Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Ukishapandisha Kima cha chini automatically wote wanapanda. Mshahara Ni haki ya kila mfanyakazi
Hapa kitaalamu watu wanahisi hiyo 23% itaongezeka kwenye mishahara yao [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

SEMA MAMA AMEAMUA KUWACHANGANYA SANA WATU KWA NAMBA

Kama ile 100 billions za mafuta

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mnaacha kujiajiri mnahangaika kuwa watumwa serilalini. Halafu mnashangilia nyongeza ya kimshahara wakati maisha nayo yanapanda. Mindless
Povu la nini dada? Kwamba walioajiriwa wana dhambi sana au?
Kujiajiri ni juhudi za mtu binafsi, kama ww umejajir usi kashifu ambao hawaja jiajiri?
Kama ww ni muajiriwa usikashifu waliojiajir.

Wote wanatafuta riziki tofauti ni njia tu.
 
Nashangaa mijitu inashangilia. Inamaana kuwa wale wenye mishahara ya laki mbili wataongezewa hiyo asilimia ila wenye mishahara mingine hakuna nyongeza
Kidogo watapandishwa madaraja na ni kww baadhi, ngoja washangilie..
 
Hata mimi naunga mkono ila ongezeko pia liendane na kushusha inflation maana mwisho wa siku unaweza kuongezeka elfu 80,000/= kwenye mshahara wako ambayo haitaleta impact yeyote kama maisha yataendelea kupanda!
Watu mnakufuru! Mlikaa miaka saba bila hata senti kuongezwa..
 
Hongera kwa serikali sikivu ya JMT, hongera kwa Mhe. Rais SSH kutimiza ahadi kwa wafanyakazi wa serikalini.

Hata hivyo serikali bado kuna kazi kubwa ya kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa jumuishi kwani serikali imeajiri wafanyakazi ambao hawazidi laki 8;
Sekta binafsi (rasmiimeajiri zaidi ya mara 4.

Sekta isiyo rasmi ina nyomi ila mchango wake kwenye kukuza uchumi wa nchi iko very fragile na uncordinated na sekta ya fedha ili kukuza uzalishaji wenye tija.

Kilimo/Ufugaji/Uvuvi iko haja ikawa highly organized ili iwe na access na sekta ya fedha ili kinachozalishwa kiwe na uhakika wa soko na kuwafanya wakulima wa-benkike, wachangia NSSF na wamudu kulipia bima ya afya;
Kinachozalishwa kwenye kilimo kikiweza kuchakatwa na viwandani vya ndani kutaongeza ajira na ku-cut down imports ya consumables.

Ni aibu tuna import 90% ya ngano.
Ni aibu tuna import surgical cotton, bandage, gauze, mashuka ya hospitali na tunalima pamba na tunashindwa kuzalisha products za pamba
Ni aibu tuna import 80% ya mafuta ya kula...the list goes on

Mguso huu utaipa serikali tax base kubwa based on purchasing power ya watu na makampuni ya ndani na hawa walio sekta isiyo rasmi na kilimo hasa cha kibiashara wataipa serikali chanzo kingine cha uhakika kukusanya kuhudumia Watanzania ikiwamo mishahara na maslahi mengine ya watumishi wa umma.

Hongera Mhe. Rais SSH

#Kazi iendelee
 
Mm ni mtumishi mzee, kwa taarifa yako hata walipopunguza kodi kuwa 8% effect unaiona kwenye mshahara wako. Kama mtumishi hukuona kuna nyongeza ya elfu kadhaa ya pesa imeongezeka kwako??
Soma vizuri hii statement ya ikulu
Screenshot_20220514-154241_1.jpg
 
Mshahara kadiri unavyopanda na KODI huwa kubwa lazima mtambue hilo.
Hivyo hiyo nyongeza ni flat rate kwa wote ila sasa utaona umeopata % chache kutokana na nyongeza ya makato ya kodi ambayo hutokea kutokana na viwango vya mshahara.

Sio kwamba 23.3% inaenda kuongeza kwenye take home yako NOOOOO. Inaenda kusogeza Basic Salary yako, kisha Kodi inafuata na hapa lazima muelewe kodi inatofautiana kati ya kiwango cha mshahara mmoja na wingine.
 
Afadhali wewe umeliona hilo. Unless otherwise mwandishi naye kiswahili kwake ni taabu, Lakini tafsiri ya aya ya kwanza ni hii.

1. Rais amekubali kuongeza mshahara kwa kiasi ambacho bado hakijawekwa wazi na ameongeza pia kima Cha chini kwa 23.3/%
2. Rasi amekubali kuongeza mshahara kwa 23.3% na kima Cha chini kwa 23.3%.
Namba 1 ndio jibu sahihi
 
Back
Top Bottom