Rais Samia ampendekeza Profesa Janabi kuwa Mkurugenzi wa WHO-Afrika

Rais Samia ampendekeza Profesa Janabi kuwa Mkurugenzi wa WHO-Afrika

Wanaomjua Hasa Kusoma Naye Wanasema Bongo Upande Wa Shule Ya Udaktari Alishindwa Ikabidi Aende Ng'ambo Kusoma
Ila Upande Wa Chakula Atatusumbua Sana Atagoma Tusile Chochote Tushinde Njaa
Mjanja sana we jamaa....
Eti upande wa shule ya udaktari alishindwa...hii maana yake nini?
Kwa uelewa wangu mdogo maana yake alikuwa Discontinued au nakosea mkuu?....nipo tayari kusahihishwa
 
Profesa Mohamed Yakub Janabi ni Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Oktoba 2022 mpaka sasa. Kabla ya Hapo alikuwa Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Jakaya Kikwete.

Mwaka 2005 alichaguliwa kuwa daktari binafsi wa Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Disemba 8 2024 ameteuliwa kuwa mshauri wa Raisi kwenye maswala ya afya, akiwa anaendelea na majukumu yake kama Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya taifa Muhimbili.

Elimu​

Dkt. Janabi amepata kusoma katika vyuo mbali mbali ndani na nje ya Tanzania. Vyuo hivyo ni pamoja na:-
  1. Kharkov Medical Institute (Russia)
  2. Liverpool School of Tropical Medicine (England)
  3. University of Queensland Medical School (Australia)
  4. Graduate School of Medicine Osaka University Hospital (Japan)
  5. Bergen University (Norway)
NYONGEZA

MKURGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi, juzi aligeuka kivutio kijijini kwake Mtakanini, Kata ya Msindo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, ambako na timu yake ya wataalamu walikwenda kutoa huduma za afya.

Wananchi hao walifurahi kumwona mtoto wao ambaye ni maarufu kwa kutoa ushauri wa kutunza afya kwa kula vyakula vinavyofaa na umuhimu wa kufanya mazoezi, huku wakishukuru kwa uamuzi huo na kuomba muda zaidi kwa wataalamu kutoa huduma.

Daktari huyo bingwa ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ni mzaliwa wa kijiji hicho ambaye elimu yake ya msingi alianzia kijijini hapo.

Prof. Janabi alikwenda kuungana na madaktari bingwa watatu waliokuwa wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo, kisukari, tezi dume na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa gazeti hili, wananchi hao walisema wamefurahishwa na mtoto wa nyumbani kuwakumbuka na kutumia utaalamu wake na wenzake kwenda kuwasaidia.

“Tulimsubiri yeye na wataalamu wengine kwa hamu kubwa. Wamekaa nasi kwa wiki moja tunatamani wangeendelea kukaa nasi au kwenda kwenye vituo vingine. Tunatamani mpango huu uwe endelevu tupate alimu ya afya kama anavyotoa kwa wengine huko aliko,” alisema Cartas Nyoni.

“Profesa Janabi ni mwanetu, amekuja kwa muda mfupi tunatamani angekaa muda mrefu ili watu waelewe vizuri, tunawaomba wawe wanatutembelea wakiwa na vifaa vya kisasa kama walivyokuja navyo sasa. Wananchi wanyonge wamepata huduma vizuri na bure wangekwenda kwenye vituo vya afya, hospitali za rufani wangetozwa fedha nyingi, tunaomba huduma kama hizi kwa wananchi tunaoishi vijijini,” alisema.
Je ni Chuo Kikuu gani kilichompa u-Profesa? Na kwa machapisho gani?
 
View attachment 3173721
Ni kweli Rais amempendekeza Prof Janabi kwa ajili ya kugombea nafasi iliyoachwa wazi na Dr Ndugulile hivi karibuni. Nilikuwa naijua CV ya marehemu vizuri sana, lakini nina wasiwasi na huyu Profesa Janabi ambaye amepata umaarufu kwenue mitandao ya Jamii dhidi ya kulakula hovyo.

Awali alikuwa Daktari binafsi wa Rais wa awamu ya 4 Jakaya Kikwete kabla hajapata kuwa mkuu wa JKCI na kisha MNH.

Je ataweza kushinda kiti hicho kama Ndugulile?

Basi tupeni wasifu (CV) wake hapa

Soma Hii Link
 
Ni Mtanzania mwenzetu tunatakiwa tumuunge mkono !
Yule alikuwa ni Dr. Na huyu wa sasa ni Prof wote ni wasomi wazuri tu !
Au nasema uongo ndugu zanguni. ???!
Tuubaguzi baguzi twingine hapa TZ tulishakataaga tangu enzi za Mwalimu 😳🙌👍🙏
 
View attachment 3173721
Ni kweli Rais amempendekeza Prof Janabi kwa ajili ya kugombea nafasi iliyoachwa wazi na Dr Ndugulile hivi karibuni. Nilikuwa naijua CV ya marehemu vizuri sana, lakini nina wasiwasi na huyu Profesa Janabi ambaye amepata umaarufu kwenue mitandao ya Jamii dhidi ya kulakula hovyo.

Awali alikuwa Daktari binafsi wa Rais wa awamu ya 4 Jakaya Kikwete kabla hajapata kuwa mkuu wa JKCI na kisha MNH.

Je ataweza kushinda kiti hicho kama Ndugulile?

Basi tupeni wasifu (CV) wake hapa
Ulitakiwa ukitoe kwanza hicho cheo chake cha Profesa, halafu ndiyo uombe CV yake. Kitendo tu cha mtu huyu kuwa ni Profesa; tayari kunampa extra merit kwa kazi hiyo
Still, mimi nilipendelea zaidi aendelee kutumika Muhimbili; anyway God knows
 
Back
Top Bottom