Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Members, Kwa mujibu wa Gazeti la mwananchi Kamanda wa Takukuru Hamduni anasema watakapomuhitaji Paul Makonda watasema.

Hivi kwa mtu smart Unawezaje kuendelea kuwepo Nchini kwa matukio kama ya Makonda.

Maisha ya kuishi bila dhamana yatakuharibia familia na wewe mwenyewe, Una muda wa kujipanga na kukimbia, Sasa Unajadiliwa wewe kila kona ya nchi.

Mfalme hayupo tena, Nasema ondoka, Ondoka unasagiwa kunguni.

Tuhuma nyingi nzito hata kabla ya Ole Sabaya zilielekezwa kwa Paul Makonda na Kikosi kazi chake, Tena huyu alitembea na watu wenye sare kabisa bora ya Ole Sabaya,Makonda alipovamia Clouds media ili awashughulikie Shilawadu ilikuwa ni kama movie ya kivita.

Mali alizojipatia Bwana Makonda toka kwa matajiri kwa dhuluma zinajulikana, Ni Kheri akakimbia na kuanza upya maisha, Akikamatwa Mali hatazitumia tena.

Mtu smart angeanza kuuza Mali zake za dhuluma taratibu kabla ya kukamatwa.

Nina hakika hata akiendelea kubaki tayari amejawa hofu ambayo itamfanya aishi kama digidigi, Huyu alisema hakuna mtu anakula raha Tanzania kama yeye.
 
Mwaka wote huu Makonda aepuke media, akae kimya.
hiyo hulka hana.
anapenda shobo, anapenda kuzungumziwa na kusifiwa.

anapenda kupost picha zake, za mkewe na watoto wake kwenye ukurasa wake instagram. he can't keep it low key....hawezi kuji control kwenye hilo....nadhani bado haamini kuwa yeye sio tena miongoni mwa wateule wa rais. ushamba bado unamsumbua.
 
Tulien huu mchezo hautaki hasira
Usimshtue boya wewe
Tushazuia mipakan na airport zote hawez kwenda mahali popote
 
Sabaya akirudi uraiani hana maisha amini nakwambia hata mwaka hatoboi jela ni jambo jema kwake
 
Acha uongo. Msikilize Mama hapa chini

View attachment 1809459
"Chunga sana watu wasikuongee vibaya...." ukichukua hiyo kauli inakutosha kujua huyo kipenzi chako yuko kwenye fungu gani... Je mali alizojilimbikizia zinafanana na kipato chake? Je aliyowafanyia NASCO, GBP, Manji nk. Yalifaa? Je alivyovamia Clouds ilikuwa utumishi uliotukuka? Au hao watajwa hawana "watu" nyuma yao ambao wanamuongea vibaya "mungu" wa daslamu?
 
hahahhh waswahili wanasema yatima hadeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…