Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Hakuna mwenye military CV Tanzania. Mara ya mwisho tumekuwa na military project was 1979, kizazi cha viongozi wa kijeshi wa leo walikuwa chekechekea.

Venance Mabeyo kwenye exit interview kaulizwa, nini vilikuwa vizingiti, mabalaa na changamoto kubwa kuliko zote ulizozipitia katika military carrer yako ???

Mabeyo akasema mafuriko na kifo cha Magufuli!

Disastrously embarrasing response, but it was the truth.

Sembuse huyu mteule wa leo ambaye hakuna aliyewahi kumsikia.
 
Karushwa viwili
Nimeambiwa kuwa kijeshi ni swala la kawaida,, Amiri jeshi mkuu anaweza kukupandisha vyeo kadri atakavyoona yeye ni sawa,,,,na CDF pia ana uwezo huo...

so Lipo sawa kwa taratibu za Jeshi.
 
Watu hawana masihara na ugali wao panda kwenye gari sit, nyingi ila utaishia kusimama kutoka mwanzo wa safari Hadi mwisho wa safari.
 
Ule uzi wa utabiri wa nani atakuwa CDF mpya umemuharibia sana Luteni Jenerali Mkingule hana hu na ule uzi
 
Hiyo error katika kutoa pasi na unapogundua umekosea unaurudisha mpira nyuma kidogo au unaendelea mbele.

Karata hazikuchangwa vizuri ndio maana haya hutokea.
 
Hiyo error katika kutoa pasi na unapogundua umekosea unaurudisha mpira nyuma kidogo au unaendelea mbele.

Karata hazikuchangwa vizuri ndio maana haya hutokea.
Dah,
Nimekusoma na kucheka kidogo ulivyopiga chenga hapa!

Hiki ndicho kipaji tulichojaliwa waTanzania wengi wa sasa, na ndicho kinachotumiwa na wanasiasa wetu kadri wawezavyo kwa maslahi yao.

"Unatoa pasi, unagundua umekosea..."; halafu sijui inakuwaje "...uurudishe mpira nyuma kidogo...", na huku ulishatoa pasi! Bila shaka utakuwa na miguu ya sumaku.
 
Hata chanzo ulichoweka kinakataa kuita hilo tukio kama coup. Tofautisha coup na mutiny
 
Napinga vikali jeshi kuwa na viwanda au kufanya biashara. Jeshi la Misri hapa Afrika ndio huwa linafanya hivyo, linasumbua sana serikali za kiraia. Jeshi la Pakistan nalo liko hivyo wasumbufu mno.

Mfumo wetu ulitakiwa uwe exactly kama tunakoiga Uingereza. Kule humpati mtu katoka Sandhurst alafu eti anakuwa balozi sijui mkuu wa bodi gani. Unafanya ilivyosomea.

Wizara ya ulinzi ndio iwe na research facilities na departments kusaidiana na sekta binafsi. Kama Marekani walivyo na DARPA au India walivyo na DRDO inayoshirikiana na kina Mahindra na TATA
 
Hii staili ya kupandisha vyeo na kuteua alianza JPM ina maana ile safu ya juu haiamiki kwa Cha cheo Cha CDF.......??????

..Ni utaratibu wa siku nyingi ktk kuteua Cdf na CoS.

..Kama anayeteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi sio Mkuu wa utawala jeshini [ namba mbili kwa cheo] basi ni lazima mteuliwa ataruka rank moja.

..Kwa mfano, 1974, Kanali Abdallah Twalipo alikuwa RC Ziwa Magharibi / Kagera akaruka ngazi ya Brigedia akapanda kuwa Meja Jenerali na kuteuliwa kuwa Cdf.

..Pia miaka ya 80 Meja Jenerali Ernest Mwita Kiaro aliruka rank ya Lt.Jenerali na kupanda kuwa Jenerali na kuteuliwa kuwa Cdf.

..Miaka ya 90 Meja Jenerali Robert Mboma aliruka rank ya Lt.Jenerali akawa Jenerali na kuteuliwa Mkuu wa Majeshi.

Nas Jr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…