Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Mmebadilishana wewe umechukua nafasi ya uvccm
Hapana. Mimi NASIFIA mazuri yanapofanyika na NAKOSOA mabaya yakifanyika.

Mama akipatia (kama hapa kwa sabaya) Namsifia,na akikosea namkosoa vizuri kabisa.

Mimi sio kama maroboti ya Uvccm ambayo yamekuwa programmed kusifia tu kila kitu bila kutumia akili.
 
Hawezi kuwaondoa kwa matakwa ya mtu tu, unatakiwa kuuanika uchafu wao ili kujustfy unachokisema vinginevyo itatafsiriwa kama chuki inafsi kati yako na hao unaowataja
 
Hahahaha... Unachonifurahisha tu ni jinsi ambavyo sasa hivi umechukua nafasi ya Bavicha kuwa mpinzani wa Serikali ya CCM.
sijawahi na sitawahi.

chadema sijawahi kuwachukulia kama wapinzani,bali wahuni fulani wenye uwezo wa kuongea.
 
😹😹 Siku ya kufa nyani miti yote huteleza! Acha akatumikie upumbavu wake, alishindwa kusoma alama za nyakati mapema
 
Well
Wanasiasa wanajuana, wala tusishangilie sana tuache akiba ya maneno, hakuna cha zaidi kitatokea juu ya mtu huyu, walikuwepo wakina bashite!
 
Ameen ameen
 
Wewe Sabaya Muongo sana unaandika youth summit 2010 commissioned by Pinda wakati ulipopewa fedha uliishia kuwasomba wanachuo wa SJUT kwenda African dreams ukaishia kuwapa soda fedha zingine zote ukaweka mfukoni. Eti Youth Summit! Wadanganye wasiofahamu ukaghai wako!

Elimu yako ni ya kuungaunga na unafahamu vitu ulivyokuwa unavifanya pale SJUT. Sawa bhana, nature ya kazi yako ila wasiokufahamu watatema maneno sana. Naomba niishie hapa tutakapoonana tutabadilishana mawaili matatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…