Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,903
- 1,360
Wakati mwingine ukimya ni silaha nzuri ila ukimya huo uambatane na kutatua kero zinazosemwa.Unaposema watu hawana cha kuzungumza wakati wakizungumza badala ya kuwajibu unadai umeziba masikio, unaonesha usivyojielewa.
Kutumia silaha ya kunyamaza badala ya kuwajibu kunaonesha usivyojitambua, usiyejua wajibu wako kwa wale unaowaongoza, umejiachia tu nature ikuongoze, halafu ajabu unajiona mshindi!.
Hata anaposema "anatukanwa" hicho ni kisingizio tu cha kukwepa kujibu hoja, na maswali anayoulizwa.
Nimekuja kugundua kuwa ukiwa kiongozi wa nchi yenye mfumo wa vyama vingi vilivyo huru, ni rahisi sana kuendelea kutawala maana matatizo yote wanakwambia, wewe kazi yako ni kuyatatua halafu ukifika uchaguzi wanakosa hoja - unaendelea kutawala. Ndiyo maana kuna msemo wa hekima kuwa upinzani ni kioo cha watawala