Rais Samia amteua Mavere Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)

Nampongeza Raisi kuanza kuteua wenye uwezo toka private sector watasaidia sana nchi na kubadilisha utendaji kwenye taasisi kutoka business as usual

Wengi serikalini sio wabunifu ni wafanyakazi kwa mazoea

Taasisi nyingi za umma na ubalozini vizuri zipate watu toka private sector
 
Suala ni kungalia uwezo wa mtu na ifanyike comprehensive Vetting ya kuangalia character na Capacity bila kujali katoka Private au Government.Kwa Taarifa yako, Ex-DG wa MSD Mr. Laurean Bwanakunu(DG kabla ya Mej. General Mhidze) alitokea Private Sector kwenye NGO kama Mr. Mavere lkn aliishia kutumbuliwa na kashfa kibao nyuma yake.

MSD is very Complex Institution, Msivimbishe Kichwa Mr. Mavere jipange uende MSD kwa umakini, otherwise utaishia kuharibu CV kama Laurean
 
Huyu ndugu Mavere Tukai ni "kichwa" haswaa.....

Ni "pharmaceutical management specialist"....

Jamaa yuko FOCUSED na DETERMINED sana.....

Alikuwa pale USAID....wamarekani wanamfahamu kwa uwezo mkubwa alionao....watammiss sana.....

Imefika muda atutumikie katika MSD.....

Kila la heri kwake kamarada Mavere Tukai ,amen🙏

#Siempre JMT🙏
#YetzerHatov🙏
Kichwa ndio maana yake nini??

Kwani kuna siku nchi hii ameteuliwa mtu ambae ni kiuno?
 
Nampongeza Raisi kuanza kuteua wenye uwezo toka private sector watasaidia sana nchi na kubadilisha utendaji kwenye taasisi kutoka business as usual

Wengi serikalini sio wabunifu ni wafanyakazi kwa mazoea

Taasisi nyingi za umma na ubalozini vizuri zipate watu toka private sector
Tatizo wengi ni wezi.
 
Kichwa ndio maana yake nini??
Tukai Mavere is a pharmaceutical management specialist and a procurement professional experienced in pharmaceutical management, supply chain management and projects management. His supply chain management knowledge were acquired from the Chartered Institute of Purchasing and Supplies (CIPS); he also has a Bachelor Degree in Pharmacy [BPHARM] and Masters Degree in Pharmaceutical Services and Medicines Control: Mavere has hands-on experience in procurement, project management, supervision, and training and pharmaceutical supply chain management. He has a total of 14 year work experience and over ten year experience in supply chain management.
 
Sasa mkuu huo ndio ukichwa?

Mimi navyojua kichwa ama ukichwa uko kwenye creativity, innovations nk kumbe ukichwa ni kua na masters degree na professional certification, aisee.

Haya tusubiri.
 
Aende akafanye kazi kwa manufaa ya watanzania sio manufaa yake binafsi.

Tatizo kubwa ya wanao teuliwa wanawaza zaidi kujineemesha wao badala ya kuwatumikia wnanchi. tubadilike.
 
Sasa mkuu huo ndio ukichwa?

Mimi navyojua kichwa ama ukichwa uko kwenye creativity, innovations nk kumbe ukichwa ni kua na masters degree na professional certification, aisee.

Haya tusubiri.
Ni mtaalamu anatokea USAID kule waajiri vichwa tu tena vikali vyenye uwezo mkubwa wa creativity innovation nk

Professional certification yake umeiona ?ni ya kimataifa siyo ya Tanzania .Tanzania wapo wachache sana professionals wenye international certification
 
Tukai Mavere is a pharmaceutical management specialist and a procurement professional experienced in pharmaceutical management, supply chain management and projects management. His supply chain management knowledge were acquired from the Chartered Institute of Purchasing and Supplies (CIPS); he also has a Bachelor Degree in Pharmacy [BPHARM] and Masters Degree in Pharmaceutical Services and Medicines Control: Mavere has hands-on experience in procurement, project management, supervision, and training and pharmaceutical supply chain management. He has a total of 14 year work experience and over ten year experience in supply chain management.
I think the big issue at MSD is not about procurement and supply ...the issue is how to mobilize sustainable financial and other resources.
Nimtakie kila la kheri lakini atumie hoja yangu kuongezea kitu pale MSD.
 
Watenguliwa wa Magu bwana, wana asili ya wizi wizi tu! Sijui alikuwa anawatuma! Na wala hawajawahi kuguswa!
 
Sawa.....

Yangekuwa ni maelekezo ya kuzodolewa kusikokwisha iwapo angeniteua mimi Jumbe Brown ,kijana muuza kahawa na Al Kasus hapa kwa Mtogole.......

#Siempre JMT[emoji120]
Kuwa na adabu kwa mtogole,mtogole unamjua wewe?pumbafyu
 
Mashirika mengi yanahitaji professionals
 
Ni mtaalamu anatokea USAID kule waajiri vichwa tu tena vikali vyenye uwezo mkubwa wa creativity innovation nk

Professional certification yake umeiona ?ni ya kimataifa siyo ya Tanzania .Tanzania wapo wachache sana professionals wenye international certification
Acha uchawa huko USAID kuna vilaza kibao wanachojua ni kuandika vi-report vya ku-solicit donor funding lkn impact kwenye Taasisi kama MSD unakuta haziko practical na zisizo na impact kwenye operations,mtihani rahisi wa kuanzia kwa Mavere ni MSD kutoa Automated O/S notification ndani ya 24 hrs kwa Hospitals na HFs,jambo ambalo akiwa Global Health alikuwa analipigia debe
 
Kwa mnayejua, ni hana uwezo au tunapinga tu sababu tuko upande unaotakiwa upinge?!
Anafanya USAID, kuwa mujibu wao hiyo inatosha. Kiasi naunga mkono kiasi nachelea. Lakini tukumbuke hizi kazi za mashirika ya kimisaada ya nchi za ng'ambo nyingi zipo katika mtindo wa "donor demand oriented with strictly and stringent regulations and protocol" ambazo hazitoi "room" ya kuwa "innovative" bali kuwa standard "operator".

