Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Yeye si alikuwa makamu wa Rais, alitoa ushauri gani? Aache unafiki
Kweli alikuwa Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa sasa wa Chama chake ndiye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido. Vifaranga vilichomwa moto pale Namanga.......
Tumepitia mambo kadhaa magumu miaka michache iliyopita
 
Aliyechoma alitumia vigezo gani kufanya hivyo? Alichukuliwa hatua gani?

Cheo ni dhamana. Kuna tabia ya kujisahau na kutumia vibaya vyeo na madaraka tunayokabidhiwa
 
Vifaranga waliochomwa walipatikana na nini?
 
Na Chongolo alikuwa ndiye Mkuu wa Wilaya kule Longido

Mh Rais Rutto alianzia kwenye kuku na hadi leo ni mkulima wa kuku mkubwa sana Kenya. Siku akisema ili biashara ya Tanzania na Kenya ishamiri zaidi tunataka Mh KM angatuliwe inaonesha hiyo itawezekana na akimtuma CS Dualle afikishie huo ujumbe.
 
Akili nyingine ni ya ajabu sana, inakuwaje unachoma Moto viumbe hai bila huruma??? Hata kama mmiliki ameingiza kimakosa haikufaa apigwe faini ili siku nyingine afuate utaratibu!?

Hatuwezi kuunga mkono Jambo hilo!
Sheria ndiyo inasema hivyo na ni duniani kote usipofuata taratibu. Ndio maana wakati wa corona hata binadamu alikuwa anawekwa karantini kwanza. Magonjwa ya kuambukiza ndio sababu mkuu
 
Aendelee kujifananisha huku nchi ikiyumba
 
Kwenye hili Rais Samia yupo sahihi. Kila mwenye akili timamu alijua uamuzi ule ulikuwa ni ukichaa, na Dunia nzima iliiona Tanzania kama ni nchi ya watu wenye uwendawazimu.
Katika kusimamia sheria??
 
Anajua atawachota chawa wanaomchukia Magu. Mama anaupiga mwingiii pondea pondea Jiwe kutuliza hasira za wapenda dezo
 
Labda wangefanyaje?mbona vitu vya magendo vinavyoingia nchini vinateketezwa? Hao kuku wanaopitishwa bila kufuata utaratibu ikiwemo kuhakikiwa afya zao wakiingiza magonjwa hatari nchini nani atawajibika?sheria ifuate mkondo wake ...Peleka wanyama hai hata ulaya bila kufuata utaratibu uone kama havichomwi moto.hilo ni suala la usalama wa taifa....mapembe ya ndovu tunayoteketeza yanaleta faida gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Delila ameanza kuongea ya JPM
 

Bidhaa zenye ubora wa chini huchomwa tofauti hazina uhai na si viumbe vya Mwenyezi Mungu. Sasa maadamu tumeonea huruma viumbe vifaranga kwa minajili hiyo hiyo tuonee huruma viumbe Binadamu linapokuja suala hili hot la ughali wa maisha. Wenye viwanda naona bei wanapanga tu wanavyotaka wala hatuna hakika ni nguvu ya soko au ndio na wao wanafukia mashimo ya ile miaka 5 au la?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…