Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Huyu Jane Lowassa ni mjinga na hajielewi, achana naye...

Hajui kuwa mtu hupata mahitaji yake muhimu ya kila siku i.e chakula, mavazi, malazi (mahali pa kuishi/kulala) nk nk kwa KUFANYA KAZI. Kazi yaweza kuwa ya kujiajiri au kuajiriwa na mtu, taasisi, shirika au serikali ...


Duniani kote na nchi yoyote kuna mgawanyo wa kazi (DIVISION OF LABOUR). Haiwezekani kila mtu ajiajiri na kuwa mfanyabiashara, machinga nk nk..

By the way, hata uwe mfanyabiashara uliyejiajiri mwisho wa siku utahitaji wafanyakazi kukusaidia kazi zako ambao ni lazima uwalipe mshahara...!

Jane Lowassa, suppose kila mtu angekuwa kwenye duka/biashara yake "aliyojiajiri (kama usemavyo), nani sasa angekuwa mhasibu wake? Dereva wake? Mbeba mzigo wake? nk nk

Duniani, binadamu wote tunaishi kwa kutegemeana...

Mfanyabishara aliyejiari kama wewe Jane Lowassa unamhitaji nesi, daktari, dereva wa gari yako, mwalimu afundishe watoto wako shule, msukuma mkokoteni abebe bidhaa zako nk nk..

Si hivyo tu, bali mfanyakazi huyu mwalimu, askari polisi au jeshi, daktari, Mtendaji wa kijiji, dereva, mkatisha tiketi, mwendesha mitambo kiwandani nk nk wanapopata mishahara yao mwisho wa siku wanampelekea mfanyabiashara au mtoa huduma aliyejiajiri in exchange with goods/services...

Jane Lowassa, asikudanganye mtu. Waliojiajiri/wafanyabishara wenye akili huomba na kupigana kufa na kupona kuhakikisha mfanyakazi ana mshahara kila mwezi au kila siku tena ulioboreshwa ili wawe na uwezo kununua bidhaa au huduma zao...

Ni mfanyabishara aliyejiari mjinga pekee anayeweza kuwaponda na kuwaombea wafanyakazi na wakulima mabaya maana hiyo inakuwa ni chanzo cha kudoda kwa bidhaa au huduma zao...!!

Jane Lowassa mpaka hapo umeelewa? Au bado uko gizani?
Maelezo Sahihi kabisa kuhusu division of labour.
 
Hapo umezungumzia chumi mbili tofauti.

Ile ya serikali kuwa na pesa na ile ya wananchi kuwa na pesa.

Ni jambo la kuamua.

Tofauti ya Samia na Magufuli ndio hii.

Samia ameamua kuwapa pesa wananchi na Magufuli yeye aliamua Serikali ndio iwe na pesa.

Sada hapo kila chumi ina faida na hasara.

Lakini mwisho wa siku mwananchi anapaswa kunufaika na serikali pia kufanya mambo ya maendeleo hilo lazima liwe balanced.
Hapa sasa umeongea mkuu, lazima iwe balanced.

Wananchi wakiitwa kuchanga michango ya mitaro barabarani na serikali ya mtaa wasishindwe kwa sababu ya umasikini na serikali isishindwe kufanya mambo yake muhimu ikategemea matajiri. NAKUBALIANA NA WEWE KABISAAAA.
 
Huyo hajaelewa! Hapo hawajaongeza mshahara kwa asilimia 23.3%! Serikali imekubali ongezeko la mshahara kwa 23.3% kwa kila cha chini! Maana yake kwamba kama kila cha chini kilikuwa lakini mbili(200,00) inamaa itaongeza 23.3% kwa kimya hicho cha chini na kuwa kama 238,000/,=kwa maana hiyo 38,000/= ndo ongezeko kwa nagzi hiyo ya chini si kwa ngazi nyingine! Sio kuwa mshahara umepanda kwa asilimia 23.3% kwa wafanya kazi wote hapana!
Kwanza hapo 23.3% sio 38000/= ni 46,600/= na pia haiwezekani kuongeza asilimia kwa kima cha chini cha mshahara bila kugusa mshahara wa kima cha juu kwa yeyote anayestahili, kwa mfano aliyetumikia cheo chake kwa miaka mingi.
 
