Rais Samia analazimisha kuizanzibarisha Tanganyika kwa nguvu

Watastaafu baada ya yeye kuondoka watanganyika mkitaka. Ukiingia ofisini wazanzibari wote unawapa uhamisho, unawahamishia Zanzibar.
 
Nawasilisha.
Mada yako hii inastahili jibu linalojitosheleza; lakini kwa sasa hivi ninalo hili la kukueleza kifupi tu ili ulipime na mada husika.
Akina Makonda (Bashite) wakati huu wanapewa nafasi. Hawa siyo waZanzibari; unajua kwa nini?

Ili huyo mteuzi afanikishe zaidi anayoyafanya wakati huu baada ya hao akina Makonda kumrudisha kwenye ngwe yake mwenyewe.

Wewe hapa unalalamikia waZanzibari?

Mbona hawa ni rasha rasha tu, wakati waTanganyika wakirudishwa kwenye himaya ya waarabu!

Kwa hiyo mada yako umeinyima wigo wake unaostahili, kwa kuzungumzia jambo dogo zaidi, huku jambo kubwa linalo hatarisha nchi yetu sote tukiwa hatujalitupia darubini.

WaZanzibari wote wanaweza kuhamia Tanganyika na pasiwepo na madhara yoyote. Haya mengine ambayo Samia anayafanya na ambayo bado hatujayapa fikra zaidi ndiko huko kuliko na hatari zaidi kwa nchi yetu.

Ni lazima tuanze kukazia darubini huko.
 
Binafsi sioni tatizo hapo. Huwa sipendi tabia ya ubaguzi ubaguzi tena hao wazanzibari ni watenda haki sana unapowakuta kwenye ofisi za uma, wengi wao wana hofu ya Mungu.
 
Watastaafu baada ya yeye kuondoka watanganyika mkitaka. Ukiingia ofisini wazanzibari wote unawapa uhamisho, unawahamishia Zanzibar.
Huyu Mama anawaharibia wenzake, hajui tu. Na wasiwasi watu watawarudishia hawachelewi kuuza kila kisiwa labda abadili katiba na kupunguza madaraka ya Rais wa URT.
 
Ujifunze kukaa ndani ya mada. Una uwezo wakuanzisha thread nyingine ya mhuni Makonda na tukaja tukachangia pia.
 
utaratibu huu ulianza awamu ya 5, acha kazi iendelee....... Mwamba alikuwa anateua ndg zake kwa wingi watu wakiuliza mnasema kwani siyo Watanzania? Mama nae anateua wazenji kwani siyo watanzania, mwamba kuna kipindi alihamishia kazi za serikali chato, watu wakahoji mkawa mnajibu kwani chato siyo tz? Sasa tunaelekea kizimkazi, tulieni dawa iwaingie. Jamhuri ya muungano wa Tz........
 
Nyerere pia aliiba Kura Zanzibar 95.
 
Angalia pia na Watanganyika wenye vyeo mpaka Ikulu halafu ulete tena uzi.
Kelele za watanganyika kukosa kazi baada ya kuhitimu zipo dhahiri.
Sikiliza pia kelele za Wazanzibari. Ukiona kwako kwaungua ujue kwa mwinzio kwateketea.
Idadi ya watu wa Zanzibar (Pemba, Unguja na visiwa vingine) haipindukii milioni moja. Tanganyika ina idadi ya zaidi ya watu milioni 64. Sasa iweje Zanzibar yenye watu wachache kiasi
Hata kujua kinahoendelea hujui halafu unaleta longolongo jukwaani kwa ujinga ( ignorance).

Sikiliza: Kwa mujibu wa sensa ya mwisho, Tanzania ina watu milioni 62, kati ya hai milini 1.8 ni Wazanzibari. Sasa hiyo ya chini ya milioni moja imetoka kwako. Umelala, wewe ni mbumbu au umejawa na chuki? Zanzibar na Wazanzibari ilikuwepo kabla hujazaliwa na itaendelea kuwepo hata baada ya wewe na mimi kuondoka.
 
Mtoa mada unasahau kwamba wanzibari wote ni watanzania na sifa za uteuzi katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa umma sharti uwe mtanzania.
 
Mkuu wa wilaya niliyopo ni mzanzibar na katibu wa ccm wilaya ni mzanzibar
 
Mkuu mm siongei juu ya historia ya Tanganyika na Zanzibar. Naongea juu ya uwiano wa idadi ya watu ukilinganisha na ugawaji wa vyeo vinavyogawiwa ovyo kwa kukiuka katiba.

Pili, Rais hana mamlska kisheria na kikatiba kumteua mzanzibar kuwa RAS, DAS au mkurugenzi na kumleta hapa Tanganyika.

Acha ujuaji uchwara kasome katiba ya nchi. Ni kwa vile Rais hashtakiki mahakamani. Ndio maana tunamshtaki kwenye mahakama ya umma hapa JF. Usijifanye mjuaji wakati hujui kitu.
 
Mlipenda wenyewe,na mvimbe mpasuke.
Acha muisome nambaaaa.
 
Mtoa mada unasahau kwamba wanzibari wote ni watanzania na sifa za uteuzi katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa umma sharti uwe mtanzania.
Watanganyika tunaweza kufanya kazi katika Serikali na Taasisi za Umma Zanzibar???
 
Chanzo cha haya yote ni uwepo wa Muungano wa kidwanzi; yaani Muungano wa changu changu, chako changu. I wish kila nchi ingejitegemea kivyake kwa [emoji817]%
Hii ndio hoja na mleta mada anaweza kuonekana kama labda ana chuki ila dah kwa Sasa speed ni kubwa mno hadi sio poa
 
Unalalamika kitu gani wakati uvunjaji wa sheria na taratibu za utumishi wa ummaa aliuanza jpm tukamshangilia na kumpongeza? Aliteua wanasiasa na mtu yeyote aliyemtaka na kuwapa vyeo ktk utumishi wa umma, wanajeshi & polisi wakapewa vyeo vya kisiasa. Nafasi za kuteua makada kama vile maDC, maRC nk hazikumtosha, makada watiiufu wakazawadiwa hadi uDAS, uDED nk, Bashiru katibu mkuu wa chama cha siasa akateuliwa kuwa KM kiongozi. Kama alifanya hivyo tukanyamaza kwann hisiwe kwa Samia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…