Nadhani katika suala la COVID-19 Magufuli alifanya vizuri, kiuhalisia hofu ilikuwa kubwa kuliko gonjwa lenyewe, mfano hadi mwaka huu April 2022, Tanzania Ina wagonjwa 33,800 wa COVID 19, na vifo takribani 700, katika nchi yenye population of 63M, jamani idadi ya wagonjwa na vifo ni kidogo sana kulinganisha na nchi ambazo zilitumia njia tofauti na Ile aliyotumia Magufuli, Rais anafanya maamuzi kulingana na takwimu za watalaamu, hali halisi ya ugonjwa nchini, na nchi jirani , Bara la Africa na mataifa mengine, kama wewe ni Rais wa nchi Kwa takwimu hizi je ungeweza ku apply lockdown?
Tuongee ukweli tu bila kuwa na mihemko ya so called tuliumizwa or alikuwa dictator, kama Samia hakubaliani na njia iliyotumika na kuwa vusha watanzania walio wengi atueleze Kwa nini sasa hivi haweki lockdown Tanzania? Mbona hata toka aingie madarakani hajafikisha hata 5% ya chanjo Kwa watanzania? 98% ya watanzania hawavai barakoa na watu wanaishi , binafsi sioni tatizo la mbinu alizotumia Magufuli kututoa katika janga hili, kama watu wangekufa hata 10,000 tungesema serikali haikuchua tahadhari na iwajibike, lakini hakuna.
Siku zote Waafrica sisi tulikuwa affected by colonial minds , hatujikubali hata kama tunafanya vitu Kwa ufasaha mpaka hapo western wakisema hili jambo ni sahihi au la, itatuchukua muda sana kuendelea Africa hadi tujitoe kwenye hizo minds za kufanya jambo tukitegemea tupate approval kutoka katika mataifa mengine, huo ni utumwa mkubwa sana wa kifikra ambao tumerithi.
Hivi inawezekana vipi mtu ana kulecture how to control COVID wakati yeye ana vifo million 5 wakati wewe una vifo 10,000? , does it make sense?