Ni aibu kwa CHADEMA ambayo ilitaka kutumia maafa haya kufanyia siasa zao chafu.kwa hakika CHADEMA ni li chama la hovyo sana .ndio maana linaendelea kupuuzwa na watanzania kila uchwao. Watu wapo kwenye majonzi halafu ninyi mnaleta siasa zenu uchwara.
Wewe Lucas Mwashambwa ulitaka CHADEMA wapeleke misaada. Haya sasa wamepeleka na wamezuiwa. CCM wamejimilikisha mpaka maafa. Tukisema wao ndo chanzo cha maafa wasikatae.

Miongoni mwa waliopatwa na maafa wamo wanachama wa vyama tofauti. Unamzuiaje kiongozi wa Chama kwenda kuona Watanzania wenzake?

Hapo wanataka wakiitisha kimkutano waseme ni CCM pekee ilikuja kuwaona.
 
Sasa picha zipo wapi?

Weka picha tuone hiyena hiyena!

Raha ya shughuli hekaheka
 
Walikufa watu 69 tu??? Kwa haya maelezo inaonekana jambo lilikuwa zito sana
 
Wataalamu waelezea udongo kunyonya maji mengi katika mlima Hanang

14 October 2022​

KIFAHAMU CHANZO CHA MAJI CHENYE MITO NANE NDANI YA MLIMA HANANG NA MSAADA WAKE KWA WANANCHI

Mhifadhi wa hifadhi ya Mlima Hanang yenye utajiri wa maji ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani na katika mashamba makubwa ya ngano.

View: https://m.youtube.com/watch?v=kXIktyk8JUUMaji yanayopenya ktk miamba (Underground water system) na kutiririsha maji mengi kupitia chemchemi za maji kujitokeza ktk miamba na kufanya mito ya maji kadhaa kutiririka kutoka hifadhi ya msitu wa mlima Hanang nchini Tanzania.

Mlima Hanang uhifadhi maji kwa misimu mingi hata mvua zisiponyesha kwa miaka kadhaa anabainisha mhifadhi wa msitu wa mlima Hanang.

Hivyo mlima Hanang ni kama dodoki yaani sponji 🧽 kukusanya maji mengi hivyo miamba na ardhi ya mlima kuwa na unyevunyevu petevu kwa kuelemewa na maji, ndiyo maana kuna chemuchemi nyingi kutoka miambani na pia katika miteremko ya mlima huo wa nne kwa urefu nchini Tanzania ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…