Hakuna mtu anakufuru boss! Ila tunachojiuliza kama gharama zimependa ongezeko litaleta impact kidogo sana! Mfano imeongezeka 60,000 kwenye mshahara wako hapo impact yake ni kubwa kiasi gani?
Iyo 60k ilioongezeka...toa na Makato ndo utapata take home kilichoongezeka....ambacho ni kidogo ukilinganisha na gharama za maisha kwa sasa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo hakuna ufafanuzi hapo! Ongezeko la asiliamia 23.3%la kila cha chini cha msharana! Sio ongezeko la mshahara kwa asilimia 23.3%! Hapo tuelewane kwanza ndo tuweze kuongea zaidi hapo ni jambo zuri!
OFF COURSE WOTE WAAJIRIWA WOTE WATAPATA NYONGEZA HII ILA "DIMINISHING RATE UP WARDS" ( SAMAHANI SIJUI VEMA KISWAHILI CHAKE ....ILA NI HIVI MWENYE MSHAHARA GHAFI WA 270,000/= AKIONGEZEWA 23.3%, ANAYEFUATA WA 320,000 ATAPATA NYONGEZA YA CHINI KATI YAKE NA ALIYEMFUATIA KWA TOFAUTI YA 5% AU ZAIDI KULINGANA NA MAAMUZI ( NA FEDHA ILIYOTOLEWA )
....HIVYO ATAPATA NYONGEZA YA 23.3% PUNGUZA 5% AU ZAIDI = 18.3 %AU CHINI YA 18.3 % ...
ITAENDA HIVI KWA KWENDA KIMA CHA JUU HADI TUIKUTE 0.001%. LIMIT
 
Kabla ya kusema lolote naomba mtaalam yeyote aeleze maana ya23% kima cha chini. Hii 23% itaenda kwa kima cha kati au juu au hao hawaongezewi maana wananchi mtaani wanajua kila mtu anaongezewa 23%. Yaani kama mtu analipwa milioni 10 anaongezwea 23% yake
 
OFF COURSE WOTE WAAJIRIWA WOTE WATAPATA NYONGEZA HII ILA "DIMINISHING RATE UP WARDS" ( SAMAHANI SIJUI VEMA KISWAHILI CHAKE ....ILA NI HIVI MWENYE MSHAHARA GHAFI WA 270,000/= AKIONGEZEWA 23.3%, ANAYEFUATA WA 320,000 ATAPATA NYONGEZA YA CHINI KATI YAKE NA ALIYEMFUATIA KWA TOFAUTI YA 5% AU ZAIDI KULINGANA NA MAAMUZI ( NA FEDHA ILIYOTOLEWA )
....HIVYO ATAPATA NYONGEZA YA 23.3% PUNGUZA 5% AU ZAIDI = 18.3 %AU CHINI YA 18.3 % ...
ITAENDA HIVI KWA KWENDA KIMA CHA JUU HADI TUIKUTE 0.001%. LIMIT
Ok!
 
Hapo nimeongea na mtumishi mmoja wa umma anasema hiyo nyongeza ya 23% ipo hivi.
Kama Kima cha chini cha mshahara ni laki tatu itakuwa hivi
300,000 × 0.23 = 69,000.
Kwa hiyo watumishi wote wa serikali wataongezewa 69,000 kwenye mishahara yao.
Kwa aliyekuwa analipwa
500,000+ 69,000 =569,000
600,000+69,000=669,000
700,000+69,000=769,000
1,000,000+69,000=1,069,000
Hivyo hivyo kwa mishahara ya ngazi zote.
 
Back
Top Bottom