Rais Samia analazimisha kuizanzibarisha Tanganyika kwa nguvu

Rais Samia analazimisha kuizanzibarisha Tanganyika kwa nguvu

Unalalamika kitu gani wakati uvunjaji wa sheria na taratibu za utumishi wa ummaa aliuanza jpm tukamshangilia na kumpongeza? Aliteua wanasiasa na mtu yeyote aliyemtaka na kuwapa vyeo ktk utumishi wa umma, wanajeshi & polisi wakapewa vyeo vya kisiasa. Nafasi za kuteua makada kama vile maDC, maRC nk hazikumtosha, makada watiiufu wakazawadiwa hadi uDAS, uDED nk, Bashiru katibu mkuu wa chama cha siasa akateuliwa kuwa KM kiongozi. Kama alifanya hivyo tukanyamaza kwann hisiwe kwa Samia?
Umeandika vitu vingi ambavyo hata havihusiki huku umeshindwaje kutetea hoja yako bila kumshambulia Magufuli ambaye hata mwenye thread hakumtaja?
 
Sheria gani ianyoruhusu upande mmoja kunyonywa na mwingine ukineemeka? Kama hujui hili suala vizuri ni bora ukae kimya milele. Uliwahi kusikia au kushuhudia mtanganyika akiteuliwa kuwa DC au mkurugenzi huko Zanzibar?
Mkuu narejea tena kukuambia kwamba hujui na hutaki hata kujifunza. Mjinga akielimishwa na bado akawa mjinga, huyu huitwa MPUMBAVU. Ikiwa wewe unaona upande wa Zanzibar unanyonya Tanganyika, wapo tunaoona upande wa Tanganyika unanyonya Zanzibar. Nakuhakikishia tu kwamba najua ninayoyasema, tofauti na wewe. Kuthibitisha kwamba najua ninayoyasema nawe hujui usemayo chukua haya:
1 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Zanzibar anaitwa Suzan Kunambi huyu ni Mtanganganyika.
2 Mkurugenzi wa Mipango na Uendeshaji katika Wizara ys Wanawake, Jinsia na Watoto Zanzibar anaitwa Daima Mkalimoto. Huyu anatoka Tanganyika ie ni Mtanganyika. Wapo wengi mpaka majaji wa mahakama kuu. Sasa wewe fanya utafiti utayajua haya, ila najua hutofanya kwani hamna kitu kichwani hivyo utakuja na madai yasiyokuwa na ushahidi.
Asante. Naitwa Zawadini. Natokea Zanzibar.
 
Tafuteni hela
Ni umasikini tu ndio huwa unavinasaba vya ubaguzi....
Wabongo wenye hela zao, hususani wafanya biashara huwezi kuwasikia wanalialia, kawaida wale waliotopea kwenye hizi ajira za utumishi ndio huwa njaa kali na kila siku kutafuta mchawi wa umasikini wao...
Mkuu kwani huu uzi unahusu masuala ya kutafuta hela au unalenga uvunjivu wa katiba anaoufanya rais kwa kuwateua wapemba kushika nafasi za watanganyika? Elewa mada kwanza kabla ya kuchangia.
 
Magufuli mwenyewe alisemwa anajaza wasukuma.Sasa yamekuwa ya Samia Suluhu.Sasa sijuwi mnataka nini nyie mbwa.
Mkuu hivi huwezi kutetea hoja bila kutanguliza matusi? Noona unatafuta ban kwa nguvu.
 
Tulizoea kuona wazaznzibar (maarufu kwa jina la wapemba) wametapakaa kila mahali hapa Tanganyika wakifanya biashara na shughuli nyingine za kiuchumi. Hili kama watanganyika hatuna shida nalo. Hawa ni wajasiriamali na watafutaji kama walivyo watu wa mataifa mengine waliomo hapa nchini. Tunao wachina, wahindi, wakenya, n.k, na haijawahi kuwa shida.

Kinachoudhi na kusikitisha zaidi ni kitendo cha Rais Dr Samia kuwachukua wazanzibar (hata wasiokuwa na vigezo) na kuwapa vyeo hapa Tanganyika wakati watanganyika hawana kazi. Ukitembelea kwenye ofisi za umma utashangaa kuona utitiri wa wazanzibar wakiwa wamepewa nyadhfa mbali kama vile wakurugenzi, DAS, RAS, wakuu wa mashirika ya umma, wenyeviti wa bodi mbalimbali, n.k. Rais anafanya haya yote kwa makusudi na kwa lazima huku akiwaacha watanganyika wakipuyanga bila kazi. Huu ni zaidi ya uhujumu uchumi.

