christeve88
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 2,841
- 4,531
Kanuni ni moja tu mtu akikubagua nawe mbague.Huwezi kuona tatizo sababu hujabaguliwa. Jamaa siyo mbaguzi anawanyooshea kidole wabaguzi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kanuni ni moja tu mtu akikubagua nawe mbague.Huwezi kuona tatizo sababu hujabaguliwa. Jamaa siyo mbaguzi anawanyooshea kidole wabaguzi.
Umeandika vitu vingi ambavyo hata havihusiki huku umeshindwaje kutetea hoja yako bila kumshambulia Magufuli ambaye hata mwenye thread hakumtaja?Unalalamika kitu gani wakati uvunjaji wa sheria na taratibu za utumishi wa ummaa aliuanza jpm tukamshangilia na kumpongeza? Aliteua wanasiasa na mtu yeyote aliyemtaka na kuwapa vyeo ktk utumishi wa umma, wanajeshi & polisi wakapewa vyeo vya kisiasa. Nafasi za kuteua makada kama vile maDC, maRC nk hazikumtosha, makada watiiufu wakazawadiwa hadi uDAS, uDED nk, Bashiru katibu mkuu wa chama cha siasa akateuliwa kuwa KM kiongozi. Kama alifanya hivyo tukanyamaza kwann hisiwe kwa Samia?
Mkuu narejea tena kukuambia kwamba hujui na hutaki hata kujifunza. Mjinga akielimishwa na bado akawa mjinga, huyu huitwa MPUMBAVU. Ikiwa wewe unaona upande wa Zanzibar unanyonya Tanganyika, wapo tunaoona upande wa Tanganyika unanyonya Zanzibar. Nakuhakikishia tu kwamba najua ninayoyasema, tofauti na wewe. Kuthibitisha kwamba najua ninayoyasema nawe hujui usemayo chukua haya:Sheria gani ianyoruhusu upande mmoja kunyonywa na mwingine ukineemeka? Kama hujui hili suala vizuri ni bora ukae kimya milele. Uliwahi kusikia au kushuhudia mtanganyika akiteuliwa kuwa DC au mkurugenzi huko Zanzibar?
Mkuu kwani huu uzi unahusu masuala ya kutafuta hela au unalenga uvunjivu wa katiba anaoufanya rais kwa kuwateua wapemba kushika nafasi za watanganyika? Elewa mada kwanza kabla ya kuchangia.Tafuteni hela
Ni umasikini tu ndio huwa unavinasaba vya ubaguzi....
Wabongo wenye hela zao, hususani wafanya biashara huwezi kuwasikia wanalialia, kawaida wale waliotopea kwenye hizi ajira za utumishi ndio huwa njaa kali na kila siku kutafuta mchawi wa umasikini wao...
Au Muungano tuachane nao kabisa!Chanzo cha haya yote ni uwepo wa Muungano wa kidwanzi; yaani Muungano wa changu changu, chako changu. I wish kila nchi ingejitegemea kivyake kwa 💯%
CCM mbele kwa mbele.Kwani Zanzibar siyo Tanzania kama Chato?Tulizoea kuona wazaznzibar (maarufu kwa jina la wapemba) wametapakaa kila mahali hapa Tanganyika wakifanya biashara na shughuli nyingine za kiuchumi. Hili kama watanganyika hatuna shida nalo. Hawa ni wajasiriamali na watafutaji kama walivyo watu wa mataifa mengine waliomo hapa nchini. Tunao wachina, wahindi, wakenya, n.k, na haijawahi kuwa shida.
Kinachoudhi na kusikitisha zaidi ni kitendo cha Rais Dr Samia kuwachukua wazanzibar (hata wasiokuwa na vigezo) na kuwapa vyeo hapa Tanganyika wakati watanganyika hawana kazi. Ukitembelea kwenye ofisi za umma utashangaa kuona utitiri wa wazanzibar wakiwa wamepewa nyadhfa mbali kama vile wakurugenzi, DAS, RAS, wakuu wa mashirika ya umma, wenyeviti wa bodi mbalimbali, n.k. Rais anafanya haya yote kwa makusudi na kwa lazima huku akiwaacha watanganyika wakipuyanga bila kazi. Huu ni zaidi ya uhujumu uchumi.
Ndugu wanaJF na wananchi kwa ujumla, tuhuma hizi hazijaanza leo. Soma baadhi ya nyuzi zilizowahi kuwekwa humu kulalamikia upendeleo unaofanywa na mamlaka kwenye teuzi mbalimbali:
1. Teuzi za Rais Samia zina upendeleo?
2. Teuzi za Rais Samia kulikoni?
3. Wafahamu Wajumbe wa Bodi ya TCRA iliyovunjwa
Kelele za watanganyika kukosa kazi baada ya kuhitimu zipo dhahiri. Hata humu JF siku za karibuni kumekuwa na nyuzi nyingi zinazoonyesha wasomi wa Tanganyika kuhitimu vyuo vikuu na kuishia kufanya kazi za ovyo ovyo wakati kazi walizostahili kufanya zinagawiwa ovyo kwa wazanzibar. Nyuzi zifuatazo ni sehemu ya ushahidi huo:
1. Nimekutana na Degree Graduate wa HR kutoka Mzumbe anauza Pub
2. Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!
3. Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi
MAONI YANGU
Idadi ya watu wa Zanzibar (Pemba, Unguja na visiwa vingine) haipindukii milioni moja. Tanganyika ina idadi ya zaidi ya watu milioni 64. Sasa iweje Zanzibar yenye watu wachache kiasi hiki wananchi wake wapewe kipaumbele huku watanganyika walio wengi wanaendelea kusaga meno?
Ifike mahali katiba itamke bayana idadi ya nafasi wanazostahili wazanzibar (kwa kufuata uwiano wa idadi ya watu) badala ya kufanya teuzi kibubu na kusababisha malalamiko. Na tunapendekeza hili jambo liingizwe kwenye katiba mpya kabisa ili kukata mzizi wa fitna.
Nawasilisha.
Sahihi kabisa.Hii issue naona kila siku tutazidi kulaumiana tu, ikipatikana Katiba bora ikawabana hawa jamaa kufanya haya mambo ndio tutapata majibu ya maana, lakini tofauti na hapo sioni kama midomo yetu itakuja kuwafunza chochote hawa watawala.
Bila shaka Samia alijifunza kwa Magufuli, akaona jinsi mambo yalivyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake, nae amekuja kuendeleza pale alipoishia mtangulizi wake, inshort ana experience na exposure ya kile anachokifanya ndio maana haogopi chochote.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kwani ni uongo?Magufuli mwenyewe alisemwa anajaza wasukuma.Sasa yamekuwa ya Samia Suluhu.Sasa sijuwi mnataka nini nyie mbwa.
Hata kuwa tu VEO mkuu hakuna, huku Wazanzibar wamejaa utadhani ni kwao INAKERA
Ardhi ya huku bara tunakufa tukiiacha kubwa tu, maheka kwa maheka leo nongwa zetu zitupeke Zanzibar!Uongozi ni ardhi, au Kila mtu akienda mahali anafuata ardhi? Jibu swali, unaweza kwenda kupata madaraka Zanzibar ukiwa mtu wa bara ili tuone huo muungano una maana gani?
Waliouweka huu muungano namna ulivyo waliona uhalali wa kufanya hivyo miaka ile.Unaweza kwenda Zanzibar kama ni mtu wa bara upewe madaraka ili tudhibitishe huu uundwaji wa Tanzania?
Sio Kila mtu anataka ardhi boss, kwani sisi tuliojazana hapa Dar tumefuata ardhi? Acha utetezi wa kulazimisha.Ardhi ya huku bara tunakufa tukiiacha kubwa tu, maheka kwa maheka leo nongwa zetu zitupeke Zanzibar!
Chuki huwa hazina mpango wowote.
Tuachane na vigezo vya chuki na kulipa visasi, huwa havitusaidii. Tunawaona wazenji kama vile wanafaidi sana kumbe wanayo mateso yao mengi tu.Sio Kila mtu anataka ardhi boss, kwani sisi tuliojazana hapa Dar tumefuata ardhi? Acha utetezi wa kulazimisha.
Akina nani waliuweka, kwani ni lazima tufuate mawazo Yao hata kama yana walakini? Uhalali wa miaka hiyo hauna uhalali wa miaka hii.Waliouweka huu muungano namna ulivyo waliona uhalali wa kufanya hivyo miaka ile.
Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?Tuachane na vigezo vya chuki na kulipa visasi, huwa havitusaidii. Tunawaona wazenji kama vile wanafaidi sana kumbe wanayo mateso yao mengi tu.
Mkuu hapa hatuongelei suala la ardhi bali tunaongea kuhusu Samia kuvunja katiba ya nchi kwa kuwateua wapemba kushika nafasi za watanganyika. Mfano halisi ni yule mpemba wa NECTA. Ina maana hata huyu mpemba siku anatangaza matokeo hukumuona au unatetea ujinga bila sababu za msingi mkuu?Ardhi ya huku bara tunakufa tukiiacha kubwa tu, maheka kwa maheka leo nongwa zetu zitupeke Zanzibar!
Chuki huwa hazina mpango wowote.
Hili limuungano halina faida yoyote zaidi ya kuendelea kuwanyonya na kuwatumikisha watanganyika bila sababu za msingi.Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?
Wapo wengi wenye kuuona una faida, sisi tunaolalamika humu JF tuna maoni tofauti na uhalali wa kinachoendelea kwenye maisha halisi,Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?