Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

12 August 2019

OPERESHINI KIKAKA 2019


Mkuu wa Brigedi ya kanda ya magharibi (202 Kikundi cha Vikosi) Brigedia Jenerali, Julius Mkunda alisema hayo mkoani Kigoma wakati akiahirisha zoezi la kijeshi la kujiweka tayari kwa wapiganaji wa jeshi kupambana adui pindi anapotokea na kusema kuwa amani na usalama wa Watanzania ni lazime upewe kiupaumbele.



katika zoezi hilo lililofanyika kwenye mapori ya wilaya za Kibondo, Kasulu na Kakonko na kutambulika kama kama Opereshini KIKAKA

Opereshini KIKAKA Brigedia Jenerali Mkunda alisema kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mapori hayo, kutumika kwa shughuli za maficho ya ujambazaji, uwindaji haramu na kilimo mambo ambayo yanafanywa na wageni kutoka nchi jirani.

"Tanzania siyo shamba la bibi kwa kila anayetaka anakuja kufanya anachojisikia, hatutakubali tutawaadhibu wale wote wenye nia mbaya ya kutumia mapori yetu kwa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi yetu, lakini vinatishia amani na usalama wa raia na mali zao na kuwafanya waishi kwa woga,"Alisema Brigedia Jenerali Mkunda.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita kutoka Brigedi ya kanda ya Magharibi, Kanali Wilbert Ibuge alisema kuwa mapori yote ambayo watu wanayaona nchini yana wenyewe na wenyewe ni jeshi la wananchi wa Tanzania ambao wana wajibu wa kuyatunza na kuyalinda na hivyo hakuna mtu yeyote ambaye ataingia kwenye mapori hayo akaachwa ayatumie anavyotaka.

Mkuu huyo wa mafunzo alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utimamu na utayari wa jeshi kujindaa kupambana pindi adui anapotokea na kwa sababu kwenye vita hakuna mahali pa kufanya majaribio hivyo kazi ya kuwasaka na kuwakamata wale wote ambao wataingia kwenye mapori hayo na kufanya vitendo vya uhalifu itatumika kama sehemu ya mazoezi kwa vitendo kwa wapiganaji.
Source : Na Editha Karlo,wa michuzi Tv, Kigoma


26 June 2022

“SIVAI KOMBATI KWA KUIGIZA MIMI NI MWANAJESHI,TUCHAPE KAZI”- RC Brig. Gen IBUGE


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewaeleza madiwani wa Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma kwa nyakati tofauti kuwa jukumu alilopewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kusimamia utendaji kazi ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wa Ruvuma kwa kutekeleza Ilani ya CCM ya 2020 hadi 2025 na kwamba hana mpango wa kuingia kwenye Siasa.
Source : Nyasa DC online
 
14 June 2022

WAPIGANAJI WA JWTZ WATAKIWA KUISHI KWA VIAPO VYA UTII


Mkuu wa Operesheni na Mafunzo ya Kijeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali John Jacob Mkunda amewataka askari wapya wa Jeshi hilo kuishi kwa viapo vya Utii, kulinda nchi na mipaka yake.

Wapiganaji wanafunzi Zaidi ya elfu mbili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakifurahia kumaliza mafunzo ya matumizi ya silaha za kivita katika pori la Pongwe Msungure Msata mkoani Pwani Chini ya shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko, Meja Jenerali Mkunda amesema kuishi kwa utii ni pamoja na kuilinda na kuiteta na katiba ya Tanzania.
 
..sijaelewa mantiki ya kuteua CoS halafu asifikishe hata mwaka anateuliwa mwingine.

..kwanini hakumuacha CoS Yakubu Mohammed astaafu wakati mmoja na Cdf Mabeyo?

..Hiyo ingemuwezesha kuteua Cdf na CoS kwa wakati mmoja kama ilivyofanyika wakati wa Kiaro na Kiwelu, au Mboma na Sayore.

Cc Kichuguu
 
Tunaweza kusema kuwa pamoja na kuwa na madaraka yote, hadi uwezo wa kuwa juu ya Katiba,; lakini inapokuja kwenye eneo la hawa jamaa, mtu huyo mmoja ni lazima atii.

Hawezi kujiamria atakavyo yeye kama huku kwingne kote.
 
Inawezekana uwezo wa mteuzi hauna nguvu kama tunavyofikiri huku mitaani.
Angalia #241 hapo chini.

Hawa wenzetu inawezekana bado wana uhuru wa kufanya mambo yao wanavyoona wao inawafaa, siyo kama huku kwingine ambako mwenye madaraka yote ni huyo huyo mmoja, asiyeweza kuhojiwa na yeyote, hata Bunge.
 

A very lucky man. Naona hata cheo cha Major Gen hajakitumikia sana!
 
[emoji837] BREAKING NEWS

Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha Cheo Meja Jenerali Jacob Mkunda Kuwa Jenerali na amemteua Kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi-CDF

[emoji406]-IKULU
Hii imekaaje.
Kumpandisha mtu cheo na kumpa ukuu wa Kitengo! Ina maana hakuwepo mwenye nafasi ya kupewa hiyo cheo.
Asante Mabeyo.
 
Niliposoma ulichoandika hapa nilikuwa bado sijaangalia jina.
Nashangaa kidogo, lakini nimeanza kuzoea tabia hizi za kiTanzania zinazobadilika kila mara. Hazitabiriki.

Sasa uliyoandika hapo, sijui kama utayakumbuka baada ya miaka miwili mitatu ijayo!

Ningekuwa na uwezo ningeyaweka kwenye paji la uso wako kama lebo, ili usithubutu kusahau ulichoandika hapa.

Na ili usinione mimi kama ninakuonea, hebu jikumbushe habari zako juu ya Lissu, miaka michache iliyopita.
 
Hii imekaaje.
Kumpandisha mtu cheo na kumpa ukuu wa Kitengo! Ina maana hakuwepo mwenye nafasi ya kupewa hiyo cheo.
Asante Mabeyo.
May be waliopo wana some flaws.

General anaendoka anawajus vizuri nje ndani.

Na kwenye hii selectio ame play part kubwa kumshauri rais

Congrats General J.J MKUNDA afande tunaokbs utupatie jeshi imara la wanachi sio la kikundi Fulani.

Wazi afandeeee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…