Rais Samia ameshazidiwa na wapigaji suala la bei ya petroli?

TPDC wakianza kuuza mafuta mtawafunga mpaka mahakama itakataa kuwafunga tena. Mafuta ni biashara kichaa na ina risks nyingi. TPDC wamejipanga kubeba hizo risks?
Serikali ina hisa PUMA. Kwanini wasipambane PUMA ibebe interest za umma na kuwa kampuni yenye unafuu? Tusisahau pia kuna kodi kadhaa kwenye kila lita ya mafuta.
 
Bajeti ya Mwigulu hamkuisoma kwenye kipengele cha kodi ya mafuta ndugu zangu?

Au mliishia kusherehekea bia za buku ???
 
Bajeti ya Mwigulu hamkuisoma kwenye kipengele cha kodi ya mafuta ndugu zangu?

Au mliishia kusherehekea bia za buku ???
Uzi wa bajeti ulikuwa na replays 90

Wa Sabaya replays elfu 1 na zaidi

Wa kusaini petition ya kumtoa mondi BET ulikuwa na replays 800 na zaidi

Sasa utapambanua ni wapi watz akili zao zipo
 

TPDC lazima wafeli
Kwanza watapigwa vita na hao Oil cartel
Pili kampuni za umma zina bureaucracy nyingi
Na kushindwa kufanya maamuzi ya haraka..
Unless ianzishwe kampuni ingine iwe listed DSE....
 
Nyang'au atakuwa ni mke wako.
 
Nyie watu mnapenda sana Magu kumpa sifa zisizo zake!!! Magu hakuwa na uwezo wa ku-control bei ya mafuta, bali ilikuwa ukiona ipo chini, basi bei hata soko la dunia ipo chini!!

Magu angekuwa na uwezo wa ku-control bei za soko la dunia basi angefanya hivyo hata kwa mazao ya wakulima!!
 
Acha ku-mind vitu vidogo, hilo na jina la utani tu, huna haja ya kutoa povu!!! Hivi nyie mnavyoita Watanzania Bongo Lala, watu wameshawahi kuwahusisha na watu wa majumbani kwenu? Mbona una mambo ya kiboya!!
Nyang'au ni jina la tusi. Anyway, bei ya mafuta ya Kenya uliyoweka ni sahihi.
 
One of the best reading of the pertaining situation, I would say.

"Tunafungua nchi",; na bado!

Unafungua nchi na hukuandaa chochote kukabiliana na ufunguzi huo, lazima upigwe tu.
Ngoja tusubiri kuona nani "atamzingua" mwingine, 'cartels' au Samia?
 
Nyang'au ni jina la tusi. Anyway, bei ya mafuta ya Kenya uliyoweka ni sahihi.
Tunavyotumia nyang'au hatumaanishi tusi, bali enzi za Nyerere alikuwa anawachukulia Wakenya ni mabepari, kwahiyo neno nyang'au linawakilisha mapepari kwa sababu ujamaa ulikuwa unaamini mabepari hayajali utu wa mtu bali mali!

Aidha, ulikuwa unachukulia mabepari ni waporaji tu wa mali, na hivyo kuwa kama manyang'au!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…