Rais Samia anafanya kile ambacho wengi wenye akili tunataka afanye! Kwa hili anastahili pongezi

Rais Samia anafanya kile ambacho wengi wenye akili tunataka afanye! Kwa hili anastahili pongezi

Yani wee jamaa bado mawazo yako ni ya kizamani mno.Rasilimali kubwa ambayo tunatakiwa kuiendeleza ni akili ya watu wetu (human resource).Hii ikiwa kubwa rasilimali nyingine zote zitakuwa na maana vinginevyo zitabakia kuwa takataka tu. DR Congo wana rasilimali nyingi mno kuliko hata zilizopo Tz lakini kwa sababu ya kukosa akili wamebaki kuuana wenyewe kwa wenyewe na kubakia masikini.Hivyo mimi ningekuelewa kama ungezungumzia kuwekeza vya kutosha ktk elimu.
Endelea kuishi kwa mawazo mfu! Kuwekeza kwenye Elimu ni jambo lingine na kuwekeza kwenye utalii ili upate hela za uhakika za kukuwezesha kuwekeza kwenye elimu bora ni jambo lingine
 
Kuweka wazi ni jambo moja na kuchukua hatua ni jambo lingine.

Wananchi wanataka kuona hiyo ripoti ya CAG ikifanyiwa kazi. (Jambo ambalo nina hakika halitafanyika kwenye huu utawala) CCM ni mafia.
Sasa hivi wananchi wengi(hata upinzani) wanacheza ngoma ya hiki chama bila kujitambua.
Amechukua hatua ya kubadilisha Uongozi wa MSD kwa kumuweka Mtendaji mwingine! Tafuta lingine
 
ukisema tutumie gharama kubwa kuutngaza utalii na wakati huku ndani ya nchi miundo mbinu ya kufika kwenye hizo sehemu ili watalii wapelekwe haipo sawa. utakuwa tabularasa. miundo mbinu ya hotels barabara bado sio rafiki. taasisi zinazosimamia utalii zenyewe ni mkanganyiko haileweki nani ni nani ukienda huku unakutana na TAWA huku TANAPA kule wengine vurugu tupu.
Watalii wanaofika Ngorongoro na Serengeti wanafikaje?

Nitakubaliana na wewe ukisema miondombinu iboreshwe zaidi hasa kwenye maeneo ambayo we have not invested enough kama Ruaha National Park, Selous, Kitulo na Katavi National Park
 
Hayo madudu ni bajeti ya 2021/2022 ambayo inaendelea kutekelezwa. Meanwhile mama kaanza nayo na anaitekeleza.

Wachota hela hiyo ni timu msoga kwa taarifa yako. Na mama hawezi wadhibiti hao kwa kuwa ndo wanamlinda na kuongoza nchi.

Kwani January amewekwa pale na nani kukatakata umeme.

Kwani kodi utitiri za miamala kila nahali zimewekwa na nani. Na je fedha lukuki za miamala zinaketa madiliko gani ya maendeleo tangu zianze mwaka jana.

Ester Bulaya alisema hakuna barabara mpya zinazojengwa tangu mrithi wa marehem ashike kijiti. Ulimwelewa?

Kwa ujumla spidi ya maendeleo imerudi nyuma. Mama anabadilshia baibui kwenye ndege. Ana safari nyingi za nje kuliko za kutembelea wananchi.
Endelea kuishi kwenye hiyo dunia yako ya chuki inayokupa mawazo ya kusadikika
 
Kukaa Marekani unamaanisha nini? Rais yupo Marekani Kikazi na anafanya kazi za kuliletea maendeleo Taifa huko Marekani! Shida iko wapi?

Unataka akae Tanzania tu Tanzania wakati kuna kazi muhimu za kufanya Marekani? Utakuwa na mtindio wa ubongo
Tunaomba Raisi Wa Marekani Aje Tanzania Akae Wiki Mbili.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Yani wee jamaa bado mawazo yako ni ya kizamani mno.Rasilimali kubwa ambayo tunatakiwa kuiendeleza ni akili ya watu wetu (human resource).Hii ikiwa kubwa rasilimali nyingine zote zitakuwa na maana vinginevyo zitabakia kuwa takataka tu. DR Congo wana rasilimali nyingi mno kuliko hata zilizopo Tz lakini kwa sababu ya kukosa akili wamebaki kuuana wenyewe kwa wenyewe na kubakia masikini.Hivyo mimi ningekuelewa kama ungezungumzia kuwekeza vya kutosha ktk elimu.

Mkuu utalii sio akili ya zamani
Pia tunaweza kuza utalii na akili za watu simultaneously
 
Dogo wacha kulamba mavi ya watu....hii kazi afanyayo rais ni kazi wanaifanya mabalozi wetu na maofisa wao. Mama anapoteza muda tu na pesa za wananchi kuzunguka maduniani kuitangaza Tanzania.

Mzee mabalozi wakitangaza haiwi sawa na raisi
Pia mtoa mada kasema point sana kuwa tuwe na matangazo ya utalii katika channel kubwa dunian
Licha ya kuwa tutatumia pesa but am sure pesa yetu itarudi zaidi
 
Mzee mabalozi wakitangaza haiwi sawa na raisi
Pia mtoa mada kasema point sana kuwa tuwe na matangazo ya utalii katika channel kubwa dunian
Licha ya kuwa tutatumia pesa but am sure pesa yetu itarudi zaidi
Tatizo lao ushamba tu
 
Kwa miaka mingi sana Tanzania tumekuwa tunalalamika jambo moja kuu, nalo ni kwamba, pamoja na kuwa na maliasili na utajiri mwingi ila nchi yetu hasa wananchi wamekuwa masikini sana!

