Rais Samia aweka rekodi ya Dunia. Tuna uwezo wa kuzalisha umeme hata mvua isiponyesha miaka 3. Lita bilioni 2 za maji bwawa la Nyerere zakusanywa

Hahahaha Aisee noma sana.haya Lucas
 
Acha habari za uzushi ndugu yangu mtanzania. Serikali ya CCM imekuwa na dhamira njema na utayari mkubwa sana wa kushughulika na kutatua changamoto za watanzania.
Tangu 1961 - 2025 matatizo ni yale yale mpaka leo.
 
Tangu 1961 - 2025 matatizo ni yale yale mpaka leo.
Kwani wewe kwa ufahamu wako unafikiria mwaka 1961 Watanzania tulikuwa wangapi na sasa tupo wangapi? Kama idadi ya watu inaongezeka. Unafikiri kero zenyewe zitakosekana vipi kuwepo na kuongezeka?
 
Habari yako, Lucas Hebel Mwashambwa,

Kwa kuzingatia hoja zako juu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ni muhimu pia kuzingatia maoni yanayopinga au kutoa mtazamo tofauti kuhusu mambo uliyoyasema. Kwa hiyo, nitabisha kwa hoja hasi kwa kuzingatia baadhi ya mambo ambayo yanaweza kutoa mtazamo tofauti kuhusu uongozi wake na mafanikio ya Taifa letu.
1.Uwekezaji wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na Uzalishaji wa Umeme Ingawa mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere umeendelea vizuri na kufikia asilimia 99.8, ni muhimu kujiuliza:

Je, uwekezaji huu ulifanywa kwa gharama gani kwa wananchi wa kawaida?

Uwekezaji wa mabilioni ya shilingi kwenye mradi huu umeweza kusababisha kupunguzwa kwa bajeti katika sekta nyingine muhimu kama elimu, afya, na miundombinu ya kijamii. Je, hii imeathiri wananchi wa kawaida?
1. Je, uzalishaji wa umeme umeleta faida kwa wananchi wote?

Ingawa umeme unazalishwa kwa wingi, bado kuna maeneo mengi ya vijijini ambayo hayajafikiwa na umeme wa taifa. Je, mafanikio haya yanawafikia wananchi wote, au yanakusudiwa kwa faida ya watu wachache na sekta ya viwanda?

2.Mvua na Ukame
Unasema kuwa hata kama mvua haitanyesha kwa miaka mitatu, Tanzania bado itakuwa na umeme wa kutosha. Hata hivyo, ukame hauna athari tu kwenye uzalishaji wa umeme bali pia kwenye kilimo, ufugaji, na maji ya kunywa. Je, serikali imejiandaa kwa kutosha kukabiliana na athari za ukame kwenye sekta hizi?

3. Uongozi wa Rais Samia na Uwajibikaji
Unamtaja Rais Samia kama kiongozi mwenye maono makubwa na uwezo wa kiakili. Hata hivyo, ni muhimu kujiuliza:
Je, uongozi wake umekuwa na uwajibikaji na uwazi kwa wananchi?

Kuna maswali juu ya uwazi katika mikataba ya uwekezaji, hasa katika sekta ya nishati na madini. Je, wananchi wamepewa taarifa kamili kuhusu mikataba hii?
Je, anaendesha serikali kwa misingi ya haki na usawa?

Kuna malalamiko kutoka kwa baadhi ya watanzania kwamba uongozi wake haujawa wa kuwajibika kwa wote, hasa wale walio katika maeneo ya vijijini na wale ambao hawana sauti katika jamii.

4.Kuhusu Ushindani wa Ndani ya CCM
Unasema kuwa Rais Samia hana haja ya kushindanishwa ndani ya chama chake kwa sababu ana uwezo mkubwa. Hata hivyo, demokrasia inahitaji uwiano wa nguvu na uwajibikaji. Kwa kumwachia kiongozi asiwe na mshindani, inaweza kusababisha uongozi usio na mizani na kukosa uwajibikaji. Je, hii ni njia sahihi ya kuendesha demokrasia?

