Pre GE2025 Rais Samia atenga siku moja kila mwezi kusikiliza kero za watanzania

Pre GE2025 Rais Samia atenga siku moja kila mwezi kusikiliza kero za watanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja"

Kwa hiyo siku nyingine zote zilizobaki za Mwezi atakua anafanya shughuli gani!?
Unataka kusema kwa sasa hana kazi anasubiri atenge hiyo siku moja ndo aanze kazi?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja

"Amefanya hivyo kwa sababu kuu tatu moja ni kuwafanya viongozi wengine wawe na tabia ya kusikiliza kero za Wananchi, sababu ya pili ni kumuenzi Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na jambo la tatu ni kutoa nafasi ya kutumia cheo na nyadhifa za uongozi kuwasaidia Wananchi"

View attachment 2925211
Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na mafunzo wa CCM​
Chawa watakuwa wanapangwa kuuliza maswali, pia atakuwa anasikiliza akiwa wapi?
 
sasa kama nchi imejaa machawa wateule wa raisi hawawezi kazi zao na raisi mwenyewe anaona siku 12 kwa mwaka ataweza sikiliza kero za wananchi basi aendelee ila akae akijua kama anafanya hizo shughuli hakuna haja ya kuwalipa viongozi aliowateua kumsaidia mbali na hapo ni maigizo tu kama ya ndugu mwenezi kupita sehemu zenye wateule na kuvumbua makosa kama vile hakuna ufuatiliaji
 
Na ametenga siku ngapi kwa ajili ya kuzishughulikia?🐒
 
SULTAN TAMBA FILMS.

Huyu aliyekuwa hataki kusikiliza watu kwenye ziara zake ndo aanze kusikiliza leo!

Sawa, ngoja tusubiri huo utaratibu utakuwaje na kama itaishia kwenye kusikiliza tu au na kutatua.

BTW:Toka 2019 wastaafu wanasotea mapunjo ya pensions zao baada ya waajiri (DEDs) kutowasilisha michango ya wanachama hao kikamilifu.
 
Ardhi,
Plot yangu nambari 471, block A, iliyopo mbezi, goig, imeporwa na kujengwa bonge la nyumba, huyu ndugu aliyepora eneo langu ambaye jina lake linaweza KLO, naomba anirudishie tafadhali sana sana sana. Wanakwiba ardhi wazi wazi bila woga kabisa!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja

"Amefanya hivyo kwa sababu kuu tatu moja ni kuwafanya viongozi wengine wawe na tabia ya kusikiliza kero za Wananchi, sababu ya pili ni kumuenzi Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na jambo la tatu ni kutoa nafasi ya kutumia cheo na nyadhifa za uongozi kuwasaidia Wananchi"

View attachment 2925211
Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na mafunzo wa CCM​
Tunataka apunguze hizo mafao ya wenyewe kwa wenyewe kwanza.
Punguza Safari za nje na jopo lako.
Kuna walioko chini yako wanakamua sana pesa za miradi na kwingineko kila kukicha na unajua unakaa kimya.
Wawajibishe wanaokwamisha.
Wananchi Kuna maeneo wanaishi kwa shida sana na watoto wao kwenda shule umbali sana kwa mguu na Hawaili mlo mchana.
Barabara zinazosimamiwa na TARURA pamoja na kupewa pesa ziko Hoi!

Mama Kuna shida mahali wako watakaopanga kutoa majibu za hovyo.

Fanya uende mwenyewe maeneo fulani kwa kushtukiza na hasa mkoani au wilayani achana na mjini hutapata jawabu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja

"Amefanya hivyo kwa sababu kuu tatu moja ni kuwafanya viongozi wengine wawe na tabia ya kusikiliza kero za Wananchi, sababu ya pili ni kumuenzi Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na jambo la tatu ni kutoa nafasi ya kutumia cheo na nyadhifa za uongozi kuwasaidia Wananchi"

View attachment 2925211
Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na mafunzo wa CCM​
Hilo la kwenda Dar Dod na Zanz. Ni utapeli mtupu.
Hapo Lumumba Kuna nini zaidi ya machawa wake.

Hebu mwambie aende hapo Chalinze au Kilosa akasikilize kero kama hakuja kulilia ofisini!
Tusidanganyane.
Tutapiga kelele!!
 
Ila Rais katudharau Sana. Kaona uchaguzi unakaribia kaamua kutudanganya. Ok
 
Atoe namba kabisa siku hiyo tutume meseji na azijibu na wengine wapige simu apokee tumuambie moja na mbili
 
Mbona shida za wananchi zinajulikana ziko wazi kabisa. Tengenezeni mifumo imara, inueni uchumi wa watu
 
Kila mwisho wa mwezi awe anatoa taarifa kwa njia ya hotuba kwa wananchi kupitia studio iliyopo Ikulu.
Lengo iwe kuzungumzia mambo muhimu kama vile jinsi gani Serikali inadhibiti mfumuko wa bei(Suala hili hajawahi kuonyesha kama ana mkakati wa kudhibiti).
Akemee kupandishwa kiholela kwa bei ya mafuta na bidhaa zingine.

Wananchi wanataka unafuu wa maisha na haki , azungumze na viongozi waliochini yake kwanza kabla ya kuanza kusikiliza kero za wananchi.
 
Back
Top Bottom