Hongera kwa serikali sikivu ya JMT, hongera kwa Mhe. Rais SSH kutimiza ahadi kwa wafanyakazi wa serikalini.
Hata hivyo serikali bado kuna kazi kubwa ya kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa jumuishi kwani serikali imeajiri wafanyakazi ambao hawazidi laki 8;
Sekta binafsi (rasmiimeajiri zaidi ya mara 4.
Sekta isiyo rasmi ina nyomi ila mchango wake kwenye kukuza uchumi wa nchi iko very fragile na uncordinated na sekta ya fedha ili kukuza uzalishaji wenye tija.
Kilimo/Ufugaji/Uvuvi iko haja ikawa highly organized ili iwe na access na sekta ya fedha ili kinachozalishwa kiwe na uhakika wa soko na kuwafanya wakulima wa-benkike, wachangia NSSF na wamudu kulipia bima ya afya;
Kinachozalishwa kwenye kilimo kikiweza kuchakatwa na viwandani vya ndani kutaongeza ajira na ku-cut down imports ya consumables.
Ni aibu tuna import 90% ya ngano.
Ni aibu tuna import surgical cotton, bandage, gauze, mashuka ya hospitali na tunalima pamba na tunashindwa kuzalisha products za pamba
Ni aibu tuna import 80% ya mafuta ya kula...the list goes on
Mguso huu utaipa serikali tax base kubwa based on purchasing power ya watu na makampuni ya ndani na hawa walio sekta isiyo rasmi na kilimo hasa cha kibiashara wataipa serikali chanzo kingine cha uhakika kukusanya kuhudumia Watanzania ikiwamo mishahara na maslahi mengine ya watumishi wa umma.
Hongera Mhe. Rais SSH
#Kazi iendelee