Rais Samia apokea Taarifa ya Ukaguzi Maalum BoT, CAG abaini uwepo wa malipo kufanywa nje ya bajeti

Mpango ni Makamu hivyo hakuna jipya, acha watu waendelee kupiga pesa
Kwani katiba ya Tanzania inampa makamu wa rais kinga ya kutoshtakiwa endapo ataliingizia taifa hasara?
 

 
Maaamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tumeanza kumkumbuka baba Petrol hainunuliki.
Mwenzio kuanzia leo gari napaki, nitalitumia panapo na umuhimu mkubwa tu. Nitatembea, atakae thubutu kuniuliza namwambia naogopa kitambi.
 
Una ndoto za alinacha haaa haaa nyani, ngedere, sokwe wakae kujadili ujenzi wa nyumba.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hela zimetoka hazina kwenda tanroads na TPA kinyume cha utaratibu. Zilikuwa pesa ngapi? Bila shaka Mamia ya Mabilioni ya pesa tunazokamuliwa kodi.

Kinyume cha utaratibu ni kumaanisha pesa hizo zilikwenda kuishia mikononi mwa watu wasio husika. Flow hiyo haiwezekani bila ya angalau watu hawa kushiriki kwenye uhalifu huo kikamilifu:

Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gavana Benki kuu, Wakurugenzi wakuu TPA na Tanroads.

Tunayo haki ya kujua zilikuwa pesa ngapi na ziliishia wapi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Najiuliza tu, haya mambo mwisho wake ni lini,

Ni vyema kama hatuna wasimamizi na wenye uchungu na nchi yetu, basi tuwe tunafanya uchaguzi wa uraisi kila siku ili angalau kila Mtanzania afikie hiyo ngazi, ili kila mmoja ajichotee
Ukiambiwa kuna uhitaji wa kuwepo katiba mpya unajifanya haina umuimu alafu unakuja kulalamika hapa.unalalamika nini sasa.
 
Mkuu nitofautiane kidogo na we we. Katiba mpya haiwezi ikaleta mwarobaini wa ufisadi nchi hii, zaidi sana italeta mabadiriko katika mifumo ya kiuongozi.
Madaraka yatashikwa na watu walewale wenye njaa.
Nionavyo Mimi shida kubwa inaanzia chini kabisa ktk ngazi ya familia ambako ndiko hasa hulka, utashi, maadili, nidhamu nk ndiko vinapojengwa. Neno maadili mema kwa sasa limekuwa ni kitendawili kwa jamii zetu ambapo kila mmoja amekuwa mchumia tumbo. Unaweza kushangaa hata hiyo katiba mpya ikipatikana inakuwa ni njia tu ya kuwaweka wenye njaa madarakani.
 
Ni lini hivyo vyama vimeongoza ili tuvihukumu kua haviwezi.hoja ya vyama pinzani kuongoza sio kwasababu ni visafi au havina mapungufu bali ni ili kuleta ushindani na uwajibikaji ndani ya nchi.kukiwa na vyama vinavyopokezana uongozi lazima maendeleo yaje kwasababu kunakua na ushindani na wananchi ndio watakaoamua chama gani kiongoze.Na hoja ya katiba ata nchi ya chama kimoja lazima iwe na katiba kwahiyo hoja yako yakuzungumzia upinzani kua hoja yao inajali kuchukua madaraka ni hoja mfu sana na inatolewa na mtu mwenye uelewa duni wa mamlaka na wajibu wa katiba ndani ya nchi.
 
Tatizo mama alishampa mmoja wa watuhumiwa madaraka makubwa ambayo imekuwa mtihani mkubwa kwake kufanya maamuzi magumu dhidi ya muhusika. anyway tuende hivyohivyo
Unafikiri hata asingekiwa amempa majukumu hayo je angeweza kuongea BIG NO CCM HAWANA JIPYA MKUU PIGA KAZ


OVER
 
As expected. Isingewezekana kabisa kumuimplicate Makamu waRais awa sasa ambaye ni pick ya Samia ambaye alikuwa Waziri huko mida ile. CCM ni ileile
Huoni hata kwenye ripoti ya kwanza iliyoonyesha madudu kila kona, ni Wizara ya Fedha na Ofisi ya Makamu wa Rais tu ndiyo zilipata hati safi. Sisi bado sana kwenye mambo ya accountability na transparency. Hovyo tu !!!

Hata ukitajwa umekwapua mamilioni hakuna lo lote utafanywa. Huoni akina Kigwangalla bado wanadunda mtaani na kutambia vijana wajiajiri. Ingekuwa wote wanaotajwa wanatupwa ndani na mali zao kutaifishwa hali pengine ingeanza kubadilika. Kwa sasa sioni hata faida ya kuwa na CAG
 
Kwanini unawaza kirahisi hivyo.kinakushinda nini kuwaza kua na kitu kizuri kitakachomfunga kengele kila mtu nchi hii,kwa usawa,haki na uwajibikaji.kuanzia ngazi ya jamii hadi taifa.Inawezekana sana labda tuamue kutokua serious.Tunavyozidi kuwaza kua haiwezekani ndivyo ambavyo tunaendelea kujitoa kwenye nafasi yakutafakari kwa mapana zaidi ya nini kifanyike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…