Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Nipo
Ila umeelewa vizuri hapo kilichoandikwa? Maana najua walimu wengi upeo ni mdogo
Kweli Aisee Walimu wengi wana upeo mdogo maana Magufuli mwenyewe alishakua ni Mwl na upeo wake tuliouona ulivyokua hafifu.
 
Hebu nisaidieni kwa mnaojua kukokotoa hizo asilimia. Kwa mfano mwenye basic salary ya 940, 000/= hiyo aailimia 23 ndio inakuwa sh. ngapi?

Piga 0.23 zidisha mara 940000 jibu utaona kama 216 yaani laki mbili na 16 ndio ongezeko lako hivo utafika kwenye milioni laki moja na hamsini hivi
 
Mwaka jana waliongeza kima cha chini kutoka 170,000/= mpaka 270,000/= lakini wale wa juu hatukuguswa.
 
Mchawi si lazima aruke na ungo
 
Kila mtu akijiajiri nani atafundisha watoto wako utakaowazaa? Vp kuhusu polisi watakaolinda biashara yako uliyojiajiri?
Huyu Jane Lowassa ni mjinga na hajielewi, achana naye...

Hajui kuwa mtu hupata mahitaji yake muhimu ya kila siku i.e chakula, mavazi, malazi (mahali pa kuishi/kulala) nk nk kwa KUFANYA KAZI. Kazi yaweza kuwa ya kujiajiri au kuajiriwa na mtu, taasisi, shirika au serikali ...


Duniani kote na nchi yoyote kuna mgawanyo wa kazi (DIVISION OF LABOUR). Haiwezekani kila mtu ajiajiri na kuwa mfanyabiashara binafsi, machinga, mkulima nk nk..

By the way, hata uwe mfanyabiashara uliyejiajiri mwisho wa siku utahitaji wafanyakazi kukusaidia kazi zako ambao ni lazima uwalipe mshahara. Hawa wafanyakazi mara kwa mara utakuwa unakaa nao mezani ku - negotiate maslahi. This is very common. Ukiwapuuza na kuwadharau shughuli zako zikwame na biashara yako inaanguka..!

Jane Lowassa, suppose kila mtu angekuwa kwenye duka/biashara yake "aliyojiajiri (kama usemavyo), nani sasa angekuwa mhasibu wake? Dereva wake? Mbeba mzigo wake? nk nk

Duniani, binadamu wote tunaishi kwa kutegemeana...

Mfanyabishara aliyejiari kama wewe Jane Lowassa unamhitaji nesi, daktari, dereva wa gari yako, mwalimu afundishe watoto wako shule, msukuma mkokoteni abebe bidhaa zako nk nk..

Si hivyo tu, bali mfanyakazi huyu mwalimu, askari polisi au jeshi, daktari, Mtendaji wa kijiji, dereva, mkatisha tiketi, mwendesha mitambo kiwandani nk nk wanapopata mishahara yao mwisho wa siku wanampelekea mfanyabiashara au mtoa huduma aliyejiajiri in exchange with goods/services...

Jane Lowassa, asikudanganye mtu. Waliojiajiri/wafanyabishara wenye akili huomba na kupigana kufa na kupona kuhakikisha mfanyakazi ana mshahara kila mwezi au kila siku tena ulioboreshwa ili wawe na uwezo kununua bidhaa au huduma zao...

Ni mfanyabishara aliyejiari mjinga pekee anayeweza kuwaponda na kuwaombea wafanyakazi na wakulima mabaya maana hiyo inakuwa ni chanzo cha kudoda kwa bidhaa au huduma zao...!!

Jane Lowassa mpaka hapo umeelewa? Au bado uko gizani?
 
Sekta binafsi ili uongezewe mshahara inabidi uongezewe kazi, ila serikalini mtu anaongezewa mshahara bila kuongezewa kazi?
Sekta binafsi output yako itafanya uongezewe mshahara au ubaki kama ulivyo, huko serikalini wao wanaongezwa tu, vigezo nadhani ni "kupanda kwa gharama za maisha". No wonder watu wengi wanapigania ajira za serikali ili "wakapumzike".
 
kwenye chapisho kumeandikwa IKIWEMO KIMA CHA CHINI kwa 23.3% hii umeelewa vipi!?.
 
Okay...

Nimekuelewa ndugu yangu...
 
Gharama za maisha hazipungui kwa kupunguza uwezo wa raia wako kufanya manunuzi tu.

Hata kuongeza matumizi ya serikali kwa mataifa mengine kama kutoa tenda, kufanya malipo makubwa nje bila kuongeza uwezo wa manunuzi kwa raia wako nako kunaongeza gharama za maisha sababu wananchi wako wanakuwa hawana pesa.

Viwanja vitauzwa hata milioni na hiyo milioni mtu hatakuwa nayo sababu hulipi mishahara na raia hawana uwezo wa maendeleo zaidi ya kula.

Unatakiwa kubalance, ukiona raia wana pesa nyingi unazipunguza, ukiona raia hawana pesa unaziongeza. Wakati mwingine gharama za maisha zinakuwa juu sababu uchumi unakuwa ni wa serikali tu bila kuhusisha wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…