Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Kumtukana mwizi sio suluhisho. Hata wacheza movie huwa wanatukanana afu wakishamaliza ku act wanalipwa na kila mtu kusahau alichotukanwa.

Dawa ya wezi ni raisi kuagizwa wakamatwe wafungwe na kutaifisha mali zao zote ili iwe funzo na mfano kwa wengine.

Kuwambia wajitasmini ni kuwapa njia nyingine ya kupiga kwa style ambayo wanajua itakuwa ngumu tena kujulikana.
Hapo pa kutaifisha mali zao ndo penyewe ukitaifisha kwa vigogo wa 5 hivi akili itaka sawa kwa wengine kinyume na hapo ujui amna kitu
 
Ripoti ya CAG sio hukumu ya Mahakama,ikithibitika hatua zitachukukiwa..

Kumbuka Rais Samia sio mtu wa mihemko,kukurupuka na ku loose temper kirahisi ,ukifanya hivyo anaweza umiza wengi.
A Hypocrite, Flatterer and dame Fool at Work.
 
Hapo pa kutaifisha mali zao ndo penyewe ukitaifisha kwa vigogo wa 5 hivi akili itaka sawa kwa wengine kinyume na hapo ujui amna kitu
Kweli mkuu kinyume na hapo itakuwa ni sawa na kumpigia ngoma chura acheze.
 
Hapo unazungumzia katiba mpya!
Binafsi naona vyama vyote Tanzania au Afrika vimeanzishwa kwa lengo kutafuna fedha za wananchi, ndomaana ukivichunguza hata uendeshaji wao ni wa upigaji upigaji.

Cha kufanya ni kuwa na wagombea huru ambao watagombea uongozi bila kupitia chama chochote cha siasa. Maana wanasiasa wote ni wezi, waongo na wanafiki.
 
V
Vyovyote vile ila 70% Magufuli aliendesha nchi kama Raisi
Rais anayeongoza kuiba mali ya nchi na kuua? Rais anayekandamiza katiba na kubana democracy? Hapana yule alikuwa kichaa na waliomuweka walikosea. Ila Mungu akaenda kwenye mode ya factory reset pale 17/ 03/ 21
 
Wewe ongea utakavyo, effectiveness ya raisi inaonekana kwenye ubora social services, infrastructures, uwajibikaji na uchumi wa wananchi at large. Kingine nchi yetu sio ya kibepari bali ni ya kijamaa na mfumo wa uendeshaji wa Magufuli ulikuwa of that type. Thus why waliolazimisha kuishi kibepari waliumia.
 
Binafsi naona vyama vyote Tanzania au Afrika vimeanzishwa kwa lengo kutafuna fedha za wananchi, ndomaana ukivichunguza hata uendeshaji wao ni wa upigaji upigaji.

Cha kufanya ni kuwa na wagombea huru ambao watagombea uongozi bila kupitia chama chochote cha siasa. Maana wanasiasa wote ni wezi, waongo na wanafiki.
Dah! Umejibu vizuri Sana sijui nani kawadanganya CCM pekee ndio tatizo
 
Wewe ongea utakavyo, effectiveness ya raisi inaonekana kwenye ubora social services, infrastructures, uwajibikaji na uchumi wa wananchi at large. Kingine nchi yetu sio ya kibepari bali ni ya kijamaa na mfumo wa uendeshaji wa Magufuli ulikuwa of that type. Thus why waliolazimisha kuishi kibepari waliumia.
Miradi Mingi kipindi chake ulienda kwa kasi tofauti na awamu zingine za Uraisi ni kwasababu ya usimamizi wake mzuri.
 
Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa raisi kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.
Yes ni kweli ila kabla hajachukuliwa hatua ni lazima kwanza ithibitishwe kwa ushahidi usiotia shaka ndipo hatua zichukuliwe!.
Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake raisi eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.
Hajashindwa na hashindwi, bali enzi za mabavu na kuwachukulia hatua watu kwa tuhuma tuu, zimepita!, sasa tuko kwenye enzi za uthibitisho na ushahidi usiotia shaka!
Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.
Hatukamati watu kwa tuhuma tuu, sasa ni mpaka uthibitisho!.
China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali.
Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.
Hizo nchi zote mbili ni udikiteta!, sisi huko tumeisha vuka tuko kwenye utawala wa sheria.
Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu,
Kwa mujibu wa sheria
kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.
Wakenya ni Wakenya na sisi Watanzania ni Watanzania!, Watanzania tuko kama Watanzania, hatuko kama Wakenya, sisi ni watu wapole , wastaarabu, watulivu, wapenda Armani na utulivu!
Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Pole sana, na wala usisikitike, huu ndio utawala wa sheria unavyotaka na unavyo fanya, na ni kuyavuna mabua, tumeisha yavuna sana!, msitake kuturudisha kule!.

P
 
Wewe ongea utakavyo, effectiveness ya raisi inaonekana kwenye ubora social services, infrastructures, uwajibikaji na uchumi wa wananchi at large. Kingine nchi yetu sio ya kibepari bali ni ya kijamaa na mfumo wa uendeshaji wa Magufuli ulikuwa of that type. Thus why waliolazimisha kuishi kibepari waliumia.
Huo ndiyo ujinga wa kutegemea mfumo wa mtu binafsi ndiyo uendeshe nchi badala ya mihimili ya nchi iliyojengwa kwenye Katiba bora.

Bado Samia ni kiongozi bora kwa vile CAG amesoma ripoti kwa uhuru bila kuogopa. Magufuli alimfukuza Prof Assad kwa kuonyesha upotevu wa Tsh 1.5 Trillion. Lakini nyie devil worshippers bado akili zenu zimeshikwa na Dikteta tuliyemfukia Chato
 
Raisi ambaye anaangalia wezi wanaiba ndio raisi ambaye wapuuzi mnamtaka.
 
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa raisi kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake raisi eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anaeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe na kurudishwa katika mikono ya wananchi.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali.
Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Raisi na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu, kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Na kuvuna mabua ndio kunakofanyika kwa sasa !! Nchi hii ukiwaambia mimi sikuzowea kufukuzana fukuzana na kufokeana fokeana hapo ujue umewawashia taa ya kijani mijizi ya pesa za umma !!
 
Yes ni kweli ila kabla hajachukuliwa hatua ni lazima kwanza ithibitishwe kwa ushahidi usiotia shaka ndipo hatua zichukuliwe!.

Hajashindwa na hashindwi, bali enzi za mabavu na kuwachukulia hatua watu kwa tuhuma tuu, zimepita!, sasa tuko kwenye enzi za uthibitisho na ushahidi usiotia shaka!

Hatukamati watu kwa tuhuma tuu, sasa ni mpaka uthibitisho!.

Hizo nchi zote mbili ni udikiteta!, sisi huko tumeisha vuka tuko kwenye utawala wa sheria.

Kwa mujibu wa sheria

Wakenya ni Wakenya na sisi Watanzania ni Watanzania!, Watanzania tuko kama Watanzania, hatuko kama Wakenya, sisi ni watu wapole , wastaarabu, watulivu, wapenda Armani na utulivu!

Pole sana, na wala usisikitike, huu ndio utawala wa sheria unavyotaka na unavyo fanya, na ni kuyavuna mabua, tumeisha yavuna sana!, msitake kuturudisha kule!.

P
Acha kuleta porojo. Yaaani unataka ushahidi gani hata kama kuna premafacie evidence?
 
Back
Top Bottom