Rais Samia anapaswa kujua kuwa bila Magufuli asingekuwa Rais

Rais Samia anapaswa kujua kuwa bila Magufuli asingekuwa Rais

Kumekuwa na mfululizo wa mashambulizi makali ya maneno ya kisiasa kutoka kwa Rais Samia na wasaidizi wake wa karibu dhidi ya mtangulizi wake marehemu Magufuli.

Binafsi sifurahishwi nayo kwa kuwa yamemlenga mtu aliyekufa (Magufuli) na yanasemwa na waliokuwa wasaidizi wa marehemu Magufuli, ambao waliibuliwa na kubebwa kwa 100% na Magufuli mwenyewe. Kumkana sasa Magufuli na siasa zake kabla ya kuwaomba radhi watanzania waliomizwa na utawala wa Magufuli huku Samia akiwa msaidizi na mshauri mkuu wa Magufuli, ni jambo la fedheha sana.

Yaani mabaya yote ya utawala wa Magufuli (kama ubabe, unyanyasaji, utesaji, wizi) wanasema yalikuwa ya Magufuli mwenyewe, lakini mema yote ya Magufuli (kama ujenzi, miradi, usimamizi, uwajibikaji) wanasema yalikuwa ya wote kwa umoja wao! Huu ni unafiki mkubwa.

Sote tunajua kuwa uchaguzi wa 2015 ulichezewa ili Magufuli aingie madarakani, na uchaguzi wa 2020 ulichezewa na Magufuli mwenyewe kwa 100% ili aendelee kukaa madarakani. Na Magufuli aliyafanya hayo yote kwa maslahi yake binafsi, maslahi ya CCM na maslahi ya wasaidizi wake. Leo hii watu wale wale kumkaanga Magufuli kisiasa ni jambo la ajabu sana.
Kwanini hawakusema hayo wakati Magufuli akiwa bado hai?
Kwanini hawakukaa hata pembeni ili kukwepa kushiriki dhuluma aliyotendwa na Magufuli?

Yaani leo hii Magufuli amegeuzwa na CCM ya mama Samia kuwa dampo la kufichia uchafu wote wa kisiasa unaonuka wa CCM uliofanywa na CCM na serikali yake tangu 2015-2021. Hii hatari sasa.

Ilitosha sana kwa mama Samia na CCM yake kuja kwanza hadharani kuwaomba radhi watanzania kwa utawala mbovu wa Magufuli uliokosa aibu, utu na haki, kisha kutafuta maridhiano ili ukurasa mbovu wa utawala wa Magufuli ufungwe milele katika taifa letu.
Kwanza mimi nafirahi Sana SSH anavyomnanga yule zombie kwa sababu tabia ya kushambulia wastaafu iliasisiwa na Jiwe,hata hiki cha kusema Rais kafanya xy sijui katoa pesa vyote alileta Jiwe ..

Hivyo ni muda muafaka kwa wafuasi wa Jiwe kukinywea kikombe kile kile ambacho Mwendazake alikitumia kuwanyweshea wastaafu wengine hasa JK..

Pili Mwendazake alitakiwa kujua kwamba bila JK yeye asingekuwa Rais hivyo hakupaswa kumnanga na kumdharirisha kwa matusi mbalimbali hadi kufikia kumuita anawashwa washwa..

Samia shikilia hapo hapo ,bahati nzuri tunamtolea kama mfano mbaya na sio kumnanga.
 
Siyo kweli. Kwanza Magufuli ndiyo anapaswa kushukuru kwa kuwa Mgombea. Kwenye kura aliongoza Amina Salum, akafuata Magufuli then Asha Rose Migiro.

Kama Mkapa asingemkomalia Kikwete huyo Mwendazake asingesikika popote
Akili kisoda
 
Kumekuwa na mfululizo wa mashambulizi makali ya maneno ya kisiasa kutoka kwa Rais Samia na wasaidizi wake wa karibu dhidi ya mtangulizi wake marehemu Magufuli.

Binafsi sifurahishwi nayo kwa kuwa yamemlenga mtu aliyekufa (Magufuli) na yanasemwa na waliokuwa wasaidizi wa marehemu Magufuli, ambao waliibuliwa na kubebwa kwa 100% na Magufuli mwenyewe. Kumkana sasa Magufuli na siasa zake kabla ya kuwaomba radhi watanzania waliomizwa na utawala wa Magufuli huku Samia akiwa msaidizi na mshauri mkuu wa Magufuli, ni jambo la fedheha sana.

Yaani mabaya yote ya utawala wa Magufuli (kama ubabe, unyanyasaji, utesaji, wizi) wanasema yalikuwa ya Magufuli mwenyewe, lakini mema yote ya Magufuli (kama ujenzi, miradi, usimamizi, uwajibikaji) wanasema yalikuwa ya wote kwa umoja wao! Huu ni unafiki mkubwa.

