Uzi wako ni mzuri sana mkuu.
Umemshauri na kunikumbusha Mheshimiwa rais kwa staha na heshima sio kama hawa mapunguani wengine.
Naomba kujuzwa zaidi kwenye hiyo hoja hapo.
Mimi nijuavyo ni kwamba Rais anakuwa na ilani ya chama chake ambayo ndio alioitumia kuwashawishi WANANCHI. Narudia tena mkuu, kuwashawishi WANANCHI wamchague na wala sio wana CCM kama inavyodhaniwa ili wamchague.
Sasa Leo unaposema watu wa kumwambia ukweli rais ni wapinzani wake, hii imekaajee??
Kwahiyo aachane na ahadi (ilani) ya chama?? Ambazo wananchi ndio walizielewa na kumchagua au kukichagua chama chake?? Ili awasikilize wapinzani???