Rais Samia atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Raphael Chegeni

Siku chache baada ya Wakuu wa Mikoa wapya 9 kuteuliwa, Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni

Amemteua Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, na ataapishwa na Wateule wengine kesho (Agosti 01, 2022)

Kabla ya uteuzi wa Rais, Meja Jenerali Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP)

View attachment 2310242

View attachment 2310215
Bado TIss na uhamiaji sasa
 
Ubalozi na ukuu wa mkoa,aliyepata shavu ni mkuu wa mkoa ndio representative wa raisi,balozi anaripoti kwa katibu mkuu wizara ya mambo ya nje

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums

Ubalozi na ukuu wa mkoa,aliyepata shavu ni mkuu wa mkoa ndio representative wa raisi,balozi anaripoti kwa katibu mkuu wizara ya mambo ya nje

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Uncle Fogo iko hivi kwa tafsiri ya huku vijiweni ubalozi maana yake una nguvu za kiushawishi na Boss moja hakuihitaji kwenye siasa za ndani ( neutralisation of threats) URc maana yake anakutaka ila katika mamlaka madogo.

Kwa Lugha nyingine Sirro anaushawishi polisi kuliko huyu bwana kwenye jeshi la magereza ila kwa navyomjua hata hiyo nafasi hata hudumu sana yeye mwenyewe anajua kadharauliwa.
 
Jamani huyu mzee kapata kazi ya mkataba wa miaka 5 nchi moja wapo bara la Asia toka shirika la UN anaenda kusimamia maswala ya fedha japo siyo ndo atakuwa mkuu,

Jaribu kutafakari unaweza acha kazi ambayo ushasaini mkataba kisa kazi ya kuteuliwa ambayo hujui hatma yako

Mzee alimuandikia mama barua na maelezo ya kutosha mama kamuelewa kateua mwingine

Kesho mniite mbwa kama mama asiposema ameombwa
 
Chegeni huyu ninayemjua kaomba mwenyewe kutenguliwa, pesa anazo si za nawazo ..Isamilo Hotel ya jijini Mwanza, Majumba ya kutosha Dar, Dodoma, Mwanza nk...watoto wake wote wapo kwenye Financial institutions kubwa Dubai, Austraria na USA, mke wake.....niishie hapa nisije jichoresha Bure nyuma ya I'd feki! Kifupi jamaa pesa ipo, kwenye siasa Kawa mbuge wa Busega kuanzia kwa Mkapa hadi awamu ya tano alipoondelewa na yule dk wa mifugo....Kisha kuingia tena na baadae Jiwe akamuweka pembeni pamoja na kuongoza kura za maoni!

Tengua ya Leo ngoja tusubiri ufafanuzi vinginevyo rais wetu kazungukwa na mafisi kundi la watu wa ovyo kuwahi kutokea!
Asingekua anatokea kwenye media analialia kuenguliwa ubunge
 
Magereza sio fani yake angemrudisha tu Jeshini akatumikie taaluma yake, Mara hakina maajabu kama Ali Hapi alipamudu, mjeda wa nini sasa?
 
Mmedangwa na nani amekua demoted ,kipesa cjui ila kicheo amepanda ,hapo sasa hivi anapigiwa saluti hadi na CDF .yeye ni sehemu ya rais wa nchi now

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Aiseee unajua majambo mzee wangu 🤣🤣🤣🤣
 
Chegeni huyu ninayemjua kaomba mwenyewe kutenguliwa, pesa anazo si za nawazo ..Isamilo Hotel ya jijini Mwanza, Majumba ya kutosha Dar, Dodoma, Mwanza nk...watoto wake wote wapo kwenye Financial institutions kubwa Dubai, Austraria na USA, mke wake.....niishie hapa nisije jichoresha Bure nyuma ya I'd feki! Kifupi jamaa pesa ipo, kwenye siasa Kawa mbuge wa Busega kuanzia kwa Mkapa hadi awamu ya tano alipoondelewa na yule dk wa mifugo....Kisha kuingia tena na baadae Jiwe akamuweka pembeni pamoja na kuongoza kura za maoni!

Tengua ya Leo ngoja tusubiri ufafanuzi vinginevyo rais wetu kazungukwa na mafisi kundi la watu wa ovyo kuwahi kutokea!
Acha uongo. Chegeni namjua vizr walipigana ngumi na DR. Kamani. Unadhani hayo yote uliyoyataja hakuwa nayo! Licha ya hao lakin mwaka 2020 aligombea Tena.
Acha kupotosha. Hii ni serikali ya kishikaji. Nani amesahau ya MATARAGIO pale kampuni ya Mafuta
 
Kupigana, kukimbua na masanduku ya kura ni jadi ya CCM...
Nikupe dodoso, unawafahamu wanasiasa wa kanda ya ziwa ambao hawakupiga magoti na kuimba mapambio awamu ya Magufuli.....? Chegeni ni mmoja wao, sababu unajua ni kwanini...?
Acha uongo. Chegeni namjua vizr walipigana ngumi na DR. Kamani. Unadhani hayo yote uliyoyataja hakuwa nayo! Licha ya hao lakin mwaka 2020 aligombea Tena.
Acha kupotosha. Hii ni serikali ya kishikaji. Nani amesahau ya MATARAGIO pale kampuni ya Mafuta
 
Jamani huyu mzee kapata kazi ya mkataba wa miaka 5 nchi moja wapo bara la Asia toka shirika la UN anaenda kusimamia maswala ya fedha japo siyo ndo atakuwa mkuu,

Jaribu kutafakari unaweza acha kazi ambayo ushasaini mkataba kisa kazi ya kuteuliwa ambayo hujui hatma yako

Mzee alimuandikia mama barua na maelezo ya kutosha mama kamuelewa kateua mwingine

Kesho mniite mbwa kama mama asiposema ameombwa
Tunahifadhi hii Risiti .
 
Back
Top Bottom