hivi wewe si ulikuwaga mfuasi wa ibilisi meko wewe???SSH anaweza kuchukiwa kwa sababu ya jinsia yake lakini hana tofauti na JPM tena yeye anakwenda mbali zaidi kwa kuwa karibu na dunia nzima kwa ujumla.
Huku Dar wale wapangaji wa kwenye majengo ya Masaki na maeneo mengine wameshaanza kurudi maana yake upo mzunguko wa pesa kwa sasa.
Hao kina mama wa vijijini wenye nongwa za yule jamaa yao aliyekuwa akichanganya lugha majukwaani na wanamuelewa na kucheka wanajitafutia tu maumivu ya mioyo na kununa kusiko na sababu.
huyu ni mrundi asikupe shida, huwa anashinda ziwa tanganyika sana maeneo ya kibiriziMzee upo Tanzania hiihii au ndio kujitoa ufahamu kwasababu unatumia Phillipo Bukililo unaamini kabisa kwamba jina lako litaonekana somewhere!?
Maana nashindwa kukuelewa!!??...Jamaa ameongea point zilizopo kabisa na mtaani hali halisi ndio hiyo au mwenzetu sio mtz?!?.
Ni kweli kabisa Samia kuna mambo mazuri kafanya(anafanya) na anajitahidi kwa kiasi chake ila kwa sababu zilizotajwa na muanzisha thread ni kweli kabisa zinamfanya achukiwe.
Njoo mtaani huku uone watu wanavyomuongelea kiufupi hawamuelewi kabisa nenda hata facebook upate maoni ya raia kiukweli watu wamekataa kabisa kumuelewa na yeye anajua hilo pamoja na kwamba kajenga madarasa na blahblah kibao ila watu HAWAMUELEWI
Hakuna wakuleta machafuko nchi hii, maana watanzania Wana Imani na matumaini makubwa Sana na serikali ya CCM, ndio maana unaona hata Lisu aliposema muandamane hata wewe mwenyewe ulimpuuza na Kuendelea na shughuli zako za kukupatia kipato,maana unayo Imani na CCM na unatambua wazi kuwa Lisu Ni mbabaishaji tuChawa watu walishaamka muda mrefu, au unadhani matumizi ya vyombo vya dola yataendelea kuwa upande wenu kila siku? Machafuko tu ndio yatawaondoa madarakani nyie majizi ya kura.
"Watanzania wote", hilo tu linaonyesha huna kitu kichwani. Sijui kwa nini unapoteza muda hapa JF.Watanzania wote tumeona maendeleo makubwa aliyoleta Rais Samia Suluhu kwa kipindi cha siku 567 kwaiyo 2025 mama hana haja ya kufanya ata campaign maana matendo yake yanajieleza tupo nae mpaka 2030
EeeenHeeee!Matumaini ya kuzoa viti vya ubunge upo kama ilivyokuwa awamu ya nne.
IlngoJuzi tu hapa Geita alipokuja Kinana walimwambiaa kabisa Samia hapendwi, mwanzoni kabisa mwa mwaka huu alikuja Shaka akasema Samia mitano tena wananzengo tena akina mama wa CCM wakasema NDOHOOOOO nilishangaa sana.
Hata tume ije kutoka marekani bado CCM itashinda kwa kishindo tuRuhusuni uchaguzi huru msiwe mnawatoa mawakala wa upinzani vituoni mkama mnajiamini
Democracy kwenye Nchi iliyozowea kuendeshwa na Chama kimoja tena cha kikomusti inatakiwa struglle kwelikweli.EeeenHeeee!
Hiyo awamu ya nne yenyewe hao wapinzani walioingia bungeni ilikuwa ni kwa jasho na damu, au hukumbuki?
Ndugu yangu usihangaike na Watanzania sababu aijulikani wanataka niniJuzi kati, nilisafiri toka Kyela kwenda Zanzibar via Dar, ulikuwa usafiri maalum, abiria sio zaidi ya 30.
Baada ya Konyagi kadhaa, huku safari ikiendelea mjadala wa siasa ukaanza! Zaidi ulikuwa ukilinganisha awamu ya tano na ya sita.
