MAMBO YALIYOFANYWA NA SERIKALI YA RAIS SAMIA, KATIKA KUKABILIANA NA MAAFA YA HANANG
● Serikali Imewaokoa Watanzania 117 na waliopewa huduma bure za matibabu kupitia gharama iliyobebwa na Rais Samia.
● Serikali imegharamia mazishi ya Watanzania 79 waliofariki kwenye maafa ya Hanang.
● Serikali inaendelea na zoezi la kutafuta miili ya watanzania wengine walioathirika na maafa hayo.
● Serikali imeanzisha makazi ya muda kwa wakazi 440 ambao walipoteza makazi yao ya kudumu.
● Serikali inatoa huduma za Malazi, Afya, Chakula, usafi pamoja na huduma za kisaikolojia.
● Serikali imeendelea kugawa misaada mbalimbali kutoka kwa Sekta mbalimbali.
● Serikali inaendelea kusikiliza na kutatua changamoto za mtu mmoja mmoja walioathirika na maafa.
● Serikali imetoa Askari 1200 wanaohusika kwenye zoezi la uokoaji wa maafa.
● Setikali imeandaa chakula kinachotosha kwa siku 30 kwa ajili ya wananchi.
● Serikali inapambana kurejesha miundombinu inayotakiwa kwenye mitaa na vijiji na huduma za biashara zimeanza kurejea.
● Serikali imerejesha tena huduma za umeme Hanang Transfoma 79 zimerejeshwa na Nguzo 600 zimesimamishwa tena.
● Serikali imeanza kuchimba visima 10 vya maji, pia imeleta matanki ya maji yenye lita za maji 5000.
● Serikali imetoa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi Milioni 300.