Rais Samia anafanya kile ambacho wengi wenye akili tunataka afanye! Kwa hili anastahili pongezi

Rais Samia anafanya kile ambacho wengi wenye akili tunataka afanye! Kwa hili anastahili pongezi

Kwa miaka mingi sana Tanzania tumekuwa tunalalamika jambo moja kuu, nalo ni kwamba, pamoja na kuwa na maliasili na utajiri mwingi ila nchi yetu hasa wananchi wamekuwa masikini sana!

Mjadala huu umezungumzwa na kipindi kirefu sana na moja ya sababu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Tanzania kuendelea kuwa masikini pamoja na kuwa na utajiri na Maliasili nyingi ni kwa sababu tumekuwa hatutumii utajiri wetu vizuri ikiwemo kuutangaza kwa dunia ili utunufaishe kiuchumi! Siku zote biashara ni Matangazo!

Kwenye hili suala napenda leo nikiri kuwa Rais Samia ameanza kulipatia majibu suala hili!

Kwa Bara la Afrika, nchi zinazoongoza kwa kupokea watalii wengi ni Morocco, Algeria, Misri na South Africa. Nchi hizi zinapokea watalii zaidi ya Mil 5 hadi Mil 10 kwa mwaka. Na kusema kweli hizi nchi utalii unazinufaisha sana! Kiuhalisia hizi ndo nchi zenye Uchumi mkubwa Afrika na ndo zinaongoza kwa kuwa na chumi imara na maisha bora kwa sehemu kubwa ya wananchi wake!

Ila kwa uhalisia, Kama umetembelea nchi hizi zinazoongoza kwa utalii Africa utagundua kuwa hazina kitu kikubwa kuizidi Tanzania na ukweli ni kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kuzizidi nchi zote hizi.

Kwa South Africa tu! Watalii wengi hupenda kutembelea makumbusho ya Mandela, beach za Cape Town na Mbuga maarufu ya Kruger National Park.

Kiuhalisia Tanzania tuna makumbusho nzuri za freedom fighters wa kusini mwa Afrika zilizopo Bagamoyo, Morogoro na Mtwara na pia Makumbusho ya Mwalimu Nyerere ambae kwa sehemu kubwa anaheshimika sana duniani. Ukiuliza kwa nini hazifahamiki jibu ni moja tu! Hatujazitangaza vya kutosha duniani huko! Na huu ndo ukweli! Vitu vyetu vizuri hatuvitangazi !

Kwa Kruger National Park ya South Afrika Hii ni sawa na nusu au robo ya Mikumi National Park. Kwa idadi ya wanyama haifikii Serengeti au Selous hata kwa robo tu, Ila Leo hii duniani huko ni watu wachache sana wanaijua Selous. Pamoja na Serengeti na Ngorongoro kufahamika ila bado hatujazipa promo za kutosha duniani huko! Selous ambayo kiuhalisia ina wanyama wengi kuliko hata Serengeti haitembelewi hata na watalii 10000 tu kwa mwaka na sababu kuu ni kwamba hatujaitangaza na haijulikani! Kweli kwa muda mrefu tumekuwa kichwa cha mwenda Wazimu!

Kwa beach za Cape Town hizi kwa uzuri hazifikii hata robo kwa uzuri compared na beach za Zanzibar na Mafia! Ila still wao beach zao zinatwmbelewa na watalii wengi kuliko beach zetu za Zanzibar na Mafia. Shida ni moja tu! Tumekuwa hatujitangazi na kujiuza kwa dunia ipasavyo!

Kabla ya COVID , sekta ya utalii ndo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa zaidi katika kuingiza fedha za kigeni na kwenye pato la Taifa hapa Tanzania! Imekuwa ikifanya hivi huku Tanzania ikiwa haijawai kupokea Watalii Milioni 3 tu tangu kupata uhuru! Fedha hizi ndo zimekuwa zikiendesha nchi, kulipa mishahara na kununua madawa! Swali la kujiuliza ni Je hali ingekuwaje Tanzania ingekuwa inapokea watalii Milioni 5 au 7 au 8 au 10 kwa mwaka? Leo hii si tungekuwa na maendeleo makubwa sana?

Kusema kweli napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa Hii Royal Tour, napenda sana tufanye season 2 ya Royal Tour ambapo tuionyeshe Dunia makubwa zaidi yaliyopo Tanzania.

Napenda kushauri kuwa sasa kuwe na Tangazo la kuitangaza Tanzania kwenye channel kubwa kama CNN, Al Jazeera na BBC, kuwe pia na Matangazo ya Tanzania kwenye klabu kubwa duniani kama Barcelona au Real Madrid au Liverpool au Chelsea

Tuvute mikataba nao na tuuze bidhaa zetu hata korosho na kahawa kwenye stadiums zao!

Hongera Rais Samia! Umeanza vizuri, Royal Tour iwe mwanzo tu na wala usiloose focus kwenye hili! Hayo ndo maono ya Rais!
Lakini ulisha wahi kuona rais Kagame ana acha ikulu yake kutembelea Arsenal au UK kwa mwezi mzima?
 
Kuhusu wizi, ufisadi na ubadhirifu, umesema vema. Ni tatizo kubwa kwa nchi yetu.

