Rais Samia atoa TZS Bilioni 600 Ujenzi wa Hospitali ya Muhimbili mpya
Rais AMETOA B.600? amezipata wapi?
20220603_182451.jpg
 
Hongera zao

Ila najiulizaga,kwenye kujenga majengo wako faster ila kuweka
Huduma ya upatikanaji wa madawa,machine za kufanyia vipimo
Kuna suasua

Ova
Kipi kinaanza kati yao
 
KATIBU ITIKADI NA UENEZI CCM SHAKA HAMDU SHAKA AFANYA ZIARA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE, MUHIMBILI
View attachment 2279787
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo akiwa kwenye ziara hiyo amepata nafasi ya kupokea taarifa zinazohusu taasisi hizo.
View attachment 2279798
Aidha Shaka amepata nafasi ya kuzungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa wakipatiwa huduma mbalimbali.Pia katika ziara hiyo amezungumza na baadhi ya raia wa nchi mbalimbali za Afrika wakiwemo wa Rwanda,Burundi na Congo ambao wamekuja kupata huduma za matibabu ya afya.
View attachment 2279807
Shaka amefanya ziara hiyo leo mchana na lengo la ziara yake pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kwenda kumjulia hali mzazi wa Watoto mapacha waliotengenishwa Amina Amosi(18) Mkazi wa Simiyu aliyepo Hospitalini hapo.
View attachment 2279789
Amemtia moyo huku akitoa maelekezo kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii kutembelea mzazi huyo na kumueleza namna ambavyo Serikali itamsaidia malezi ya Watoto.
View attachment 2279808
Akiwa katika ziara hiyo Shaka amepokea taarifa ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba pamoja na uwekezaji katika miundombinu.

Aidha Shaka ameeleza mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya afya huku akizungumza mipango ya kuijenga Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo zaidi ya Sh.bilioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo ambao unakwenda kuandika historia nyingine katika sekta ya afya nchini.
View attachment 2279809
Hata hivyo amewapongeza watoa huduma katika taasisi hizo kutokana na huduma bora ambazo wanazitoa katika kuwahudumia Wananchi huku akieleza kwamba Kuna mambo makubwa na mazuri yamefanyika tofauti na baadhi ya watu wanavyozungumza.
View attachment 2279810
View attachment 2279811
=====

Huu ni utapeli wa kitoto, atoe 600b, wakati vituo na hospitali zote zilizojengwa nchini ndani ya 5yrs hazijafikia 500b? Na kuna watu wataamini huu utapeli.
 
Hongera zao

Ila najiulizaga,kwenye kujenga majengo wako faster ila kuweka
Huduma ya upatikanaji wa madawa,machine za kufanyia vipimo
Kuna suasua

Ova

CCM huwa wanajali wingi na sio ubora.
 
Hela ametoa wapi? Kwenye budget ya wizara ya afya ya 2022/2023 hii Pesa ya muhimbili imo?
 
Hao Muhimbili walisema IVF ingeanza Mwaka juzi mpaka leo hatujasikia kuanza.

Kwa matamko tu rahisi kusema vitendo sasa?!
 
Back
Top Bottom