Ndugu wanaJF na wananchi kwa ujumla, tuhuma hizi hazijaanza leo. Soma baadhi ya nyuzi zilizowahi kuwekwa humu kulalamikia upendeleo unaofanywa na mamlaka kwenye teuzi mbalimbali:

1. Teuzi za Rais Samia zina upendeleo?

2. Teuzi za Rais Samia kulikoni?

3. Wafahamu Wajumbe wa Bodi ya TCRA iliyovunjwa

Kelele za watanganyika kukosa kazi baada ya kuhitimu zipo dhahiri. Hata humu JF siku za karibuni kumekuwa na nyuzi nyingi zinazoonyesha wasomi wa Tanganyika kuhitimu vyuo vikuu na kuishia kufanya kazi za ovyo ovyo wakati kazi walizostahili kufanya zinagawiwa ovyo kwa wazanzibar. Nyuzi zifuatazo ni sehemu ya ushahidi huo:

1. Nimekutana na Degree Graduate wa HR kutoka Mzumbe anauza Pub

2. Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

3. Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi

MAONI YANGU
Idadi ya watu wa Zanzibar (Pemba, Unguja na visiwa vingine) haipindukii milioni moja. Tanganyika ina idadi ya zaidi ya watu milioni 64. Sasa iweje Zanzibar yenye watu wachache kiasi hiki wananchi wake wapewe kipaumbele huku watanganyika walio wengi wanaendelea kusaga meno?

Ifike mahali katiba itamke bayana idadi ya nafasi wanazostahili wazanzibar (kwa kufuata uwiano wa idadi ya watu) badala ya kufanya teuzi kibubu na kusababisha malalamiko. Na tunapendekeza hili jambo liingizwe kwenye katiba mpya kabisa ili kukata mzizi wa fitna.

Nawasilisha.
CCM mbele kwa mbele.Kwani Zanzibar siyo Tanzania kama Chato?
 
Hii issue naona kila siku tutazidi kulaumiana tu, ikipatikana Katiba bora ikawabana hawa jamaa kufanya haya mambo ndio tutapata majibu ya maana, lakini tofauti na hapo sioni kama midomo yetu itakuja kuwafunza chochote hawa watawala.

Bila shaka Samia alijifunza kwa Magufuli, akaona jinsi mambo yalivyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake, nae amekuja kuendeleza pale alipoishia mtangulizi wake, inshort ana experience na exposure ya kile anachokifanya ndio maana haogopi chochote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Sahihi kabisa.
 
Uongozi ni ardhi, au Kila mtu akienda mahali anafuata ardhi? Jibu swali, unaweza kwenda kupata madaraka Zanzibar ukiwa mtu wa bara ili tuone huo muungano una maana gani?
Ardhi ya huku bara tunakufa tukiiacha kubwa tu, maheka kwa maheka leo nongwa zetu zitupeke Zanzibar!

Chuki huwa hazina mpango wowote.
 
Sio Kila mtu anataka ardhi boss, kwani sisi tuliojazana hapa Dar tumefuata ardhi? Acha utetezi wa kulazimisha.
Tuachane na vigezo vya chuki na kulipa visasi, huwa havitusaidii. Tunawaona wazenji kama vile wanafaidi sana kumbe wanayo mateso yao mengi tu.
 
Tuachane na vigezo vya chuki na kulipa visasi, huwa havitusaidii. Tunawaona wazenji kama vile wanafaidi sana kumbe wanayo mateso yao mengi tu.
Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?
 
Ardhi ya huku bara tunakufa tukiiacha kubwa tu, maheka kwa maheka leo nongwa zetu zitupeke Zanzibar!

Chuki huwa hazina mpango wowote.
Mkuu hapa hatuongelei suala la ardhi bali tunaongea kuhusu Samia kuvunja katiba ya nchi kwa kuwateua wapemba kushika nafasi za watanganyika. Mfano halisi ni yule mpemba wa NECTA. Ina maana hata huyu mpemba siku anatangaza matokeo hukumuona au unatetea ujinga bila sababu za msingi mkuu?
 
Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?
Hili limuungano halina faida yoyote zaidi ya kuendelea kuwanyonya na kuwatumikisha watanganyika bila sababu za msingi.
 
Kama hawafaidi si ndio uhalali wa kuachana ulipo? Kama wazenji wanaona muungano hauna faida, na sisi wabara tunaona hauna maana, ni muungano wa Nini Sasa? Au ni muungano wa matambiko?
Wapo wengi wenye kuuona una faida, sisi tunaolalamika humu JF tuna maoni tofauti na uhalali wa kinachoendelea kwenye maisha halisi,

Alikuwepo kiongozi wa serikali ya Mapinduzi akiitwa Mwakanjuki alikuwa na cheo cha Brigedia na alipigania uhuru wa Zanzibar, kwa sasa ni marehemu, asili yake ni mkoa wa Mbeya.

Abdallah Natepe kiongozi mwingine mwandamizi wa serikali ya Mapinduzi ambaye pia ni marehemu, huyu alianza miaka ile ya kabla ya mapinduzi yenyewe, mwenyeji wa mkoa wa Mtwara huku bara.

Ni vyema kutafuta habari za kina kuliko kudandia hizi harakati za chuki bila hata ya kuijua kwa kina historia.
 
Back
Top Bottom