Ulipoharibu ni pale uliposema eti Magufuli aliamua kupambana na hili. Ukweli ni kwamba Magufuli.aliwazuia au kuwaondoa wevi, mafisadi na wabadhirifu wa mwanzo, kisha akatengeneza wa kwake, huku yeye mwenyewe akishiriki kikamilifu katika uovu huo, wakati huo huo akiwapumbaza watu kuwa anapambana na uovu.

Report ya CAG, imeweka wazi ambayo wengi wa waliopumbazwa na uwongo wa marehemu Magufuli, ambapo watu wake wa karibu wakiwa ndiyo mirija ya kuibia pesa ya umma. Mayanga ni mfano wa awali.
Kwanini chuki zako za kuzuiwa usifanye biashara za magendo na kulipia kodi ipasavyo kupitia control no ktk awamu ya 5 zikufanye uwe mpuuzi kulazimisha kila Mtu amchukie Mwamba wa duniani Hayati JPM [emoji848][emoji19]
 
Lakini ulisha wahi kuona rais Kagame ana acha ikulu yake kutembelea Arsenal au UK kwa mwezi mzima?
Kwa hiyo sasa hivi rais Samia anapewa breifings za intellegencia za nchi muda wote akiwa uagaibuni sio?
 
Lakini ulisha wahi kuona rais Kagame ana acha ikulu yake kutembelea Arsenal au UK kwa mwezi mzima?
Hata Kagame juzi kaenda Uganda kwa siku mbili kusherekea birthday ya Mtoto wa Museveni Muhoozi Kaenerugaba
 
Kwanini chuki zako za kuzuiwa usifanye biashara za magendo na kulipia kodi ipasavyo kupitia control no ktk awamu ya 5 zikufanye uwe mpuuzi kulazimisha kila Mtu amchukie Mwamba wa duniani JPM [emoji848][emoji19]
Mwamba wa kuua, kuteka na kupiga risasi watu?
 
Lazaro nyarandu alifanya Royal Tour?
Neno Royal ndiyo linakubabaisha?

Theme ilikuwa ileile tu haya mengine ni porojo na kula kodi zetu tu.

Halafu mmebebana washamba tu,mlitakiwa mtoe mpunga wa maana muwakutanishe Chris Rock na Will Smith pale Los Angeles kwenye tamasha lenu halafu nyie mnarudi nyumbani.

Mpaka sasa hiyo "Low you Tour" ingekuwa ina trend huko USA,watu wangeitafuta wenyewe.

Hao uliowataja kufanya vizuri,hakuna Rais hata mmoja aliyeenda "kuzurura" huko na battalion ya wanenguaji.
 
Kukaa Marekani unamaanisha nini? Rais yupo Marekani Kikazi na anafanya kazi za kuliletea maendeleo Taifa huko Marekani! Shida iko wapi?

Unataka akae Tanzania tu Tanzania wakati kuna kazi muhimu za kufanya Marekani? Utakuwa na mtindio wa ubongo
Balozi wa Tanzania nchini Marekani anafanya kazi gani? Labda kama maza anafikiri Tanzania ni jimbo la Marekani na yeye ni gavana wa jimbo hilo.
 
Shida ita tokea mkuu wa Majeshi atakapo tangaza kuwa huyu mama atarudi Tanzania kama raia wengine na si mkuu wa nchi kama Idi Amini alivyo fanya kwa Obete miaka hiyo.
Na utashangaa jinsi Watanzania wanafiki watakavyo shangilia. Sababu anaweze sema kuwa hiki kiti hakimfai huyo mama tunahitaji katiba mpya na uchaguzi mpya ndani ya miezi mitatu ,nani atapinga Tanzania? Wote watashangilia.
 
Kukaa Marekani unamaanisha nini? Rais yupo Marekani Kikazi na anafanya kazi za kuliletea maendeleo Taifa huko Marekani! Shida iko wapi?

Unataka akae Tanzania tu Tanzania wakati kuna kazi muhimu za kufanya Marekani? Utakuwa na mtindio wa ubongo
hyo kaz binafs au ya kiserikali kama ya kiserikali kwa nn ujio wake hata BIDEN hautambui
ni profit kwa tanzania kwa nini Kkwete nae yupo USA back bencher kijana ujui kitu tulia ....
 
Mzee mabalozi wakitangaza haiwi sawa na raisi
Pia mtoa mada kasema point sana kuwa tuwe na matangazo ya utalii katika channel kubwa dunian
Licha ya kuwa tutatumia pesa but am sure pesa yetu itarudi zaidi
Itarudi kwa wananchi?
 
Kwamba unachukia sana wauwaji? Kwamba kama Samia nae akiwa muuwaji utamchukia pamoja na hayo mazuri yake unayoyaeleza?
Hata yeye akiwa na tabia za kuua, kuteka na kupiga risasi watu tutatofautiana
 
hyo kaz binafs au ya kiserikali kama ya kiserikali kwa nn ujio wake hata BIDEN hautambui
ni profit kwa tanzania kwa nini Kkwete nae yupo USA back bencher kijana ujui kitu tulia ....
Inaelekea usipomtaja kikwete unaumwa
 
Back
Top Bottom