Rais Samia analazimisha kuizanzibarisha Tanganyika kwa nguvu

Umeandika vitu vingi ambavyo hata havihusiki huku umeshindwaje kutetea hoja yako bila kumshambulia Magufuli ambaye hata mwenye thread hakumtaja?
 
Sheria gani ianyoruhusu upande mmoja kunyonywa na mwingine ukineemeka? Kama hujui hili suala vizuri ni bora ukae kimya milele. Uliwahi kusikia au kushuhudia mtanganyika akiteuliwa kuwa DC au mkurugenzi huko Zanzibar?
Mkuu narejea tena kukuambia kwamba hujui na hutaki hata kujifunza. Mjinga akielimishwa na bado akawa mjinga, huyu huitwa MPUMBAVU. Ikiwa wewe unaona upande wa Zanzibar unanyonya Tanganyika, wapo tunaoona upande wa Tanganyika unanyonya Zanzibar. Nakuhakikishia tu kwamba najua ninayoyasema, tofauti na wewe. Kuthibitisha kwamba najua ninayoyasema nawe hujui usemayo chukua haya:
1 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Zanzibar anaitwa Suzan Kunambi huyu ni Mtanganganyika.
2 Mkurugenzi wa Mipango na Uendeshaji katika Wizara ys Wanawake, Jinsia na Watoto Zanzibar anaitwa Daima Mkalimoto. Huyu anatoka Tanganyika ie ni Mtanganyika. Wapo wengi mpaka majaji wa mahakama kuu. Sasa wewe fanya utafiti utayajua haya, ila najua hutofanya kwani hamna kitu kichwani hivyo utakuja na madai yasiyokuwa na ushahidi.
Asante. Naitwa Zawadini. Natokea Zanzibar.
 
Mkuu kwani huu uzi unahusu masuala ya kutafuta hela au unalenga uvunjivu wa katiba anaoufanya rais kwa kuwateua wapemba kushika nafasi za watanganyika? Elewa mada kwanza kabla ya kuchangia.
 
Magufuli mwenyewe alisemwa anajaza wasukuma.Sasa yamekuwa ya Samia Suluhu.Sasa sijuwi mnataka nini nyie mbwa.
Mkuu hivi huwezi kutetea hoja bila kutanguliza matusi? Noona unatafuta ban kwa nguvu.
 
CCM mbele kwa mbele.Kwani Zanzibar siyo Tanzania kama Chato?
 
Sahihi kabisa.
 
Uongozi ni ardhi, au Kila mtu akienda mahali anafuata ardhi? Jibu swali, unaweza kwenda kupata madaraka Zanzibar ukiwa mtu wa bara ili tuone huo muungano una maana gani?
Ardhi ya huku bara tunakufa tukiiacha kubwa tu, maheka kwa maheka leo nongwa zetu zitupeke Zanzibar!

Chuki huwa hazina mpango wowote.
 
Sio Kila mtu anataka ardhi boss, kwani sisi tuliojazana hapa Dar tumefuata ardhi? Acha utetezi wa kulazimisha.
Tuachane na vigezo vya chuki na kulipa visasi, huwa havitusaidii. Tunawaona wazenji kama vile wanafaidi sana kumbe wanayo mateso yao mengi tu.
 
Tuachane na vigezo vya chuki na kulipa visasi, huwa havitusaidii. Tunawaona wazenji kama vile wanafaidi sana kumbe wanayo mateso yao mengi tu.
Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?
 
Ardhi ya huku bara tunakufa tukiiacha kubwa tu, maheka kwa maheka leo nongwa zetu zitupeke Zanzibar!

Chuki huwa hazina mpango wowote.
Mkuu hapa hatuongelei suala la ardhi bali tunaongea kuhusu Samia kuvunja katiba ya nchi kwa kuwateua wapemba kushika nafasi za watanganyika. Mfano halisi ni yule mpemba wa NECTA. Ina maana hata huyu mpemba siku anatangaza matokeo hukumuona au unatetea ujinga bila sababu za msingi mkuu?
 
Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?
Hili limuungano halina faida yoyote zaidi ya kuendelea kuwanyonya na kuwatumikisha watanganyika bila sababu za msingi.
 
Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?
Wapo wengi wenye kuuona una faida, sisi tunaolalamika humu JF tuna maoni tofauti na uhalali wa kinachoendelea kwenye maisha halisi,

Alikuwepo kiongozi wa serikali ya Mapinduzi akiitwa Mwakanjuki alikuwa na cheo cha Brigedia na alipigania uhuru wa Zanzibar, kwa sasa ni marehemu, asili yake ni mkoa wa Mbeya.

Abdallah Natepe kiongozi mwingine mwandamizi wa serikali ya Mapinduzi ambaye pia ni marehemu, huyu alianza miaka ile ya kabla ya mapinduzi yenyewe, mwenyeji wa mkoa wa Mtwara huku bara.

Ni vyema kutafuta habari za kina kuliko kudandia hizi harakati za chuki bila hata ya kuijua kwa kina historia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…