuka...sema tutarajie bei ya mafuta kurudi kwenye bei yake ya awali...wakifikisha sh 1,500 kwa Lita apo ndo tutasema wameshusha
Anza kujitengenezea nishati yako mwenyewe ya bure, inatokana na haja kubwa yako unayoenda kila siku, usitegemee kushuka bei ya mafuta kuliko bei ya kununulia. Njia pekee ni kuzalisha yako tu. teknolia ipo tena nyepesi sana.

Kushusha bei ya mafuta usitegemee kuwa kutakuwa kukubwa, zitachomolewa tozo tu za hapo kwnye mafuta na kwenda kubandikwa kwengine. From direct taxation to indirect taxation.

Kutumai vitu ambavyo haviingii akilini bila kuwa na njia mbadala ni ujuha. Unatakiwa uwe na njia mbadala ya kuipata nishati.


Mimi nafurahi haya yanatokea kwa kuwa ndiyo yanayofungua ubunifu "necessity is the mother of invention". Pia yanafunguwa fursa " No problems No opportunities".

Kwa hiyo mwache mama na watendaji wake wachemshe bongo tuone watakuja na lipi jipya na sisi huku nje tuchemshe bongo tuone tutakuwa na ubunifu upi mpya.

Ahsante Sheikh Kipanya kwa kuonesha mfano.
 
Hili swala sio la Kichama hili ni la Kitaifa.
 
Back
Top Bottom