Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Hongera Sana Mheshimiwa Raisi,unaupiga mwingi,unatekeleza Miradi ya Maendeleo na kuangalia masilahi ya watumishi.
Hongera Sana mama, wewe hujasubiri Miradi ikamilike ndiyo upandishe mishahara.
Mama Wastaafu hujawasahau,umeridhia kikokotoo kilichopendekezwa na tucta wakati wa Mei mosi 2022.

Utekelezaji

1.Watumishi wa Serikali kada ya operation na mikataba walikuwa wanachangia mfuko wa NSSF,na NSSF wao walisha-adopt kikokotoa cha 25% kinyemela kabla watumishi wa Serikali wanaochangia PSSSF kugomea kikokotoa cha 25%' kwa malipo ya mkupuo mmoja.
2.watumishi wa Serikali waliolipwa wanaochangia PSPF wamekuwa wanalipwa malipo ya mkupuo ya asilimia 50.

Ushauri
1. Kikokotoo Cha asilimia 33 kitumike kwa watumishi wote wa Serikali regardless ulichangia mfuko gani
2.Kwa watumishi wa Serikali waliolipwa 25 mfuko wa NSSF iwalipe tofauti.
3.kama ikikupendeza watumishi wa sekta binafsi na Serikali wawe wanalipwa kwa kikokotoo kimoja kwa mifuko yote miwili.
 
Kilio cha kila siku cha mkulima kuhusu mbolea kuuzwa kwa bei kubwa kupindukia unakitafakarije? Kumbuka wakulima no 98% yai watanzania.
 
Kama hujui kwa gharama za Maisha za leo ili mtumishi amudu Maisha inabidi kima cha chini kiwe millioni moja
 
Hapo watu hawajui tu! Hiyo 23% ni political issue ili kuwazubaisha wengine hapo kwa watu wa kima cha chini ni habari njema kwao! Waseme kwa uwazi ongezeko kwa wengine ni asilimia ngapi! Tofauti na hapo tutakuta ongezeko 17,000/=
 
Tafsiri yake ni kwamba Rais ameongeza 23.3% kwenye kima cha chini cha mshahara Kama kilikuwa (mathalan) 100,000 23.3% ni 23,300 i.e 123,300/-
 
Elimu yako ni level gani?
Mada nyingine sio za kuchangia wala ugoro na double kick
 
Tafsiri yake ni kwamba Rais ameongeza 23.3% kwenye kima cha chini cha mshahara Kama kilikuwa (mathalan) 100,000 23.3% ni 23,300 i.e 123,300/-
Kima cha chini kwa watumishi wa umma ni 300000

Hata kenya nyongeza inapimwa kwa kima cha chini

Watumishi wote wanaongezwa mshahara
 
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akubali ongezeko la 23.3% kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma.

View attachment 2224213View attachment 2224214

Rais Samia badala ya mtumishi kustaafu na kulipwa mafao yake kwa mkupuo sasa wanalipwa 33% na awali ilitakiwa kulipwa 25% . Watumishi hili mmelisoma au mmeambiwa 23.3% ya kina cha chini kilichoongezwa? Mkafurahia​

 
Hebu ngoja hapa:-
23.3/100=0.233
0.233×270000/= =62,910
KWA hiyo:-
270000+62910=332,910/=
KWA kima cha CHINI hicho!!
Nakaribisha masahihisho kama yapo!!
Mimi Raisi ajaye nimeona hivi KWA lima cha CHINI ya wewe je!!?
Meaning kila mtumishi ataongrzewa 62,910
 
Upo sahihi jinsi mshahara unavyokuwa
mkubwa ongezeko linapungua...Kuna watu wataambulia elfu kumi kama kwenye lile punguzo la Kodi
 
Ni kweli huna, sio ww tu karibu walimu wote hamna.
Kusoma tu hiyo document na kuelewa umeshindwa

Unatoa wapi uhalali na ujasiri wa kudharau, kukejeli na kutweza waalimu au watu mnaopishana nao uelewa?

Mie nilichoelewa kwenye hiyo taarifa, kama kichwa Cha habari kilivyo na paragraph ya kwanza, ni kwamba, Rais ameridhia ongezeko la mishahara Kwa wafanyakazi wote wa umma ( hajataja asilimia ngapi), ameweka wazi kwamba wale wa kima Cha chini ndio ongezeko lao la mshahara ni asilimia 23.3%.

Mbona na wewe unasema nyongeza ni Kwa kima Cha chini pekee lakini haujaitwa hauna akili?

Kutokuelewa jambo inaweza kuwa ujinga Kwa Mara Moja lakini sio kukosa akili.
 
Hivi ni kweli hamjui kusoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…