Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Hakuwa na msimamo wowote kwani mbona mikutano yake mingi ameonekama havai barakoa. Kama kweli alikuwa anapingana katika mtazamo huo angeonyesha hata kwa yeye kuvaa barakoa bila kuhamasisha wengine.
Ni njia tu za kumsigina mwenzako ili kutaka misaada.
tunasema kulikuwa na hofu ya woga., elewa hapo
 
Kasema ilikuwa ngumu kufanya kazi na Magufuli..Was this necessary?
Mimi na wewe hatupo kwenye position ya kulitolea majibu hilo swali.
Yeye (SSH) ndiye anaweza kulijibia. Ila kwa sababu alilisema, hiyo inaashiria kwamba ilikua ni muhimu kufanya hivyo.
 
U afiki mtupu. Walioweka lock up walitoboa? Kwa taarifa yako kwenye handling ya covid magufuli ni kinara duniani. Utake usitake kwa webye akili wanatambua kwamba dunia nzima inatumia method ya magufuli kwasasa with some few modifications

Una mtaarifu nani. Jifunze kujitegemea
 
Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.
Sasa wewe tukuchukulie vipi. Samia ni roboti lako, ambalo kwa bahati mbaya umeli-program vibaya? Unasema "unauhakika Samia hakudhamiria kusema hivyo...", wewe ndiye unayeshikilia dhamira yake?
 
Nyerere alikuwa na uwezo wa kujibu maswali ya waandishi wa kizungu mpaka wanaogopa kumuuliza tena, ni swala Ia IQ tu.
Okay siwezi kubisha maana sijui behind the scenes Nyerere alikuwa akijiandaa au la

Ila Nyerere alikuwa na umahiri wake na mapungufu yake, Samia nae ana umahiri wake na mapungufu yake

Pale kwenye mapungufu ndio tunashauri namna ya kurekebisha

Nyerere alikua ni kibibi cha kizungu ubavuni, si kama alikua genius kiasi hiko. Mleta mada yupo sahihi, unapokua na wasaidizi wabovu lazima utakua unavurunda vurunda mara kwa mara.
 
Mbona kama kajibu hivyo amejibu safi sana, nyinyi wabongo mushazoea kusema uongo na kupambia pambia mabosi wenu na kuwatukuza viongozi muda wote hata wakienda mchomo, siku zile Corona imeshika muliwalazimisha watu nchi nzima Corona isiitwe Corona eti iite ugonjwa wa kuambukiza., mukijaribu kuifananisha corona na magonjwa ya kawaida ili ionekane Corona sio tishio kwa maisha ya watu, wakati watu wakiendelea kupoteza maisha kwa hiyohiyo corona.

Samia nampongeza huyu mama anatabia ya kusema ukweli, na sasa anaonyesha waziwazi kwamba mwendazake alikuwa anakosea sana kwenye uongozi wake lakini kipindi kile mazingira yalikuwa hayamruhusu kumchalenge kutoka na hofu ya woga ambayo mkuu aliijenga.
Stupid
 
tunasema kulikuwa na hofu ya woga., elewa hapo
Kama unasema kulikuwa na hofu ya woga basi hufai kuwa kiongozi. Kiongozi unapaswa usimamie unachokiamini na si kuyumba, migogoro ya kimtazamo mara zote huzaa better solution.
 
ndio utuambie alitakiwa aseme vipi ?
angesema wakati ule tulidhani tatizo la Corona dogo nchinin kwetu au halipo kutokana na kipindi kile elimu kuhusu huo ugonjwa ilikuwa ndogo kwetu lakini baadaye tukaja kugundua kuwa tatizo ni kubwa ndio tukaanza kuchukua hatua stahiki hadi leo
 
Nadhani katika suala la COVID-19 Magufuli alifanya vizuri, kiuhalisia hofu ilikuwa kubwa kuliko gonjwa lenyewe, mfano hadi mwaka huu April 2022, Tanzania Ina wagonjwa 33,800 wa COVID 19, na vifo takribani 700, katika nchi yenye population of 63M, jamani idadi ya wagonjwa na vifo ni kidogo sana kulinganisha na nchi ambazo zilitumia njia tofauti na Ile aliyotumia Magufuli, Rais anafanya maamuzi kulingana na takwimu za watalaamu, hali halisi ya ugonjwa nchini, na nchi jirani , Bara la Africa na mataifa mengine, kama wewe ni Rais wa nchi Kwa takwimu hizi je ungeweza ku apply lockdown?

