Rais Samia aongea na Wazee wa Dar: Aahidi kutojali vyama katika teuzi zake. Serikali kutunza Haki, Demokrasia, Uhuru wa Habari

Rais Samia aongea na Wazee wa Dar: Aahidi kutojali vyama katika teuzi zake. Serikali kutunza Haki, Demokrasia, Uhuru wa Habari

Nimeamua kukutana na wazee mwanzoni kabisa mwa uongozi wangu, kwa kuwa wazee ni dawa na mna maarifa mengi. Tuje tuwasikilize kisha nyinyi na sisi kwa pamoja tupate mawazo mazuri"
 
Nimeamua kuongea na wazee wa Dar es Salaam, kwa sababu wazee wa Dar es Salaam wapo wa kutoka mikoa tofauti tofauti nchini, hivyo kuongea na nyinyi hapa ni kama naongea na wazee wa sehemu zote nchini"
 
Hivi mkutano wa Rais na wazee Hawa huna Ina faida gani? Tulishuhudia mikutano ya Aina hii enzi za Kikwete lakini awamu hiyo tulishuhudia Dar akisheheni Panyaroad, vibaka na ujambazi wa mchana kweupe. Naona mama anafuata style ya JK. Mkutano huo hauna tija.

Kwa nini wazee wa Da'slam tuu? Kwani Tanga au Dom Hakuna wazee? Mshaurini raisi akutane na vijana pia, nasi tumueleze yakwetu.
 
Statistics za serikali sizielewi.

Wazee 2M.

Population 60M

Tax payers 3M

Dependants 55M

Hii nchi haiwezi kwenda mbali.
Ndio mambo yetu wabongo hayo, hata hatueleweki ndio maana mtu mzima miaka 30 unakuta ana baba mdogo ana miaka 6
 
Lakini pia naongea na wazee kama ilivyo desturi yetu tangu tupate uhuru kwa Marais kuongea na wazee, hususan wakiwa na jambo, lakini mimi leo naongea na wazee sina jambo lolote, ila nimeamua kuongea nanyi"
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili Ukumbi wa Mlimani City kuongea na Wazee wa Dar es Salaam

Tunakuletea updates hapa

Mwenyekiti wa Wazee wa Dar, Salum Matimbwa
Tumepata kadi za msamaha wa Bima, lakini Wazee hatupati baadhi ya vipimo na Dawa tukifika Hospitalini

Tunaomba Rais Samia tunapokuwa Hospitalini, tupate vipimo na dawa zote kadri ya Magonjwa yanayotusibu

Tunakupongeza kwa kusimamia Sheria na Utawala bora. Tunaomba juhudi ziendelee ili kushughulikia kero za Wananchi

Vyombo vya Ulinzi na Usalama vifanye kazi kwa Sheria, Kanuni na Utaratibu waliojiwekea. Inapobidi Wananchi washirikishwe ili kuondoa manung'uniko

Wazee tunaomba Vyombo vyote vya Usafiri wa Umma vitenge viti maalum vya kukaa wazee

Pia, vihimizwe kuhakikisha vinawabeba wajukuu zetu ambao ni Wanafunzi wanapokwenda na kurudi shuleni

Kuna uwakilishi wa makundi mbalimbali #Bungeni lakini Wazee hatuna uwakilishi

Hivyo tunaomba na sisi ikikupendeza Rais, tupewe nafasi hiyo ili tupate Watu wa kutusemea matatizo yetu kwenye Vyombo vya Mamlaka

Waziri wa Afya - Dkt. Dorothy Gwajima
Wazee wanazidi kuongezeka. Mwaka 2012 kulikuwa na Wazee milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 na hivi sasa wameshafika milioni 2.52.

Mauaji ya wazee yamepungua kutoka 577 mwaka 2014 hadi wazee 34 mwezi Desemba mwaka 2020.

Wazee badala ya kwenda kutoa nasaha wao wanaenda kuomba bima tu ?
 
"Mbali ya sera, tunakwenda kutunga sheria lakini pia ilani yetu ya
ccm imetuelekeza kuhusu matibabu ya wazee, hivyo sina mahali pa kulikimbia
 
Nimeona watoa hotuba baadhi Yao wakifanya reference ya CCM na si vyama vyote vya siasa kwa ujumla. Rais ni wa Watanzania, atakayoyahutubia yanahusu watanzania wote na siasa za nchi zina ubia Kati ya vyama vya upinzani na chama tawala. Hilo hakipendezi kwa mshikamano wa Taifa na uungwaji mkono wa serikali ya awamu ya sita.
Washereheshai mmefanya kosa kubwa, lirekebishe hilo next time.
Vyama vingine vimejaa wakora wabobezi tu
 
"Timu niliyoiunda kunishauri kuhusu ugonjwa wa COVID-19 na iko mbioni kunikabidhi ripoti. Yale yote ambayo yanawafanya wazee wetu kuwa katika kundi la hatari kuambikizwa ugonjwa wa COVID-19 tutakwenda kuyashughulikia
 
Mimi ni mzee tayari, na hivi karibuni nitajiunga huko. Sasa, nisipoandaa mazingira mazuri nami nitaingia huko itakuwaje ni lazima tuwaandalie mazingira mazuri wazee "
 
TASAF ipo ukingoni ila serikali kuja na mradi mwingine kama TASAF kuhudumia wazee, kwa sasa wote wenye sifa tutahakikisha wanapata huduma
 
'Suala la kuwawezesha wazee kiuchumi, nakubaliana na nyie kabisa, kama alivyosema waziri tunatumia mfuko wa TASAF kuwawezesha wazee, na kuanzia mwaka huu sasa tunakwenda kwenye wilaya zote na sio kwa kuchagua'
 
"Kwa hali ilivyo sasa, na uwezo wa uchumi wetu ulivyo, uchumi wetu umeshuka kutoka asilimia karibu 7 hadi asilimia 4. 67 na hii ni kutokana na athari za janga la corona, niwaeleze wazee wetu kuwa hatutaongeza pensheni lakini mvumilie tutaongeza hapo baadae"
 
La uchumi kwa Wazee wetu nisiwe muongo, hali Hii ya janga la Corona imeathiri sana uchumi, hata kwa wafanyakazi vivyo hivyo niwaombe wazee wangu mtustahimilie.
 
Back
Top Bottom