Rais Samia aweka rekodi ya Dunia. Tuna uwezo wa kuzalisha umeme hata mvua isiponyesha miaka 3. Lita bilioni 2 za maji bwawa la Nyerere zakusanywa

Umeme wa maji sio RELIABLE, palitakiwa kuwa na sources zingine za Umeme, Lukas mkishatumiwa msg kwenye ma group yenu mkiambiwa msambaze basi hakuna kusoma hakuna kufanya nini hakuna kuchuja, unakuja unazibandika kama zilivyo sio ? Hydropower inapitwa hata na Umeme wa wind turbines... Hydropower ni kama Umeme wa one hivi kwa reliability, hapo bado mzazi wa Umeme utakuwepo, sababu kuna sehemu bado Umeme unakata nimeona kuna mdau huko juu kasema. Leo kwenye whatsapp group zenu wamewatumia habari gani na picha gani mzisambaze mkuu ?
 
Kwa sasa kuna matengenezo yanaendelea baadhi ya maeneo,ikiwa ni pamoja na ubadilishaji wa nguzo pamoja na kuongeza umeme. Ambapo hata taarifa hutolewa mapema. Lakini pia napenda kukwambia kuwa Tanzania tunatumia vyanzo mbalimbali vya umeme ikiwa ni pamoja na gas,jua na tunakwenda mbali zaidi kuanza kuzalisha Umeme kwa kutumia joto ardhi.

Jambo la kukukumbusha na kukufahamisha ni kuwa umeme unaotokana na maji ni 65% pekee .ambapo hizo zingine 35% ni kutoka vyanzo vingine mchanganyiko. Naamini umeielewa sasa.
 
Sayansi ya kuhifadhi maji natumaini inatuwezesha kuwa nayo kwa miaka hiyo mitatu.

Mungu ni mkubwa sana, anao uwezo wa kutupatia joto kali kwa miezi sita mfululizo majani yote yakakauka na mifugo ikaanza kufa huko porini.

Iwepo sayansi ya kisasa ya kutoyapoteza hayo maji.
 
Lengo la hilo bwawa ilikuwa ni kupata umeme wa bei rahisi sijui kama malengo hayo yamefimiwa, la pili hilo la kusema hata misimu mitatu hilo bwawa linaweza kuzalisha umeme si mtaalamu hapo lkn hilo jambo lisifanyiwe siasa ikawa kama pale Dodoma miaka Ile ooooh Dodoma Ina visima vya maji ya kutosha kugawa morogoro na singida na yenyewe bila kuteteleka lkn ilipotangazwa tunahamia Dodoma kilichofuata mabomba mengi yanatoa mijusi,kilichopo bei ishuke baada ya bwawa huo ndio msaada Kwa mwananchi na si kuwepo umeme ambao kununua ni shida
 
Hivi lilijengwa kwa Maamuzi ya Awamu ya 5 au ya 6. Na wadau wa ppp walikuwa wanataka umeme utoke wapi vile na sio huko rufiji
 
Huu ni wakati wa Tundu Antipas Lissu.
 
Ishia hapo hapoooo! Aiseee mbona mnapenda sanaa uchawa hivo, sifa kwa mama kidogo tu sifa kwa mama.
Sikiliza hizo pongezi anastahili MAGUFURI kwasababu yeye ndo aliyewasha gari hata mabeberu walipokua wanamchimba beat yeye ndo alikula msimamo. Huyu ameendeleza tu ni kama saidia fundi tu na alivo hivo angeweza kukataa wakati ndo huko huko anakoomba na mikopo. R I P
MAGUFURI Mungu aiweke nafsi yako mahali pema peponi.
 
Wivu tu ndio unakusimbua hapa. Si mlikuwa mnabetua Midomo yenu kuwa mama hatakamilisha mradi huo? Saizi mmeanza kuweweseka na kupiga mayowe.
Kauli za watu wasiokua na hoja Huwa wanakimbilia neno wivu utafikiri hii nchi ni Mali ya familia!
Jibu hoja nilizoandika!
Nyie nyie machawa ambao hamjitambui Ndio nlikua sceptical kama atamaliza. Acha ujinga
 
Zanzibar bei ni 27,000 lakini Hai/Boman'ombe ni 320,000+ hovyo kabisa
 
Mbona Magufuli hatajwi kqwenye hiyo rekodi?. Isingekuwa uthubutu wa Magufuli haya yote mnayoyasema yasingekuwapo. Msiwe wasauhulifu.
Hawa wakina mama wa CCM hawana akili wao wanasifia wapate pombe na nyama hata akija shetani watamsifia
 
Hivi we pimbi,Sasa hapa Samia anahusika vipi?bwawa kajenga Magu.na mvua kaleta Mungu.acha mambo yako ya kijinga na kichawachawa
 
Hivi we pimbi,Sasa hapa Samia anahusika vipi?bwawa kajenga Magu.na mvua kaleta Mungu.acha mambo yako ya kijinga na kichawachawa
Kalipwa hela ya bia tayari kashalewa anaandika upuuuz chai kabisa.
 
Muwe na SHUKRANI enyi vibaka. Hiyo ni kazi ya JPM mpongezeni
 
Kauli za watu wasiokua na hoja Huwa wanakimbilia neno wivu utafikiri hii nchi ni Mali ya familia!
Jibu hoja nilizoandika!
Nyie nyie machawa ambao hamjitambui Ndio nlikua sceptical kama atamaliza. Acha ujinga
Huna hoja inayopaswa kutolewa majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…