Tuongee ukweli tu bila kuwa na mihemko ya so called tuliumizwa or alikuwa dictator, kama Samia hakubaliani na njia iliyotumika na kuwa vusha watanzania walio wengi atueleze Kwa nini sasa hivi haweki lockdown Tanzania? Mbona hata toka aingie madarakani hajafikisha hata 5% ya chanjo Kwa watanzania? 98% ya watanzania hawavai barakoa na watu wanaishi , binafsi sioni tatizo la mbinu alizotumia Magufuli kututoa katika janga hili, kama watu wangekufa hata 10,000 tungesema serikali haikuchua tahadhari na iwajibike, lakini hakuna.


Siku zote Waafrica sisi tulikuwa affected by colonial minds , hatujikubali hata kama tunafanya vitu Kwa ufasaha mpaka hapo western wakisema hili jambo ni sahihi au la, itatuchukua muda sana kuendelea Africa hadi tujitoe kwenye hizo minds za kufanya jambo tukitegemea tupate approval kutoka katika mataifa mengine, huo ni utumwa mkubwa sana wa kifikra ambao tumerithi.

Hivi inawezekana vipi mtu ana kulecture how to control COVID wakati yeye ana vifo million 5 wakati wewe una vifo 10,000? , does it make sense?
 
Mahojiano ya jana ya Rais Samia na Gazeti la New York Times alinukuliwa akisema alipata wakati mgumu kufanya kazi na Hayati Magufuli kutokana na msimamo wa Magufuli juu ya Covid-19.

Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.

Kwa wanaoangalia mahojiano ya viongozi na waandishi wa habari wa nchi za 'mbele' wanajua jinsi waandishi hao wanavyokuwa aggressive, mnakumbuka Tundu Lissu mwenyewe alivyobanwa na mwandishi wa BBC hadi kujikuta ametamka atawapa mashoga haki zao...! Baadae akaja kukana hakumaanisha hivyo, ila sikumlaumu maana unabanwa kwelikweli.

Sasa kwa mtu kama Rais ambaye ana wasaidizi wengi smart walitakiwa ku-anticipate maswali ambayo angeulizwa Rais, na Rais angekua namna ya kuyajibu kabla, kuna maswali mengine unaya-dodge tu badala ya kutoa majibu direct ambayo yataleta utata, ndivyo wanasiasa hufanya.

Wasimuache kama anaenda kuhojiwa TBC.

Nadhani hili halitajirudia tena.
Huyu mama bila kujua anajenga uhasama mkubwa sana kwa wasukuma. Akumbuke wasukuma wana mikoa mitano. Lakini pia wametakaa kila mkoa wa jamhuri ya muungano wa Tanzania uchaguzi 2025 utakuwa ni uchaguzi mgumu sana.
 
Huyu mama bila kujua anajenga uhasama mkubwa sana kwa wasukuma. Akumbuke wasukuma wana mikoa mitano. Lakini pia wametakaa kila mkoa wa jamhuri ya muungano wa Tanzania uchaguzi 2025 utakuwa ni uchaguzi mgumu sana.
Sio Wasukuma wote wanaokubalina na Magufuli
 
Okay siwezi kubisha maana sijui behind the scenes Nyerere alikuwa akijiandaa au la

Ila Nyerere alikuwa na umahiri wake na mapungufu yake, Samia nae ana umahiri wake na mapungufu yake

Pale kwenye mapungufu ndio tunashauri namna ya kurekebisha
Funza ana upeo mkubwa wa kufikiri kuliko wewe. Yeye amesema kilichokuwa kinatokea, wewe unataka washauri wamshauri nini? Idiot at is highest form!
 
Usimumunye maneno kwa kuwasingizia wasaidizi wake, wewe jua tu Upeo wa mama ni mdogo sana, hakuandaliwa na hakujiandaa kuwa rais, alijikuta tu ni rais. Hawezi kitu, labda baada ya muda huenda akakuwa, tena baada ya kupigwa interviews za kutosha.

Wewe ulishaona wapi kirikuu ikiivuta scania iliyokwama kwenye matope? Haiwezikani.
 
Back
Top Bottom