Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Hata kuchinja kuku si sahihi. Kuku pia wana haki ya kuishi.
 
Mama unajichoresha tu we fanya mambo yako bila kumhusisha Magufuli utaonekana tu, by the way hatujui unatupeleka wapi
 
Kabla hajaingia pia mgao wa umeme haukuwahi tulikuwa tunauona k.m historia
 
Yeye si alikuwa makamu wa Rais, alitoa ushauri gani? Aache unafiki
Hapo Sasa Ndiyo Utajua Siasa Lazima Uwe Ndumilakuwili Muda Wote


Mzilankende Unasemwa Huku!!
 
Rais wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano wa Wanasheria wa Africa Mashariki , amekiri wazi kwamba kitendo cha serikali ya Tanzania kupiga kiberiti vifaranga visivyo na hatia yoyote kutoka Kenya , haukuwa uamuzi sahihi.

Wakati unyama huo ukifanyika na kushangiliwa na Wanaccm wengi , Mh Samia Suluhu alikuwa Makamu wa Rais .

Chanzo : Mwananchi .

TOA MAONI YAKO
 
Rais Samia Suluhu anasimamia haki za wananchi na nchi pia anasimamia haki ata za viumbe hai pia kwaiyo haikua sahihi maana walikua na uwezo wa kuviludisha vifaranga vilikotoka
 
Mgao wa umeme na maji pamoja na gharama za maisha kupanda ndio changamoto kwa sasa wasitupoteze maboya, mambo ya vifaranga yalishapita yeye akaombe msamaha huko Kenya basi maana na yeye alihusika kwa huo ujinga kama hakupendezwa nao angejiuzuru.
 
wakati wa kutekeleza sheria kunachanganya sana, kwani sheria zetu zinasemaje?
 
Rais Samia Suluhu ameleta Suluhu kati ya Tanzania na Kenya upande wa biashara sasa Tanzania inanufaika zaidi endelea kuupiga mwingi mama
 
Ulikua ni zaidi ya upuuzi lakini sasa Rais Samia Suluhu anaendesha nchi kwa akili na sio nguvu
 
Mgao wa umeme na maji pamoja na gharama za maisha kupanda ndio changamoto kwa sasa wasitupoteze maboya, mambo ya vifaranga yalishapita yeye akaombe msamaha huko Kenya basi maana na yeye alihusika kwa huo ujinga kama hakupendezwa nao angejiuzuru.
Sasa umeme mvua ikinyesha wiki tu, hiyo agenda inawafia, 😄tafuteni ajenda nzuri,, hili la umeme ndani ya nwezi huu tu hali itakuwa stable
 
Toka juzi mama alipoingia Arusha mpaka leo umeme haujakatika.
Nashauri mama aendelee Kukaa Arusha mpaka mwisho wa mwaka
 
Kwa akili yako timamu unaamini kwamba kipindi cha Jiwe alikuwepo mtu gani wa kumshauri?!
Au uliwahi kusikia Jiwe ameshauriwa kitu na nani?
Sasa kama huwezi kutimiza majukumu yako si unajiudhuru tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…