Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Rais Samia aruhusu vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara

Mikutano ya Hadhara ni Haki ya Vyama vya Siasa. Nimekuja kutoa ruhusa; nimetengua zuio la Mikutano ya Vyama vya Siasa. Ni haki kwa Vyama vya Siasa kuendesha...

✍️
 
Usiende huko ndugu yangu huko ni mbali Sana!

Tunajenga nyumba Moja hatugombanii fito!

"Rasimu ya warioba irudi mezani SASA ijadiliwe iwe Katiba mpya"

"Ili ajaye asiharibu tena KWA kuhatarisha umoja wa kitaifa tulioujenga kwa Miaka mingi!
 
Duh! We jamaa umeandika maneno matakatifu, nakuombea Mungu akupe nafasi ya juu kabisa, tusaidiane kuijenga nchi yetu kwa njia ya amani.

Amani ni moja ya tunu tulizoachiwa na wazee wetu! Omukama akubele
Huu ni wakati wa kuijenga Tanzania yetu ili isiparaganyike na kusambaratika huko mbeleni. Bila amani hakuna siasa wala furaha.
 
Tatizo langu ni moja tu, CHADEMA ni kama fisi, unaweza wapa kila aina ya wanachotaka, wasiridhike, na wakaleta fyoko fyoko tu, Mh. Rais wetu Mama Samia, sio rahisi hao CHADEMA kuwaridhisha, kikubwa ww tenda haki, waambie kabisa, kwenye mikutano ya hadhara wakileta vurugu unawagonga rungu, wafuate utaratibu..

Kuhusu Katiba Mpya, hongera sana Mh. Rais, sitii neno, safii kabisa umesema yote.
 
Baada ya kuona watu wamejipanga kisawa sawa kuanza mikutano ya hadhara iwe kwa heri au kwa shari, hatimaye ameamua kukwepa fedheha ya kuruhusu mikutano hiyo kwa lazima.

Mpuuzi tu; kwenu hakunaga jema!!
 
Bado upinzan hawana nguv ya kufanya mikutano kwa kheri na shari uwezo huo haupo wala hajatishika, labda tu malkia wa Anga kaamua kujisafisha huko nje ya mipaka ili apate mialiko mingi maana anapenda safari ila siyo kwa kutishika
 
CCM janja janja Sana ,walishajua 2023 vyama vya siasa vinavyojitambua vingefanya mikutano bila kujali outcome , Ili Hali ni kwa Mjibu wa katiba, so wameovertake Ili kupata credit tu,
No i don't think so, ni kwa vile kiongozi alie madarakani ni mwenye mtazamo tofauti na alietangulia.

Swala la kuanza kufanya mikutano na maandamano mbali mbali halikuanza kupangwa leo. Wengi walijaribu lkn walizuiwa kufanya hiyo mikutano hata ile ya ndani, na wengine walifunguliwa kesi za kufanya mikutano bila kibali bila wapinzani wenzao waliopo nje kufanya chochote.

So kwa sasa ni kushukuru tu kutokana na aina ya kiongozi tulie nae, bila maamuzi yake hakuna ambae angefanya mkutano hata wewe mwenyewe rohoni unalijua hilo mkuu.
 
Kwa nguvu ya kikatiba aliyo nayo Rais wa Tanzania hakuna wa kumtisha. Kitu pekee ambacho kingeweza kumtisha rais ni CCM lakini wakongwe walishashtuka na kuamua rais ndo pia awe mwenyekiti wa Chama. Kwahiyo kwa kofia hizo mbili kama rais na mwenyekiti wa chama basi itoshe kusema Rais wa Tanzania anazo nguvu kubwa mno na hakuna wa kumtingisha.
 
Nimepitia comments nikabakia nacheka kimoyomoyo nikajiuliza hivi Watanzania huwa wanataka nini?

Hili jambo si mlikuwa mnalipigania limefunguliwa kwanini msifurahie ushindi?
 
Binadamu ukimtia kidole atalalamika na ukimuacha pia atalalamika
 
Back
Top Bottom