Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Mkuu kwenye siasa uwongo na kweli vinakuwepo
Kuna muda ukweli unaweza kufanya damage kubwa kuliko uwongo, hapo ndio kuna umuhimu wa kupotezea kuliko kusema
Yes kama swali gumu angesema no comment au angesema wakati ule tulidhani tatizo la Corona dogo au halipo kutokana na kipindi kile elimu kuhusu huo ugonjwa ilikuwa ndogo kwetu lakini baadaye tukaja kugundua kuwa tatizo ni kubwa ndio tukaanza kuchukua hatua stahiki
 
Shida yako ulikiwa umtaje tu Tundu Lissu, na hakusema hivyo ulivyoandika hapa mtu mwenye hila.
Hakusema hivyo? Kaangalie ile interview, halafu tuwekee alichosema
 
Wewe ndio wale wale watu wa kododge maswali, unapenda siasa tupu za kiafrika.
 
wanaomkosoa Rais walipaswa watuambie jee walitaka Rais aseme hakuwahi kutofautiana mawazo na Bosi wake?

kwanini tunataka Rais wetu awe muongo muongo?


sie tunataka dola za Wazungu mwacheni aseme lolote ambalo litarahisisha upatikanaji wa fedha

hata Comrade Kinana aliinanga sana Serikali ya Jakaya 2010-2015 ili kuingiza maboya wananchi tupate ushindi na kweli ushindi ukapatikana …mwanasiasa ili afanikishe lake hutumia 'silaha ' zote
 
Angejibu suala la Corona lilikuwa na ubishi dunia nzima, ikiwepo hata USA yenyewe, na ndani ya serikali walikuwa wakitafiti kabla ya kuchukua hatua zenye athari
 
serikali kuwa organised haimaanishi wote muwe na mawazo yanayofanana kama Mayai

kutofautiana misimamo haimaanishi serikali haina umoja

wewe unadhan kwny mkutano wa kilele wa NATO hivi karibuni unadhan wote kwny kikao walikuwa na mtazamo mmoja kwny kuisaidia Ukraine? mnakuwa na mawazo tofauti japo msimamo wa wengi unageuka kuwa ndio msimamo rasmi hata kama haukubali
 
wanaomkosoa Rais walipaswa watuambie jee walitaka Rais aseme hakuwahi kutofautiana mawazo na Bosi wake?
Hakutakiwa kujibu hivyo linachanganya hadi wawekezaji

Kuwa Serikali haiko organized
Mfano vbali kuwa waweza idhinishiwa mfano na ofisi ya makamu wa Raisi ukapata Kibali cha mambo ya mazingira kuwa jenga kiwanda mazingira safi unajengea Raisi anakuja kukuambia acha unachafua mazingira!! Funga kiwanda!!

Sio kitu kidogo makamu wa Raisi kutofautiana na Raisi
 
Mkuu tanzania bado hakujakuwa na ujasiri huo ama utamaduni huo kwamba ukishindwa kufanya naye mtu kazi wa juu yako ukae pembeni ni vile unabaki na matumaini tu na kuendelea sio kwa mama samia tu hata nyerere alikuwa mtumwa kwa wazungu

Muacheni mama awagonge zile sehemu zenu zenye maumivu, Sasa mumeona mama mwanamke wa kizanzibari alivyopiga hatua kuliko mwendazake mnakosa amani na usingizi., Mama bado yupo sana.
 
Mugabe aliulizwa kuhusu kustaafu akasema yeye kaingia madarakani mwaka 1980, lakin Elizabeth kaingia 1952 na hajawahi kuulizwa hilo
 
Sio kuwa muongo, kuna namna ya kujibu maswali bila kusema uwongo wala kusema ukweli.
Hii lazima Samia aijuie kama ataendelea kufanya interview na vyombo vya nje.
 
ndio utuambie alitakiwa aseme vipi ?
Sio kuwa muongo, kuna namna ya kujibu maswali bila kusema uwongo wala kusema ukweli.
Hii lazima Samia aijuie kama ataendelea kufanya interview na vyombo vya nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…