5. Mafanikio ya Taifa na Hali ya Wananchi wa Kawaida
Ingawa unasisitiza mafanikio makubwa ya Taifa, ni muhimu kujiuliza:
Je, mafanikio haya yamebadilisha maisha ya wananchi wa kawaida?
Bei za bidhaa za kimsingi zimeendelea kupanda, na hali ya ufukara bado ni changamoto kubwa nchini. Je, mafanikio ya Taifa yamewafikia wananchi wa kawaida?
Je, kuna usawa katika usambazaji wa mafanikio haya?
Kuna dalili za kukosekana kwa usawa katika usambazaji wa mafanikio, hasa kati ya maeneo ya mijini na vijijini.

6.Kuhusu Uuzaji wa Umeme kwa Nchi Jirani
Unasema kuwa Tanzania ina mipango ya kuuza umeme kwa nchi jirani kama Kenya na Zambia. Hata hivyo, ni muhimu kujiuliza:

Je, wananchi wa Tanzania wamepata faida kamili ya rasilimali zao kabla ya kuuza kwa nchi jirani?

Kuna wasiwasi kwamba wakati umeme unauzwa nje, bado kuna maeneo mengi nchini ambayo hayajafikiwa na umeme wa taifa.

Hitimisho
Kwa kuzingatia hoja hizi hasi, ni wazi kuwa kuna maswali mengi ambayo yanahitaji majibu kuhusu uongozi wa Rais Samia na mafanikio ya Taifa letu. Ingawa kuna mafanikio makubwa yaliyopatikana, ni muhimu kuhakikisha kuwa mafanikio haya yanawafikia wananchi wote na kuwa na uwazi na uwajibikaji katika uongozi.

Kwa hiyo, hoja yako inaweza kushindwa kwa kuzingatia mambo haya hasi ambayo yanaweza kuleta mtazamo tofauti kuhusu uongozi wa Rais Samia na mafanikio ya Taifa letu.
 
Iyeeena iyeeenaa!!!! Samia Iyeeena, iyeeena iyeeena Samia nambari wani
 
Nimesoma andiko lako lote .ambapo majibu yako yapo mengine yapo katika andiko hili na mengine yapo katika maandiko yangu mengi ambayo nimekuwa nikiyaweka humu jukwaani mara kwa mara kuelezea mafanikio ya Rais Samia katika kila nyanja.
 
Inawezekana Nyumbani kwako huna umeme
 
Hapa nilipo wiki ya tatu umeme uliopo ni low voltage, hata friza hazigandishi wala kupooza
 
Naomba unipe haya majibu..., umeme una faida gani kama sio affordable ?

Aliyetangulia alisema wote waunganishwe kwa elfu 27 na Bwawa likiisha bei ishuke sasa hivi umeme kuunganishwa umepanda na tumeambiwa hata Bwawa likiisha umeme hautashuka...

Kuna pesa za kumwaga za Nishati Safi (Misaada) Lakini bado madalali wanahangaika kugawa mitungi bure ili wauze Gesi ambayo hatuna na inanunuliwa kutoka nje (eti wanataka wapunguze bei kwa kutumia Kodi zetu)

 

Wawaulize Zambia nini kiliikuta Kariba dam.....!?
 
Anaenyesha ni Samia au Mvua au Samia ndio Kaleta mvua?
 
Huu uzi tutautumia kama risiti mgao ukianza….pumbaaaaav
 
Hapa nilipo wiki ya tatu umeme uliopo ni low voltage, hata friza hazigandishi wala kupooza
Itakuwa wapo kwenye marekebisho. maana kipindi hiki kimekuwa na matengenezo mbalimbali ikiwepo ya kuboresha nguvu na kuimbwa wa umeme kwa baadhi ya njia kutegemeana na matumizi ya eneo husika na uwekezaji uliopo eneo hilo. Kwa hiyo usijali .uwe na subira mambo yatakaa sawa tu na utafurahi Mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…