Wengi wa abiria walisimama na hoja ya kuwa awamu ya tano yapo ilikuwa fupi ilikuwa ni bora zaidi kuliko awamu zote.
Binafsi nikahoji ni ubora gani ambao wana zungumzia. Wengi wao wakaanza kutaja miuondo mbinu kadha wa kadha na wengine wakasema juu ya kudhibitiwa kwa ufisadi na rushwa.... uwajibikaki wa watendaji serikali na mengi kama hayo....
Nikauliza katika miradi hiyo ya kimkakati ni upi uliokwama ama kufutwa kabisa? Sikupata jibu la moja kwa moja, zaidi ya kusema pengine sasa ingekuwa imekwisha kamilika. Nikahoji juu ya ufahamu wao katika eneo hili, sikupata jibu sahihi au la moja kwa moja zaidi ya walivyosema awali.
Nikauliza tena juu ya ufisadi na rushwa. Je kuna ufisadi gani unaoendelea sasa na vipi kiwango cha rushwa katika awamu hii? Hapakuwa na jibu la moja kwa moja, zaidi ya kelele kwamba watu sasa wanafisadi zaidi kuliko awamu iliyopita. Nikawakumbusha kuwa tukiwa njiani kwenda Kyela na tulipofika Iringa tuliamriwa kulala hapo kwani muda wa kusafiri ulikuwa umekwisha. Ni hao hao walioanza kuwashawishi Polisi waturuhusu kwani tuna safari muhimu na maalum. Wengine wakapiga hata simu makao makuu ya jeshi la Polisi ili tu tuweze kuendelea na safari yetu!
Je hiyo haikuwa kutaka rushwa? Kwanini hatukutaka kufuata taratibu na sheria ya usafiri wakati wa usiku...! Sikupata jibu la moja kwa moja zaidi ya kelele tu! Huyu hatoboi 2025! Kwa nini hapana jibu!
Rais wa Ethiopia siyo mkuu wa serikali kikatiba bali ni mkuu wa nchi asiye na madaraka ya kuteua au kuunda serikali.5. Jinsia yake.
Hili nalo ni kujitetea tu, Jinsia Wala ht Si tatizo.
Pale Ethiopia ni JINSIA hiyo hiyo, mbona Yeye hakukimbilia Seat ya dirishani???
Alionyesha msimamo wote tumemkubali...
Sasa Kinana huyo huyo eshajuwa njia nzuri zaidi za kuwabana wapinzani, nafuu hiyo ya kupata wabunge wengi itatoka wapi?Democracy kwenye Nchi iliyozowea kuendeshwa na Chama kimoja tena cha kikomusti inatakiwa struglle kwelikweli.
Hata wakati huo Kinana na Nape walipambana na sisi kweli kweli.
Ssh angekuwa anasikiliza critics hakika angepata Mo Ibrahim award tena sababu ni mwanamke ingekuwa rahisi na angeweka landmark kwa wanawake wengine wataokaobarikiwa kukamata dola kwa uchaguzi .
Katibu mkuu mstaafu Marten Lumbanga amenukuliwa akisema " Katiba mpya haikwepeki" wanaweza wakaikwepa lakini mabadiliko yanayoendelea duniani na haswa kwa sababu ya midororo ya uchumi, mabadiliko ya tabia nchi, na mabadiliko ya serikali zinazoshinda chaguzi nchi mbalimbali wahisani. Legacy kubwa mama ataiacha ni Katiba. Maana shule hizi hata zikijengwa hazitakuja kutosha, ajira ndio kabisa
Kutesa kwa zamu (In Twanga pepeta's voice)Kila awamu kuna wanaojuta na kuna wanaofurahi.
Naona mtoa mada anajifariji tuBadili kichwa cha habari kwanza ili uzi wako uwe na maana kwa msomaji. Mama anatekeleza miradi huko mikoani.
Nasikitika kukwambia kwamba hao wanaopata madarasa mapya hawasomi uzi kama wa kwako. Hawa wanaopata umeme huko vijijini ndani ya muda huu hawana muda wa siasa za maji taka kama hizi.
Kuna watu wanaguswa moja kwa moja maisha yao, hao hawana muda wa kusoma ulichoandika achilia mbali kuwa na muda wa kukitafsiri kwa kina.