Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Mkuu kwenye siasa uwongo na kweli vinakuwepo
Kuna muda ukweli unaweza kufanya damage kubwa kuliko uwongo, hapo ndio kuna umuhimu wa kupotezea kuliko kusema
Yes kama swali gumu angesema no comment au angesema wakati ule tulidhani tatizo la Corona dogo au halipo kutokana na kipindi kile elimu kuhusu huo ugonjwa ilikuwa ndogo kwetu lakini baadaye tukaja kugundua kuwa tatizo ni kubwa ndio tukaanza kuchukua hatua stahiki
 
Wewe ndio wale wale watu wa kododge maswali, unapenda siasa tupu za kiafrika.
Mahojiano ya jana ya Rais Samia na Gazeti la New York Times alinukuliwa akisema alipata wakati mgumu kufanya kazi na Hayati Magufuli kutokana na msimamo wa Magufuli juu ya Covid-19.

Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.

Kwa wanaoangalia mahojiano ya viongozi na waandishi wa habari wa nchi za 'mbele' wanajua jinsi waandishi hao wanavyokuwa aggressive, mnakumbuka Tundu Lissu mwenyewe alivyobanwa na mwandishi wa BBC hadi kujikuta ametamka atawapa mashoga haki zao...! Baadae akaja kukana hakumaanisha hivyo, ila sikumlaumu maana unabanwa kwelikweli.

Sasa kwa mtu kama Rais ambaye ana wasaidizi wengi smart walitakiwa ku-anticipate maswali ambayo angeulizwa Rais, na Rais angekua namna ya kuyajibu kabla, kuna maswali mengine unaya-dodge tu badala ya kutoa majibu direct ambayo yataleta utata, ndivyo wanasiasa hufanya.

Wasimuache kama anaenda kuhojiwa TBC.

Nadhani hili halitajirudia tena.
 
wanaomkosoa Rais walipaswa watuambie jee walitaka Rais aseme hakuwahi kutofautiana mawazo na Bosi wake?

kwanini tunataka Rais wetu awe muongo muongo?


sie tunataka dola za Wazungu mwacheni aseme lolote ambalo litarahisisha upatikanaji wa fedha

hata Comrade Kinana aliinanga sana Serikali ya Jakaya 2010-2015 ili kuingiza maboya wananchi tupate ushindi na kweli ushindi ukapatikana …mwanasiasa ili afanikishe lake hutumia 'silaha ' zote
 
Yes kama swali gumu angesema no comment au angesema wakati ule tulidhani tatizo la Corona dogo au halipo kutokana na kipindi kile elimu kuhusu huo ugonjwa ilikuwa ndogo kwetu lakini baadaye tukaja kugundua kuwa tatizo ni kubwa ndio tukaanza kuchukua hatua
Angejibu suala la Corona lilikuwa na ubishi dunia nzima, ikiwepo hata USA yenyewe, na ndani ya serikali walikuwa wakitafiti kabla ya kuchukua hatua zenye athari
 
serikali kuwa organised haimaanishi wote muwe na mawazo yanayofanana kama Mayai

kutofautiana misimamo haimaanishi serikali haina umoja

wewe unadhan kwny mkutano wa kilele wa NATO hivi karibuni unadhan wote kwny kikao walikuwa na mtazamo mmoja kwny kuisaidia Ukraine? mnakuwa na mawazo tofauti japo msimamo wa wengi unageuka kuwa ndio msimamo rasmi hata kama haukubali
Jibu alilojibu raisi linaonyesha Serikali haikuwa organized .Raisi kivyake makamu kivyake utafikiri Serikali ya Sudan kusini kati ya Raisi Salva Kiir na makamu wake Riech machar!! Hakukuwa na unit of command and purpose

Swali je sasa Serikali ya Mama Samia iko organized from bottom to the top? Hilo swali kawaachia homework wamarekani wafanye analysis wenyewe!!
 
wanaomkosoa Rais walipaswa watuambie jee walitaka Rais aseme hakuwahi kutofautiana mawazo na Bosi wake?
Hakutakiwa kujibu hivyo linachanganya hadi wawekezaji

Kuwa Serikali haiko organized
Mfano vbali kuwa waweza idhinishiwa mfano na ofisi ya makamu wa Raisi ukapata Kibali cha mambo ya mazingira kuwa jenga kiwanda mazingira safi unajengea Raisi anakuja kukuambia acha unachafua mazingira!! Funga kiwanda!!

Sio kitu kidogo makamu wa Raisi kutofautiana na Raisi
 
Tuache unafiki, kama mazingira yalikuwa hayaruhusu alilazimishwa kufanya naye kazi, angeweza kuondoka kurudi Unguja akatulie!.

Haya mambo huwa wanadanganywa watoto, but ili upate pesa kwa wakoloni wadanganye vyovyote unavyoweza cha msingi wakupe pesa.
Mkuu tanzania bado hakujakuwa na ujasiri huo ama utamaduni huo kwamba ukishindwa kufanya naye mtu kazi wa juu yako ukae pembeni ni vile unabaki na matumaini tu na kuendelea sio kwa mama samia tu hata nyerere alikuwa mtumwa kwa wazungu

Muacheni mama awagonge zile sehemu zenu zenye maumivu, Sasa mumeona mama mwanamke wa kizanzibari alivyopiga hatua kuliko mwendazake mnakosa amani na usingizi., Mama bado yupo sana.
 
Mugabe aliulizwa kuhusu kustaafu akasema yeye kaingia madarakani mwaka 1980, lakin Elizabeth kaingia 1952 na hajawahi kuulizwa hilo
Nyerere alikuwa kiboko wakati kuna mgogoro Zanzibar wanataka kujitenga muungano Nyerere alienda uingereza akahojiwa kuhusu issue ya mgogoro wa Zanzibar chap chap akawajibu kuwa let us talk about Ireland first !! Sababu mgogoro uingereza na Ireland ni sawa na wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar !! Mwandishi Alahama chap chap akaenda muhoji swali lingine hilo akalitupa kapuni
 
wanaomkosoa Rais walipaswa watuambie jee walitaka Rais aseme hakuwahi kutofautiana mawazo na Bosi wake?

kwanini tunataka Rais wetu awe muongo muongo?


sie tunataka dola za Wazungu mwacheni aseme lolote ambalo litarahisisha upatikanaji wa fedha

hata Comrade Kinana aliinanga sana Serikali ya Jakaya 2010-2015 ili kuingiza maboya wananchi tupate ushindi na kweli ushindi ukapatikana …mwanasiasa ili afanikishe lake hutumia 'silaha ' zote
Sio kuwa muongo, kuna namna ya kujibu maswali bila kusema uwongo wala kusema ukweli.
Hii lazima Samia aijuie kama ataendelea kufanya interview na vyombo vya nje.
 
ndio utuambie alitakiwa aseme vipi ?
Sio kuwa muongo, kuna namna ya kujibu maswali bila kusema uwongo wala kusema ukweli.
Hii lazima Samia aijuie kama ataendelea kufanya interview na vyombo vya nje.
 
Back
Top Bottom