Rais Samia: Kama haumpendi Rais aliyeko, penda nchi yako

Rais Samia: Kama haumpendi Rais aliyeko, penda nchi yako

hamna ushahidi kwenye hili................na hata kama ipo hivyo ni kwa vile tuu Magufuli alimteua kuwa makamu wake na Maraisi wote wamekuwa wakiiamarisha mambo ya kwao hata kwa uchache tukumbuke hata Chato ipo vile kwasababu gani na ni ndani ya miaka mi5 ya kwanza ......ilishapendeza ,mpeni kijiji basi huku bara abadilishe kabila na ubini...........
Agombee moja kwa moja zenj......ili aitumikie kiroho safi, kwa nini kuvutana na wadanganyika akina ndugai...
 
Uyu mama ni dhaifu sana kila siku ana uongelea u Raisi tu bogus kweli
Kweli maisha yamekupiga! Usitafute mchawi umasikini wako ni akili zako na tafsiri zako. Mpaka anaye kutawala unamuona dhaifu.
Lofa katika kiwango chako uyu vs huyu! Hilo ni tatizo la kutoenda shule kabisa.
 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema urais sio mtu ni taasisi lakini kikatiba kunakuwa na mtu pale juu. Amewaambia Mawaziri kuwa kama hawampendi Rais aliyepo basi wapende nchi yao

Amesema hata kama haumpendi Rais Samia isiwe kigezo cha kupuuza mambo yote ambayo serikali inafanya. Ameruhusu watu kumchukia lakini sio kuchukia mambo ya serikali

Amewataka kuheshimu viapo vyao kwa kuwa wameapa kwa kushika vitabu vya Imani zao

Rais SSH jaribu pia uwapende Watanganyika wote.

Uwapende kama unavyopenda familia yako,unavyowapenda Wazanzibar. Utapendwa.

Chukua mikopo kwa weledi, kwa tahadhari.

Chapa kazi zaidi ya JPM, utapendwa na wengi. Acha kumtukana, kumdhalilisha kila siku kutumia watu wako.
 
Kwa Uzanzibari wake,kwa uislamu wake na Kwa kuwa na Mwanamke kawa Rais, nothing else.

Hizo ni sababu za kujihami tu, kufanikiwa kwa URAIS wake kutategemea jinsi atakavyotatua kero za wananchi!! So far wananchi wanalalamikia tozo; Kwani hizo tozo alizozileta kwenye miamala ya Simu, Magufuli alizozikataa ndio zinafanya Watu walalamike!

Nenda kakope lakini hiyo mikopo ilete nafuu kwa wananchi kwa kutolewa hizo tozo; sio mnakopa alafu bado mnawakamua wananchi kwa kuwaongezea tozo na makato mengine chungu nzima. Mikopo iwe kwa kuwapa wananchi nafuu ya maisha!!!

Mlisema mliweka hizo tozo ili kujenga madarasa hivyo kama hiyo ilikuwa Kweli tulitegemea baada ya kupata mkopo ule wa IMF na mkauelekeza kujenga madarasa basi zile tozo zingelisitishwa , unless mlikuwa mnawahadaa wananchi.!
 
Mama yetu is sensitive...anayoyasoma hasa huku mtandaoni, japo mengine ni mazuri na anayafanyia kazi lakini mengine yanamuumiza, wabongo tuwe na stara tunapo comment 😊😊😊😊🤭🤭🤭🤭
 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema urais sio mtu ni taasisi lakini kikatiba kunakuwa na mtu pale juu. Amewaambia Mawaziri kuwa kama hawampendi Rais aliyepo basi wapende nchi yao

Amesema hata kama haumpendi Rais Samia isiwe kigezo cha kupuuza mambo yote ambayo serikali inafanya. Ameruhusu watu kumchukia lakini sio kuchukia mambo ya serikali

Amewataka kuheshimu viapo vyao kwa kuwa wameapa kwa kushika vitabu vya Imani zao
naunga mkono hoja.
 
Watu wanamchukia yeye kwasababu ya mambo ya serikali.

Watu wakipenda mambo ya serikali, “automatically” wanampenda na yeye. Wakumchukia hawawezi kukosekana. Lakini hawatakuwa wengi kama mambo ya serikali yanapendwa.

Hapa rais anaweza kuwa anazungumza kwa “codes” kwamba kuna watu wanamchukia yeye binafsi kwasababu ambazo hazihusiani na mwenendo wa serikali anayoiongoza. Sikubaliani naye. Maana ni yale yale ya kutumia “gender card” pamoja na uzanzibari.

Hata kigezo cha rais kutaka ama kuomba kuchaguliwa tena, kinapimwa na jinsi ambavyo serikali imefanya mambo yanayowagusa wananchi.
Safi kabisa. Twasema hivi. Uchaguzi 2025 uwe huru na haki. Bi Tozo hapiti…
 
Haiwezekani kumtenganisha rais na urais katika hisia.

Kwa sasa yeye ndiye amevaa sura na umbo la taasisi ya urais.
 
Back
Top Bottom