Rais Samia amekubali ombi la kukutana na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Rais Samia amekubali ombi la kukutana na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Siyo maslahi ya watanzania tena katika kujihakikishia wanajikomboa kikweli kweli kwenye ukoloni wa kiuchumi na kiteknolojia bali "demokrasia". Aisee, nadhani baadhi yetu hatujajua tunataka Tanzania iwe ya namna gani. Hili ni tatizo, linatakiwa kutatuliwa.
Maslahi ya watanzania ni pamoja na Demokrasia,na mimi nimeongelea mojawapo kati ya mengi ambayo tunategemea watajadili

Kusema demokrasia haina maana ndio kitu pekee anachoenda kupigania lakini kama chama cha Upinzani waliathirika zaidi wao kidemokrasia kwa kuzuiwa kufanya shuguli zao halali za kisiasa na hata kuporwa ushindi kwa wizi
 
Good start......Urais ni pamoja na kuwasikiliza hata walio na mawazo ama fikra tofauti na zako.

Mwendazake alikuwa ni muoga sana wa hoja za ana kwa ana - alikuwa na uwezo mdogo sana wa kuhimili kifua chake.
Yule alikuwa kichaa
 
Kwanini iwe CDM pekee? Mh. Rais alisema vyama vyote vya upinzani, kwani CDM ndio special sana kwa lipi? Vyama vyote vya upinzani kama Mh Rais alivyosema vitapata fursa ya kuongea na Mh Rais, sio Mbowe pekee au CDM pekee, hiyo hapana
 
Wewe nyumbu Mwenyekiti Mbowe alimuandikia Rais barua ya kuomba kukutana naye kabla hata Mh. Rais hajatoa ahadi ya kukutana na wapinzani,sasa barua ya Mbowe kujibiwa wewe unapata maumivu gani? Wacheni roho za kihutu za yule dhalim, mwacheni Rais afanye kazi. Sasa wewe unasema hiyo hapana ina maana unampangia Rais jinsi ya kufanya kazi zake? Kama hutaki nenda kashitaki kwa mwendazake
 
Haa wapi... tetesi ni kwamba wameambiwa kupeleka hoja zao kupitia kwa Shibuda na msajili wa Vyama ,kwanza wazikague kama zinatosha... hahahahaaaa kaazi iendelee.
Hizo tetesi hata mimi nimesikia. Kaongea Kibajaji Lusinde, na mwenzie Msukuma. Wala sio za kuaminika
 
Ikulu yatakiwa kuwa makini na hawa jamaa zetu. Inspection ya maana ifanyike kwenye makoti yao, yawezekana wakawa wamebeba chupa za konyaji na matap tap mengine

Sent from my TECNO CA6 using JamiiForums mobile app
 
Hizo tetesi hata mimi nimesikia. Kaongea Kibajaji Lusinde, na mwenzie Msukuma. Wala sio za kuaminika
Sasa wewe unabisha kitu gani wakati rais mwenyewe kaiandikia cdm kuwa yupo tayari kukutana na mwenyekiti wa chama?
 
Kwanza shibuda anaenda Kama Nani?huyu jamaa ni rangimbili ondoeni kwenye nafasi ya uenyekiti wa vyama hatufai.
 
Asante hayati rais Magufuli kwa kutuachia wosia wa kuacha hofu na kumtegemea Mungu kwa kila jambo.

Kimbunga Jobo na Corona wamekiona cha mtema kuni Tanzania.
 
Tatizo mlipandikizwa chuki mkachukika kweli na kujiona kila mnalotenda zuri hata muone wenzenu wanaumia vipi,halafu anasema atakuwa kiongozi wa malaika,kwa lipi
 
Hizo tetesi hata mimi nimesikia. Kaongea Kibajaji Lusinde, na mwenzie Msukuma. Wala sio za kuaminika
Timu ya darasa la saba inapeana tough!
 
Back
Top Bottom