Rais Samia analazimisha kuizanzibarisha Tanganyika kwa nguvu

Nyerere alijaza watu wa kanda ya ziwa serikalini miaka lle ya awamu ya kwanza.

Mwinyi akajaza jamaa zake kina RIP Hassan Diria na Fatuma Said Ali katika serikali yake awamu ya pili.

Mkapa, Kikwete hali kadhalika wameendeleza hulka hiyo hiyo. Ni mbaya kwa mtazamo wa jumla lakini ni kielelezo cha kiongozi anayetaka amani katika awamu yake haswa ile ya kikazi.
 
Unaweza kwenda Zanzibar kama ni mtu wa bara upewe madaraka ili tudhibitishe huu uundwaji wa Tanzania?
Kwanini uende Zanzibar wakati huku bara kuna ardhi nyingi sana hata hatujaigusa?.

Siasa nyepesi za kunyoosheana vidole huzaa chuki na nongwa, vitu ambavyo hutuongezea misongo ya mawazo.
 
Kwanini uende Zanzibar wakati huku bara kuna ardhi nyingi sana hata hatujaigusa?.

Siasa nyepesi za kunyoosheana vidole huzaa chuki na nongwa, vitu ambavyo hutuongezea misongo ya mawazo.
Uongozi ni ardhi, au Kila mtu akienda mahali anafuata ardhi? Jibu swali, unaweza kwenda kupata madaraka Zanzibar ukiwa mtu wa bara ili tuone huo muungano una maana gani?
 
Wanaweza wakajazwa watanganyika watupu na bado usiwe wewe kwenye hizo teuzi.Na Na hata hao watanganyika watakaojazwa wanaweza wasiwe na msaada wowote kwako wala kwa nduguzo
Mkuu bado hujaelewa maudhui ya hoja yangu. hebu rudia kusoma taratibu utaelewa.
 
Mtoa mada unasahau kwamba wanzibari wote ni watanzania na sifa za uteuzi katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa umma sharti uwe mtanzania.
Mkuu tulia kwanza ukasome katiba ya nchi ukishajua mipaka ya uteuzi wa Rais ndipo uje hapa kutetea ujinga huku unaona kabisa Tanganyika inamezwa na Zanzibar. Jifunze kuwa mzalendo kwa nchi yako ya Tanganyika. Usiruhusu mzanzibar aje kukuteulia watu kutoka kwao Zenj huku vijana wa Tanganyika wakiwa hawana ajira.
 
Wewe binafsi unataka hayo madudu yaendelee? Sisi tunaokemea huu ukengeufu tunakosea wapi?
 
Naongea juu ya uwiano wa idadi ya watu ukilinganisha na ugawaji wa vyeo vinavyogawiwa ovyo kwa kukiuka katiba.
Ukiongea uwiano wa watu unapaswa kuweka takwimu sahihi na sio kutoa yako isiyokuwa sahihi. Hili hukulifanya na ndo nkakuweka sawa kwani hujui na inakurupuka.
Pili, Rais hana mamlska kisheria na kikatiba kumteua mzanzibar kuwa RAS, DAS au mkurugenzi na kumleta hapa Tanganyika.
Hapa tena huijui katiba, nenda kasome tena. Mkuu huna unaloljua unakurupuka tu. Kumbuka tu kwamba muungano ni swala la ksheria na haliaki mihemko. Jilazimishe kuena na wakati, vinginevyo tarajia kukosolewa.
 
Ujifunze kukaa ndani ya mada. Una uwezo wakuanzisha thread nyingine ya mhuni Makonda na tukaja tukachangia pia.
Kwa bahati mbaya hujui kuwa yote niliyo andika hapo yamo ndani ya mada yenyewe.
Hapana, niseme wazi, siyo "bahati mbaya", bali wigo wa akili yako ndio mfinyu, kwamba haukuwezeshi kujua mada inaanzia wapi na kuishia wapi.
 
Mkuu tupunguze kuficha ujinga kidogo vinginevyo hizi shule na vyuo vinavyojengwa Kila kukicha inakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu,Tanzania imetokana na muungano wa nchi mbili Tanganyika na jamuhuri ya watu wa Zanzibar Tanzania sio ya Waliokuwa watanganyika pekee ambao sasa ni Tanzania bara.Jambo la pili katika kumpata Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania wanzanzibari pia wanapiga kura kumchagua Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pia kasoma mambo ya muungano na yasiyo ya muungano kwenye katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
huu muungano ushakuwa mwiba huu.

wao wanashika nafasi zote uku bara adi uongozi namba moja wa nchi lakini wew wa bara hauwezi kupata ata ujumbe wa mtaa ukivuka bahari.

saivi kila wizara nyeti za bara na wao wapo.
 
Kwanini unasema alijifunza kwa Magufuli?. Kwani yeye hana maamuzi yake binafsi?
 
we lofa kahamie hiyo nchi inayoitwa Tanganyika, nchi yetu inaitwa Tanzania. Umezoea ubaguzi we kenge, kahamie huko kwenye nchi za kibaguzi.
Kwahiyo akitamka Tanganyika anabagua, ila akitamka Zanzibar ni mzalendo? Sasa sijui lofa nani kati yako wewe na yeye! 🤣 🤣 🤣
 
Tutaishia kuandikaaaa humu weeee lakini bila msingi wa suluhisho kutumia basi tutauzwa jumla
Opposition parties ndio za kulaumiwa

Hakuna mwongozo
Kila mtu ni msemaji
Social media wamejaa wa kusifu na kuabudu kutoka upinzani na chama tawala…
Mkulu sijui waziri akitimiza wajibu wake tunasifu na kushangilia…
Akina yeriko sijui madele nani viongozi wa …. ni pongezi tuuuu
are we serious na Taifa
Mikutano ni mingi tunazungumziwaaaa weeeh then what!?
Tutahubiri usiku na mchana but kama hatutakuwa bold enough kufanya yatupasayo ‘kwa vitendo’ yote ni kazi bure

Tusiwe bias tafadhalini let’s speak our opinions sio kila kitu kufutafuta tuuuu
Mnakera kwa ufupi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…