Sote tunajua kuwa uchaguzi wa 2015 ulichezewa ili Magufuli aingie madarakani, na uchaguzi wa 2020 ulichezewa na Magufuli mwenyewe kwa 100% ili aendelee kukaa madarakani. Na Magufuli aliyafanya hayo yote kwa maslahi yake binafsi, maslahi ya CCM na maslahi ya wasaidizi wake. Leo hii watu wale wale kumkaanga Magufuli kisiasa ni jambo la ajabu sana.
Kwanini hawakusema hayo wakati Magufuli akiwa bado hai?
Kwanini hawakukaa hata pembeni ili kukwepa kushiriki dhuluma aliyotendwa na Magufuli?

Yaani leo hii Magufuli amegeuzwa na CCM ya mama Samia kuwa dampo la kufichia uchafu wote wa kisiasa unaonuka wa CCM uliofanywa na CCM na serikali yake tangu 2015-2021. Hii hatari sasa.

Ilitosha sana kwa mama Samia na CCM yake kuja kwanza hadharani kuwaomba radhi watanzania kwa utawala mbovu wa Magufuli uliokosa aibu, utu na haki, kisha kutafuta maridhiano ili ukurasa mbovu wa utawala wa Magufuli ufungwe milele katika taifa letu.
Ata huyo mwendazake hakuwaheshimu
Watangulizi wake ambao ndiyo waliompa hiyo nafasi.wacha kutu Ile chuma
 
Kama hujui hizi taarifa, jihesabu wewe ni mtoto mdogo kama Kichuguu. Acha milima tukupe vitu ndiyo nawe ukomae. Endelea kusoma madini toka kwa wajuvi
Hii watu JF kutofahamiana kuna uzuri na ubaya wake. Ungejua Kichuguu ni nani ungeomba radhi haraka sana kwa andiko lako hili.

Mkuu Kichuguu msamehe huyu dogo; anayoandika yanaaksi upeo wake.
 
Bila hayati benjamini William mkapa sio magufuli magufuli hakua na lolote kipindi Cha upitishwaji wa jina
 
Magufuli aliwasema wengine na hata kuwadhalilisha Viongozi waliopita naye akubali kusemwa. Usimtendee mtu mwingine Mambo ambayo hutaki utendewe.
Mkuu tena bora yeye anasemwa akiwa marehemu, yeye aliwatolea kauli za hovyo watangulizi wake hadharani na wakiwepo,hao wanaosema Magufuri hasisemwe mamejiuliza watangulizi wake Magufuri walikuwa wanajisikiaje?.

Si bora yeye anasemwa akiwa haelewi kinachoendelea?.
 
Siyo kweli. Kwanza Magufuli ndiyo anapaswa kushukuru kwa kuwa Mgombea. Kwenye kura aliongoza Amina Salum, akafuata Magufuli then Asha Rose Migiro.

Kama Mkapa asingemkomalia Kikwete huyo Mwendazake asingesikika popote
Amina salum?!!!
Ndo kwanza nasikia hili jina!
 
Acheni kudanganya umma. Bila mkapa JPM angekuwa Rais.

Hoja ya msingi sio Bila Mkapa JPM angekuwa Rais , Hoja ya msingi ni Rais SSH kuendelea kuzungumza mabaya ya JPM as if she was not part of the rotten system ili hali yeye na timu yake haijakiri hadharani kuwa kilichofanywa na JPM wanaomba radhi na haikuwa katika matakwa yao.
Magufuli nae alizungumza mabaya ya kikwete
 
Magufuli angekuwa Rais bila Kikwete. ?

Urais anapanga Mungu shubashiii
Kama unaipinga hoja ya kwamba Magufuri kuwa rais haihusiani na Kikwete kwa kuwa tu urais anapanga Mungu, Kwa nini pia usikubali kuwa Samia kuwa rais si kwa sababu ya Magufururi bali ni kwa kuwa urais anapanga Mungu?.

Watu wengine akili sijui wanapeleka wapi!

Yahani unasema bila Magufuri,Samia hasingekuwa rais, lakini unapinga kwamba bila Kikwete Magufuri hasingekuwa rais kwa hoja kwamba Urais anapanga Mungu. Kwa hiyo urais aliopanga Mungu ni kwa Magufuri tu lakini wa Samia ni Magufuri?.
 
Huyu mama ni incompetent sana hakua na maandalizi yoyote kiufupi yupo yupo tu.
 
Amina ndio aliongoza sio Magufuli. Ndio maana alikataa Mambo ya siasa alijua akiruhusu hatamaliza miaka kumi. Alijitahidi kutengeneza himaya ya kumlinda.
1650190060954.png
 
Magufuli anajadiliwa kuliko baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Hakika JPM alikuwa chaguo la Mungu wa mbinguni.

Tofauti ni kuwa kila akijadiliwa Nyerere yanatajwa mazuri lakini ni tofauti kwa huo mjadala mwingine wengine walisifu ili wapate kuwa relevant.
 
Back
Top Bottom