Rais Samia Awaandalia Yanga Hafla ya Kuwapongeza

Rais Samia Awaandalia Yanga Hafla ya Kuwapongeza

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Ameandaa hafla ya kuwapongeza Wananchi, Young Africans SC kwa hatua waliyofikia kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika ambapo klabu hiyo ilifika fainali na kufanikiwa kutunukiwa medali kama mshindi wa pili.

Hafla hiyo ya kuipongeza klabu ya Yanga itafanyika Juni 5, 2023 Ikulu, Dar es Salaam.

F4554658-57B5-43BD-BEAB-E6D96A5E1701.jpeg
 
Hawa Yanga si wanatakiwa waende huko Sumbawanga? Au serikali (na siyo TFF) imeamua ligi iendelee kusimama?
 
Kuna kipindi nilisikia kauli kuwa mkuu wa kaya kabla ya kuwaaga wanaye alikuwa hashauriki.

Sina hakika kama mama tuliyeachiwa ni vivyo hivyo au washauri ndio wamechagua kumpotosha!
 
Hivi hafla kama hizo zinaandaliwa kwa pesa binafsi au ya umma! Maana ni upotevu wa pesa bure wakati nchi yetu ina watu wanashida nyingi wengine wanashindwa hata kujilipia matibabu ya laki moja tu wanapoteza maisha lakini anatokea mtu mmoja kwa mapenzi yake binafsi anaamua kutapanya pesa ovyo ili kufurahisha vyura.
 
Sasa mbona hiyo bendera imepinduliwa?

Au wanaisoma wao na si watu walio mbele yao.
 
Back
Top Bottom