Mjadala huu umezungumzwa na kipindi kirefu sana na moja ya sababu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Tanzania kuendelea kuwa masikini pamoja na kuwa na utajiri na Maliasili nyingi ni kwa sababu tumekuwa hatutumii utajiri wetu vizuri ikiwemo kuutangaza kwa dunia ili utunufaishe kiuchumi! Siku zote biashara ni Matangazo!

Kwenye hili suala napenda leo nikiri kuwa Rais Samia ameanza kulipatia majibu suala hili!

Kwa Bara la Afrika, nchi zinazoongoza kwa kupokea watalii wengi ni Morocco, Algeria, Misri na South Africa. Nchi hizi zinapokea watalii zaidi ya Mil 5 hadi Mil 10 kwa mwaka. Na kusema kweli hizi nchi utalii unazinufaisha sana! Kiuhalisia hizi ndo nchi zenye Uchumi mkubwa Afrika na ndo zinaongoza kwa kuwa na chumi imara na maisha bora kwa sehemu kubwa ya wananchi wake!

Ila kwa uhalisia, Kama umetembelea nchi hizi zinazoongoza kwa utalii Africa utagundua kuwa hazina kitu kikubwa kuizidi Tanzania na ukweli ni kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kuzizidi nchi zote hizi.

Kwa South Africa tu! Watalii wengi hupenda kutembelea makumbusho ya Mandela, beach za Cape Town na Mbuga maarufu ya Kruger National Park.

Kiuhalisia Tanzania tuna makumbusho nzuri za freedom fighters wa kusini mwa Afrika zilizopo Bagamoyo, Morogoro na Mtwara na pia Makumbusho ya Mwalimu Nyerere ambae kwa sehemu kubwa anaheshimika sana duniani. Ukiuliza kwa nini hazifahamiki jibu ni moja tu! Hatujazitangaza vya kutosha duniani huko! Na huu ndo ukweli! Vitu vyetu vizuri hatuvitangazi !

Kwa Kruger National Park ya South Afrika Hii ni sawa na nusu au robo ya Mikumi National Park. Kwa idadi ya wanyama haifikii Serengeti au Selous hata kwa robo tu, Ila Leo hii duniani huko ni watu wachache sana wanaijua Selous. Pamoja na Serengeti na Ngorongoro kufahamika ila bado hatujazipa promo za kutosha duniani huko! Selous ambayo kiuhalisia ina wanyama wengi kuliko hata Serengeti haitembelewi hata na watalii 10000 tu kwa mwaka na sababu kuu ni kwamba hatujaitangaza na haijulikani! Kweli kwa muda mrefu tumekuwa kichwa cha mwenda Wazimu!

Kwa beach za Cape Town hizi kwa uzuri hazifikii hata robo kwa uzuri compared na beach za Zanzibar na Mafia! Ila still wao beach zao zinatwmbelewa na watalii wengi kuliko beach zetu za Zanzibar na Mafia. Shida ni moja tu! Tumekuwa hatujitangazi na kujiuza kwa dunia ipasavyo!

Kabla ya COVID , sekta ya utalii ndo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa zaidi katika kuingiza fedha za kigeni na kwenye pato la Taifa! Imekuwa ikifanya hivi huku Tanzania ikiwa haijawai kupokea Watalii Milioni 3 tu tangu kupata uhuru! Fedha hizi ndo zimekuwa zikiendesha nchi, kulipa mishahara na kununua madawa! Swali la kujiuliza ni Je hali ingekuwaje Tanzania ingekuwa inapokea watalii Milioni 5 au 7 au 8 au 10 kwa mwaka? Leo hii si tungekuwa na maendeleo makubwa sana?

Kusema kweli napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa Hii Royal Tour, napenda sana tufanye season 2 ya Royal Tour ambapo tuionyeshe Dunia makubwa zaidi yaliyopo Tanzania.

Napenda kushauri kuwa sasa kuwe na Tangazo la kuitangaza Tanzania kwenye channel kubwa kama CNN, Al Jazeera na BBC, kuwe pia na Matangazo ya Tanzania kwenye klabu kubwa duniani kama Barcelona au Real Madrid au Liverpool au Chelsea

Tuvute mikataba nao na tuuze bidhaa zetu hata korosho na kahawa kwenye stadiums zao!

Hongera Rais Samia! Umeanza vizuri, Royal Tour iwe mwanzo tu na wala usiloose focus kwenye hili! Hayo ndo maono ya Rais!
Kukuza mfumuko wa bei kwenye kila bidhaa ndiyo wenye mnataka afanye ?
 
Wewe ni miongoni mwa wale waliopigwa pini na JPM sasa umerudi kwenye shimo lako ndio maana unaongea hovyo.

Ulikuwa unalia sana hapa awamu ya tano.
Huyu chawa anajiona ameshafika.
 
Kwa hiyo wewe ndiyo unajiona una akili ? You must be a narcissist, narcissism ni ugonjwa wa akili!
Watanzania hatuwezi kushauri bila dharau, kejeli na matusi. Wewe shauri ili nchi isonge mbele.
 
Back
Top Bottom