Nawaza tu jamani sijakonkuluudi.
 
View attachment 2187838

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi jioni ya Aprili 14, 2022 kama ifuatavyo:

Amemteua Rosemary William Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bohari ya Dawa (MSD), Bi. Slaa ni Afisa Mwandamizi katika Kampuni ya Picenaterhouse Coopers PWC.

Amemteua Mavere Ali Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Tukai ni Kiongozi Mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance.

Amemteua Raymond William Mndolwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mndolwa ni Mtaalam wa Operesheni, Kampuni ya STC Construction, Dar es Salaam.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus ni kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
View attachment 2187787
Hongera sana Mavere!

Najua kazi utaweza, sina shaka na wewe.

Ila swali kengeufu. Je, serikali haina watu wenye sifa wa kuziba nafasi hizo? Watu ambao wana uzoefu na ufanisi na mapungufu ya mifumo ya serikali walioanza ajira tokea nafasi za chini hadi kufika juu? Siamini kama kwenye kundi la watumishi wa serikali, hawapo wenye sifa kuongoza Tanesco, MSD na mashirika mengine ambayo uteuzi umefanyika nje ya taasisi za serikali. Kuna reward gani kwa watu wanaofanya kazi serikalini, kama nafasi ndogo kama hizi wanapewa watu wa nje ya mfumo?

Kama viongozi waliopo sasa kwenye taasisi zetu wameshindwa kujaza nafasi kama za Tanesco na MSD ni bora wakaondolewa na kuwekwa wengine, tuwape watumishi wengine nafasi ya kung'ara.
 
Ni mtaalamu anatokea USAID kule waajiri vichwa tu tena vikali vyenye uwezo mkubwa wa creativity innovation nk

Professional certification yake umeiona ?ni ya kimataifa siyo ya Tanzania .Tanzania wapo wachache sana professionals wenye international certification
Najua mashirika mengi ya kiMarekani yakiwa Afrika hupenda sana kuajiri mtu aliyesoma mojawapo ya digrii zake nchini Marekani. Huwa rahisi sana (Sisemi kwa Mavere). Wanamuamini zaidi hata kama hayuko vizuri. Otherwise kuna watu wengi wa kawaida sana katika haya mashirika.
 
View attachment 2187838

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi jioni ya Aprili 14, 2022 kama ifuatavyo:

Amemteua Rosemary William Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bohari ya Dawa (MSD), Bi. Slaa ni Afisa Mwandamizi katika Kampuni ya Picenaterhouse Coopers PWC.

Amemteua Mavere Ali Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Tukai ni Kiongozi Mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance.

Amemteua Raymond William Mndolwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mndolwa ni Mtaalam wa Operesheni, Kampuni ya STC Construction, Dar es Salaam.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus ni kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
View attachment 2187787
Tatizo Tanzania siyo uteuzi, bali usimamizi. Iwapo rais anawateua bila kuwasimamia, hakutakuwa na mabadiliko yoyote. Hao MSD walipokuwa wanasimamiwa walifanya vizuri, usimamizi ulipoondoka, utendaji nao ukaondoka. Bila usimamizi kutakuwa na teuzi kila kukicha bila mabadiliko yoyote.
 
Huyu Mavere Tukai ni "pharmaceutical management specialist".....amebobea haswa na ana IQ nzuri na anapenda KUSIKILIZA sana......

Mkuu wangu Nyboma kwa heshima ya ulipopita na kufanya kazi kama mzalendo si vema kuwakandia watanzania wenzako....

#Against Bigotry 🙏
#Against Any Form Of Prejudice And Discrimination 🙏

SIEMPRE JMT🙏

Chawa kazini
 
Hongera sana Mavere!

Najua kazi utaweza, sina shaka na wewe.

Ila swali kengeufu. Je, serikali haina watu wenye sifa wa kuziba nafasi hizo? Watu ambao wana uzoefu na ufanisi na mapungufu ya mifumo ya serikali walioanza ajira tokea nafasi za chini hadi kufika juu? Siamini kama kwenye kundi la watumishi wa serikali, hawapo wenye sifa kuongoza Tanesco, MSD na mashirika mengine ambayo uteuzi umefanyika nje ya taasisi za serikali. Kuna reward gani kwa watu wanaofanya kazi serikalini, kama nafasi ndogo kama hizi wanapewa watu wa nje ya mfumo?

Kama viongozi waliopo sasa kwenye taasisi zetu wameshindwa kujaza nafasi kama za Tanesco na MSD ni bora wakaondolewa na kuwekwa wengine, tuwape watumishi wengine nafasi ya kung'ara.
Kila mtanzania anapaswa kuitimikia nchi yake bila kujali yupo serikalini Kama mtumishi wa muda mrefu au nje ya taasisi za serikali
 
Back
Top Bottom